Mwanajamiione, sikubali wala sikatai mawazo yako, ila naomba tu nikukumbushe kitu kimoja, nitakupa na mfano kua, mungu ha bipiwi. Yaani ukim beep mungu, lazima akupigie. Inategemea kilio chako kikoje wakati wa kum beep. Huyu mke wa Secky alimlilia sana mwenyezi mungu juu ya mahusiano ya mumewe na huyu mtoto. Mungu akasikia kileo, akafanya kile alichoona kitamuweka huyu mama kwenye amani. Nakupa mfano mmoja tu, japo nina mingi. Kuna ajali moja iliwahi kutokea barabara ya moshi-arusha miaka kadhaa iliyopita, akafa mama na watoto wake wane au watano, sikumbuki vizuri, baba akapona lakini alilazwa. sina hakika kama unajua story behind this tragic accident? wanandoa hawa walikua hawana uelewano mzuri, mara nyingi walikua na kesi kanisani kujaribu kusuluhisha, issue ni baba kuchepuka na kuzaa hovyo. alikua na pesa zake na maduka mengi moshi na arusha. kila siku wanapomaliza kesi zao kanisani kwa mchungaji/padre, yule neno lake lilikua "sitaki kufa niache watoto wangu wateseke, bora mungu anichukue siku moja na wanangu". Alikua akiomba hivyo kila wakati, na mungu vile hajaribiwi, alitekeleza mama alivyotaka. Ile ajali ilimuondoa yeye na watoto wake wote kama alivyokua akiomba. Padri/mchungaji ndio alichaguliwa na wanafamilia kum face yule baba akiwa hospitali kumuambia familia yake is no more, maana kutwa alikua anataka kujua wanaendeleaje. Hivyo, pamoja na kwamba tunaondoka duniani kwa ahadi, lakini kuna ahadi nyingine inabidi mwenyezi mungu azi adjust kutokana na matokeo.