Kiama Kikikaribia ,basi watu wote wema wataanza kupukutika kwa spidi kubwa na hatimae watabaki watu waovu watupu.
Hapo wataanza kufanyiana mambo ya kifedhuli ikiwemo kuuwana ovyo, uasherati,wizi na dhulma,na uwongo kuwa ndio nyimbo ya taifa,mapato ya haramu ,na ulaji wa Riba wazi wazi.
Hapo Kiama kitawakuta watu wa aina hiyo wakiwa kwenye Uovu wao huo na starehe zao hizo chafu na wingi wa kulewa.
Majumba ya dini yatageuzwa Madanguro ya Mabintiwarembo na vijana watanashati wakiimba na kucheka huku wakiwa wingi wa matamanio na uzinzi ,usanii wa Maneno, huku watu hao wakimkebehi Mungu kwa kuwa ni waovu.
Miziki na madisko na Nyimbo za kila aina zitaimbwa humo wakiiminisha kuwa eti ndio sala sahihi kwa staili za Mipigo ya kidunia. Sio tena vile vinanda na vinubi.
Hapo Kiama kitawahalallikia watu wa aina hizo.