TANZIA: Bi. Asha B. Makame afariki dunia

TANZIA: Bi. Asha B. Makame afariki dunia

Mwanadamu kumbuka siku za kuishi hapa Duniani ni chache, Hakika sisi ni Mavumbi na Mavumbini tutarudi.
 
poleni wafiwa katika kipindu hiki kigumu
 
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Zanzibar, Asha Bakari Makame amefariki dunia leo huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Taarifa zilizothibitishwa na wanafamilia pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo visiwani Zanzibar, Salama Aboud Talib zinasema kiongozi huyo alikuwa ametoka nchini India kwa matibabu.

Naibu Katibu huyo amesema kuwa baada ya Makame kutoka India kwa matibabu, alipitia Dubai kwa mwanae, mahali ambapo mauti ilimkuta mapema leo.

Mbali na wadhifa huo ndani ya UWT, Asha Bakari Makame ameshawahi kuwa Waziri wa Wanawake na Watoto katika serikali ya awamu ya tano visiwani Zanzibar iliyokuwa chini ya Rais Salmin Amour.

Mbali na wadhifa huo, mwanasiasa huyo ameshawahi kuwa mwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliwahi kuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

Source Mwananchi.
 
View attachment 318027

Too sad. Nimemfahamu huyu Mama wakati wa BMK. Tutamiss mipasho yao. RIP
 
Anazikwa lini?, wamzike haraka maana taratibu za dini yao haziruhusu kuchelewesha mazishi
 
P.M.U (Pumzika Mahala Unapostahili)

Anyway kifo sio kitu kizuri lakini huyu mwanamke alinikera sana wakati wa bunge la katiba ya kihuni ya magamba
 
Kwa wanaekumbuka huyu mama alivyo ropoka na kukashifu wajumbe wenzake bunge. La katiba lazima tutoke hapo na jambo la kujifunza. Siongei kwa ubaya ila mlio pewa dhamana na wananchi mnatakiwa kujua siku zetu za kuishi hakuna hazijulikani na tutaondoka saa yoyote ila Tanzania itabaki.
Hivyo tuheshimu ya walio wengi tutoe uchama.
 
Inna Lilah wainna ilayh rajiuun. Allah amnyooshee safari yake
 
ZANZIBAR TULIIIPATA KWA KUPINDUA NA NYINYI KAMA MNAITAKA MUITAWALE ZANZIBAR MJE KUPINDUA NCHI HATUTOI KWA VIKARATASI NA KUPINDUA HAMUWEZI...... HAYO NDIO MANENO YAKE ALIYOYASEMA HUYU MAREHEMU WAKATI WA UHAI WAKE SASA LEO KAPATA NA YEE WA KUMPINDUA MUNGU MLIPE KILE ANACHOSTAHILI HAPA DUNIANI TUNAPITA NA SAA YA KUONDOKA WALA HATUIJUI
 
Kila nafsi ita onja mauti....na hesabu ni kwa karatasi ya kulia na kushoto...
 
Mkuu, CCM haina tabia ya kusema kweli. Ukisema kweli unasemwa kuwa ni mpinzani. Nadhani umenielewa

Mzee Tupatupa
Sio CCM tu ila ata ww pale unapoenda ovyo kwa maslahi yako ukiambiwa ukweli hutapenda, ata Chagadema hawapendi kuambiwa ukweli kama walivyoambiwa na Zitto katika issue ya ukaguzi wa.mahesabu jamaa akaitwa msaliti, Dr. Slaa alibaki na msimamo wake kuwa Lowassa hafai kuwa rais aliitwaje? Kisa tu leo yupo chama chao…!! Tusiwe wanafiki
 
View attachment 318027

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Zanzibar, Asha Bakari Makame amefariki dunia leo huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Taarifa zilizothibitishwa na wanafamilia pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo visiwani Zanzibar, Salama Aboud Talib zinasema kiongozi huyo alikuwa ametoka nchini India kwa matibabu.

Naibu Katibu huyo amesema kuwa baada ya Makame kutoka India kwa matibabu, alipitia Dubai kwa mwanae, mahali ambapo mauti ilimkuta mapema leo.

Mbali na wadhifa huo ndani ya UWT, Asha Bakari Makame ameshawahi kuwa Waziri wa Wanawake na Watoto katika serikali ya awamu ya tano visiwani Zanzibar iliyokuwa chini ya Rais Salmin Amour.

Mbali na wadhifa huo, mwanasiasa huyo ameshawahi kuwa mwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliwahi kuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

Naona amepinduliwa hata kabla Jussa hajamfikia!! Tumwogope Mungu wakati tunazungumza, yaani huyu mama wakati anazungumza bunge la katiba ni kama hatokufa milele!! Ni kama Z'bar ilikua yake binafsi! Namnukuu "Z'bar hatuitoi hatuitoi, hatuiti, labda kwa mapinduzi". Hii kiburi yote ya nini? Unakuwa na kiburi namna hii, bishana na kifo basi!! Mbona kinakuja na kinakuchukua na hubishan popote! Tumwogope Mungu sana

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Malipo ni hapa hapa duniani pumnzika bibi
 
View attachment 317991

Aliyewai kuwa Mwakilishi wa bunge maalum la katiba na Waziri wa wanawake na watoto Zanzibar na Makamu wa Jumuiya ya wanawake wa CCM ametangulia mbele ya haki huko Dubai baada ya kurejea matibabu yake huko India.

Mwenyeenzi Mungu amsamehe makosa yake na amlaze mahali pema. Amin
huwezi kumuombea msamaha
tusidanganyane,.....
nawala mahai pa kuiweka roho yake kwamba mahali pema au lahh,..
Mungu ndo anayejuaa matendo yake,..sisi tuseme kamaliza
safari duniani basi Mungu afanye maamuzi yake,....nasisi tujipange na safari hiyo
kwa kutenda mema mbele za Mungu mwenyezi,....bas
 
Huyu sawa tu...Ingawa wote tutakufa...ila wakitangulia maharamia kama hawa inakuwa ahueni huku duniani
Bado utasikia pengo la marehemu ni vigumu kuzibika. Kama vile aliyokuwa anatamka na kufanya yalikuwa mema. Tufike mahali tuwe wakweli, kama jambazi kafa tunasema kifo cha marehemu ni faraja kwa raia wema! Sio unafiki msibani
 
Back
Top Bottom