Tanzania yasitisha vibali vya usafirishaji wa mahindi nje ya nchi

Umenikumbusha yaan. China wana coops nzuri sana mpaka za maziwa. Kimsingi isiangalie wacheche watakaonunua unga bei juu. Maisha ya mkulima wa chini yajaliwe kwa kumuwezesha kupata competitive price popote pale
 
Tushawazoea na huyo magufuli wenu, kila kitu "magufuli magufuli, utadhani yeye ndio muanzilishi wa hili taifa
 
Upuuzi mtupu. Mimi nimeplan kuuza yangu niliyolima ifikapo december na january na nitauza popote ninapotaka. Hakuna aliyenisaidia kulima.
Ni jambo la kustaajabu sana.

Sasa mkulima wa mahindi kama wewe una mahindi yako na unategemea kuyauza upate pesa umepewa muongozo gani ili ufanikishe biashara yako ?

Kama serikali imezuia uuzaji wa mahindi nje.
Je itanunua mahindi ya wakulima wanayotaka kuyauza ?

Kwahiyo mahindi ya wakulima yaozee ghalani kwao?
Au wanataka yagawiwe bure kwa wenye njaa ?

Kama serikali inazuia kuuzwa mahindi nje basi itoe muongozo kwa wakulima na wafanya biashara wa ndani ili biashara iendelee.

Hili zao la mahindi lina ukakasi mwingi sina.
Kwa wakulima wa kibiashara.
 
Wewe ni mjinga kabisa. Tumelima kwa gharama zetu halafu kwenye kuuza mnatuletea upumbavu.
Yaan huyo anaongea ushuzi. Anajua hata kulima huyu mtu. Anajua taabu ya kulima huyu. Mkulima ana majanga makubwa yanayogawanyika seem tatu. Haki ya hewa, uzalishaji na masoko. Apo kwenye masoko kuna changamoto sana kuliko seem ingine yaan. Asa wewe jipendekeze kama unajua hata tope la mbuga likoje
 
Acheni upumbavu nyie akina john na ccm. Tunalima kwa gharama halafu kuuza mnaleta ushetani.
Umesahahu kuwa serikali inatoa ruzuku kwenye mbolea? Ruzuku ni sehemu ya gharama ambayo umesaidiwa na Serikali
 
Point kubwa ni hii. Nchi ina neema ya rutuba na wachapakazi.
Hoja ni kuongeza uzalishaji na sio kuzuia biashara.
Kilimo ndio uti wa mgongo wa nchi na yakitengenezwa mazingira mazuri ya hii biashara nchi itaingiza pesa nyingi na kuacha namna zinazo wakera wananchi.
 
Nchi ilifunguliwa na sasa mnaifunga tena?🤣🤣🤣
 
Nimpe pongezi ndugu mkulima mmoja aliyejenga nyumba na godown la kisasa kwa kuuzia wakenya mahindi kwa bei nzuri, hongera, ulitembea na fursa.

SERIKALI IJALI WAKULIMA, KAMA MAZINGIRA HAYARUHUSU WAUZE KWA WENYE UWEZO WA KUNUNUA KWA BEI NZURI BASI SERIKALI INUNUE KWA BEI NZURI HALAFU WAO NDO WAPELEKE SOKONI KWA BEI NDOGO AU WAWAWEZESHE WAKULIMA KWA PEMBEJEO NA GHARAMA ZA SHAMBA.
 
Yaani hawa jamaa wapo kwenye mamlaka lakini akili hawana. Mwaka huu mvua zilikata maeneo ya kule hanang na maeneo mengine pia. Mahindi yakakauka shambani.

Serikali haikutoa msaada wowote kwa wakulima. Nilikuwa nategemea kuvuna kwenye heka 40 angalau kuanzia magunia kumi kwa heka lakini nimevuna magunia matatu kwa heka. Gharama iliyoingia haiwezi kurudi kamwe kama sitauza kwenye soko zuri.

Halafu anakuja mpumbavu mmoja aliyeongezewa mshahara na anakula posho anasema hakuna kuuza nje. True idiots.
 
Umesahahu kuwa serikali inatoa ruzuku kwenye mbolea? Ruzuku ni sehemu ya gharama ambayo umesaidiwa na Serikali
Acha kuongea mambo usiyoyajua. Mkulima gani anapewa ruzuku? Bei za ruzuku wananunua wenye mitaji mikubwa ambao ni suppliers halafu wanawauzia wakulima kwa bei ya soko.

Mwaka huu mvua zilipokatika na mahindi kukaukia shambani serikali ilitoa ruzuku?
 
Nashauri liundwe baraza la Wakulima wa Mahindi tu.
Na wajumbe wawe wakulima wa Mahindi.

Ili kuratibu namna bora ya uzalishaji na uuzaji wa zao hilo.
Nina uhakika Mahindi ni zao lenye faida kubwa kwa mkulima na Taifa kwa jumla.
 
Tuliwaeleza muda mrefu mavuno kidogo wakabisha na mwaka huu mvua sio za kutosha
Nashangaa watu kupongeza uamuzi wa kupunguza bei ya petroli na kutaka sasa wafanyabiashara wapunguze bei ya bidhaa zao karibu zote. Hivi karibuni wafanyabiashara toka nchi jirani walifika Jijini Dodoma wakakomba maharage ya njano karibu yote katika masoko yaliyopo hapa Jijini. Awali bei ya kilo moja ilikuwa sh. 2500. Kwa sasa kilo moja ya maharage hayo imepanda hadi kufikia sh. 3500 kwa kilo moja. Amen, amen nawaambieni tusitegemee bei kushuka chini ya hapo hadi mavuno ya msimu ujao.
 
Tuu leti!
Tujiandae kwa njaa tu hamna namna.
 
Habari ya uwongo hii
 
Kuna sehemu nilimueleza kuwa huenda hujui unachozungumza. Bei ya 2017 ilikuwa chini Sana, mbona hawakukata tamaa? 2019 bei ilikuwa kubwa sana na kwa mujibu wa maelezo yako basi waliapta faida. 2019-2020 Bei ikawa chini, 2020-2021 Bei ikawa nzuri kidogo. Hayo ndio mahindi bei huwa haipo stable kutokana na sababu nyingi. Uache uongo
 
Umeandika pumba, na huyo mkulima aliyejenga godown ili awauze wakenya akili Hana au umeweka chumvi.

Huwezi kuanzisha godown kwa kuwauzia wakenya ikiwa bei ya soko ipo hivyo awe mkenya aee mganda awe mtanzania wote wananunua Bei hiyo.

2019 bei ya mahindi ilikuwa nzuri sana awe mkenya mtanzania au mganda wote walinunua kwa bei hiyo iliyokuwepo sokoni, 2020 bei ikaporomoka awe mkenya, mganda au mtanzania wote walinunua kwa bei hiyo ndogo.
 
We jamaa hii id yako nishaijua, huwa nasoma hoja zako mwanzo tu nacheka halafu siendelei kutaka kujua umeandika nn.....Una tatizo la kuanza na Unnecessarily harsh tones.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…