Unaposikiliza mahubiri/mafundisho yakakuchoma moyo wako kwa maana ya kwamba ukajiona una hatia,kwa mkristo anayejitambua hii inamanisha uombe toba na ubadilike.Hii inamanisha ni nafasi Mungu amekupa utengeneze njia zako,kwa bahati mbaya kizazi hiki cha nyoka,badala ya kutengeneza kinamchukia mwalimu/mhubiri.
Kila mtu atatoa hesabu ya matendo yake aliyoyafanya wazi na aliyoyafanya gizani/mafichoni.Nyakati za mwisho watu watakuwa ni wenye mizaha,hili lipo sana,kwenye mambo serious watu wanaweka comedy.
Elewa kwa nini upo hai mpaka leo,kuna siku zinakuja walio hai watatamani kufa bila kujua wataenda wapi,mbinguni au kuzimu.
Tuna ugonjwa wa Corona unasumbua dunia,kila mtu anaomba abaki hai,je unataka ubaki hai ili uendelee kuiba,kufanya uzinzi,kusema uongo na mengine ambayo ni chukizo kwa Mola?Fikiria Mungu akikuuliza leo kwa nini unataka uwe hai,je una sababu za msingi za kumshawishi akuache uishi?
Wengi kuna mengi hawayajui na wanaenda tu,kama ungejua nini kiko mbele yako,usingeishi hayo maisha unayoishi.
Heri mtu yule ambaye atakufa akiwa anamtumikia Mungu wa kweli,kama kuna sehemu alikosea atajuana na Mungu.Je tujiulize mimi na wewe ambao leo tuko hai,tumefanya nini katika kuujenga ufalme wa Mungu?
Kuna watu hapa, mbingu zinawatambua kama Wachungaji,Wainjilist,Mitume na Manabii wa ukweli siyo waigizaji waliojaa zama hizi,lakini bado uko huko uliko?Je ulishafikilia pumzi ya uhai ikiondolewa leo,wewe utaenda wapi as a christian?Kwa sababu sehemu za kwenda ni mbili na tunazichagua wakati huu tukiwa hai hapa duniani.Right now aidha mtu yuko kwenye ufalme wa Mungu au ufalme wa shetani.Je wewe ni wa ufalme upi?
Chukua hatua,kuna kitabu fulani nilisoma kinaonyesha kipindi hiki ni cha mavuno. Mungu anavuna walio wake na Shetani naye anavuna walio wake.Je wewe utavunwa na nani?
Be serious and take responsibility for your life.