Kwa nini wasaini bila kutushirikisha sisi wananchi?kipindi zanzibar walipotaka kuchimba mafuta waliyaondoa kwenye mambo ya muungano kwa kuhofia tanganyika itanufaika na rasilimali yao ya mafuta.kwa nini kwa sasa tena wanarudisha?Au kwa kuwa wameona maliasili tanganyika ni nyingi ndiyo maana wamesaini hiyo mukataba ya kimangungo?.Tunataka tanganyika yetu siyo upuuzipuuzi wa mikataba isiyona kichwa wala miguu.
 
Hii ndiyo kazi kubwa inayofanyika.
Sasa sina shaka tena, naomba tu ifanikiwe, tena kwa haraka.
Imeshafanikiwa kwasababu SSH amesaidia sana kuwashtua Watanganyika!
Nani anasimamia rasilimali za Tanganyika?

Hayo makubaliano , nani amesimamia masilahi ya Tanganyika?
 
Swali la kujiuliza
Hivi wale Wabunge wa Zanzibar pale Dodoma waanajadili vipi bajeti ya madini ya Tanganyika ikiwa tuna makubaliano ya nchi mbili! Hivi hamuoni kizunguzungu hapa

Ni sawa na Wabunge wa Zanzibar kwenda Dubai halafu wakirudi wanasema haliwahusu

Sasa kama madini ni kunafaisha pande mbili, mbona bandari yenye manufaa zaidi SSH hakuwashirikisha

Smell rat! Watanganyika stand up kwa nchi yenu. Makubaliano ya madini na eneo lisiloweza kuchoma mkaa ni kutaka uhalali wa kutumia rasilimali zenu Zanzibar
 
..Znz walifanya jitihada kubwa mpaka wakaondoa mafuta kwenye masuala ya muungano.

..Sasa sidhani kama kuna uwezekano wa wao kurudisha mafuta yao kwenye mikono ya muungano.
Walifanya hivyo walipodhani kuwa wana mafuta. Lakini mpaka sasa hayajapatikana ya kuweza kuvunwa. Sitashangaa wakidai kuwa mafuta/gesi asilia zirudishwe kwenye Muungano ili wafaidike na yaliyopatikana Tanganyika.

Amandla...
 
Juzi Pascal ulitoa mada, wakati watu wakiitaja Tanganyika ulilaumu wengi hawaelewi somo ;a uraia kwa sababu tuna Tanzania Leo serikali ya Tanzania imesaini makubaliano na serikali ya Zanzibar. Je ni kweli wananchi hawaelewi somo la uraia au tuna viongozi vilaza.
 
Muungano huu unachangamoto,, vipi serikali ya Tanganyika hatuioni hapo. Kama imekubali au imegoma
 
Sisi Watanganyika ni Majuha. Tunaendeshwa na wazanzibari milioni moja.
 
Isomeke Tanzania visiwani sio Tanzania Zanzibar

Jina la Znz litokomezwe kama lilivyotokomezwa la Tanganyika yetu kuimarisha Muungano
 
Sielewi kabisa.
Mzanzibar ni Mtanzania, sasa huo Mkataba umekaaje? Ndani ya Tanzania kuna nani mwingine hata ipelekee ufanyike mkataba na Mzanzibar ambaye ni Mtanzania.
Yaani Mbeya nayo inasaini Makubaliano na Wizara ya elimu au Wizara ya Kilimo au ya Sayansi na Teknolojia?
Hilo li mchi kumbe lina Majuha kiasi hicho? Halafu na yenyewe yapo tu yanaenzi Ujuha!
 
Akili ndogo tu, mapato ya madini yanatakiwa kwenda zenj, wakati madini sio ya muungano, sasa kwanini wasifanye madini kuwa suala la muungano? baadae utasikia kwa mujibu wa makubaliano mapato ya madini yatagawanya nusu kwa nusu! Lisu akisema kuna matope kwenye jumba jeupe mnasema katukana
 
Walioungananao niTanganyika hiyo Tanganyika yenyewe haionekani inayoonekana ni Tanzania kwa hiyo zanzibar kasaini hayo mashirikiano na huyo anaeonekana ambae ni Tanzania

Sent from my ATU-L31 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…