Tanzania yashindwa kwenye kesi, yaamuriwa kulipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 260

We subiri tu...

Hata Lissu kasema huu mkataba ni lazima uvunjwe hata tulipe pesa kiasi gani ni sawa tu...

Magufuli ndiyo alitumia maguvu kuvunja mamikataba haya ya hovyo lakini kimsingi alikuwa sahihi. Sema
sasa hakuna uzalendo na tumerudi kule kule. Hawa hawa wanaotushinda mahakamani wanaweza kurudi na wakasaini tena mikataba kama ile ile aliyoivunja Magufuli...Hovyo tu!

 
Nakazia tu
 
Kwenye utawala wa kufuata Sheria na kanuni aliturudisha nyuma sana kipenzi chetu wanyonge
 
Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Uingereza na Tanzania (BIT)

Ule wa mkataba baina ya serikali ya Tanzania na 'nchi' ya Dubai kuhusu bandari nao una mashaka makubwa

 
ndio maana hatuwaamini wanasheria wetu wanaoendeshwa na wanasiasa hasa hawa wa serikali.

Ndio maana tunashindwa kuwaamini hata kwenye hili la DPworld.
 
shenzi type kwenye dp world tutauza hadi wajukuu na bado tutadaiwa
 
Mwendazake alitufanyia mabalaa yya ajabu. Na bado wengine.
Kiini cha tatizo hapa ni ccm na serikali zake. Kama unaona Mwendazake alifanya vibaya, alikuwa ni moja ya rangi za hicho chama.

Aliyeko sasa hivi ni balaa...JPM cha mtoto!
 
Hakuna watu wajinga Dunia hii kama watu wa CCM , yaani tahadhari zote mna pewa bado hamuelewi, watalaam, wapinzani, wananchi wenye nia njema wana jitahidi kuwaeleza na kuwa onyesha kuwa hii mikataba mibovu lakini hayasikii, kila mwaka kuna hasara ya mikataba hii, hivi akili zao sijui zime gotea wapi, maana sio kwa ujinga huu.
 
Mwendazake alitufanyia mabalaa yya ajabu. Na bado wengine.
Mnamsingizia Magufuli haya ni mazagazaga ya Kikwete na genge lake!! Samia lazima awe mwangalifu sana na Rostam ambae kisha muingia ; akifanya mchezo Rostama atamuangamiza huyo mwanae Abdul kama alivyomungamiza marehemu Balali!!! Rostam sio mtu wa kumuweka karibu atakuliza!! Amekwisha muingiza mkenge Samia sijui utatokaje?

Fedha za maendeleo mtaishia kuwalipa wajanja fidia kutokana na upumbuvu wenu kusaini mikataba bila kuielewa!! Ona sasa hiyo invoice nyingine ya faint ya mabilioni ya shilling imekuja huku mnaongeza bei ya cement muwalipe mabwana zenu!!
 

Wana ccm wote wanaishi bila UBONGO na ndio maana miaka yote ya utawala wao ni hasara kwa nchi!!!
 
Ni hivi,Magufuli hakuwahi kuwa na nia ya kuwasaidia watz kwa ujumla.Mfano ni KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE.Kikwete aliwaangalia raia na kuwatafutia njia za kuwafanyia wepesi katika kupiga hatua kimaendeleo.Ujio wa Dangote ulilenga kuwasaidia raia katika kuleta makazi bora kwa kila raia,alikiruhusu kiwanda kizalishe Saruji ya viwango vyote ili kuwawezesha raia wa vipato vya kawaida pia kumudu gharama ya kununua Saruji kwa ujenzi wa makazi.
Kiwanda cha Dangote kilifanya Saruji huku mikoani kuuzwa kwa Tsh12000 kwa mfuko.
Magufuli alipoingia madarakani alimzuia Dangote kuzalisha Saruji ya viwango vyote na kumtaka abaki akizalisha Saruji ya viwango vya kimataifa tu ambayo mfuko mmoja ni kati ya Tsh 25000 hadi 35000.
Leo hii hakuna tena Saruji ya Dangote madukani huku mikoani,bei ya Saruji kwa sasa ni kati ya Tsh 18000 hadi 22000.

Sasa kwa mfano huu unaweza kusema Magufuli alikuwa akiwajali raia na maisha yao?.
Huo uzalendo mnaouimba toka kwake ni upi hasa?.
Kwa hiki alichokifanya kwa Saruji ya Dangote,alikifanya kwa manufaa ya nani?.
Tunawezaje muamini mtu wa aina yake katika malengo ya kuivunja mikataba hii tukiangalia mfano wa kiwanda cha Dangote?.
 
Bado Dp watakuja kujichotea pesa,mkataba mbovu sana utakaomtesa rais ajaye
 
Aliyeingia ndio mpumbavu, aliyevunja ndio alitumia akili, huwezi kuingia mkataba wa kipuuzi usio na maslahi kwa taifa halafu uje kumlaumu aliyeuvunja, wewe ndie utumie akili.
Wewe ndio huna maarifa,mkataba wowote mahali popote,wakati wowote ukiuvunja,ukisitisha,ukiuondoa kwa namna yoyote lazima ile kwako.Tumia maarifa.
 
Hili nalo wapewe DP World. Mwarabu ana pesa ndefu. Hili ni dogo sana kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…