Seif Sharif Hamad alifundishwa na Abood Jumbe Mwinyi elimu ya sekondari katika sekondari ya King George VI ambayo leo inaitwa Lumumba iliyopo mjini Zanzibar, Jumbe ni mmoja ya wasomi wa mwanzo wa Zanzibar alikuwa na shahada ya chuo kikuu cha Makerere, Jumbe alimteua Seif kuwa waziri wa elimu ,baadaye akamteua kuwa waziri kiongozi wa Zanzibar.
Seif aliiba nyaraka muhimu kuhusu serikali tatu alizokuwa ameandaa Mzee Jumbe kupitia mwanasheria mkuu wa Zanzibar ,Seif akazipeleka kwa Nyerere ndio ukawa mwisho wa Mzee Jumbe kuwa rais wa Zanzibar na alifukuzwa urais wa Zanzibar 1984.
Seif alimsaliti Mzee Jumbe ambaye alikuwa anataka muungano wa serikali tatu.
Pumzika kwa amani Mwalimu Mzee Abood Jumbe Mwinyi.