TANZIA: Mwanahabari mkongwe, Bi Sarah Dumba afariki dunia ghafla akiwa Njombe

TANZIA: Mwanahabari mkongwe, Bi Sarah Dumba afariki dunia ghafla akiwa Njombe

Asante mama kwa kutuburudisha enzi hizo hatuna television wala radio binafsi yoyote ....R.I.P Sarah Dumba kipenzi cha watu enzi hizo ...
 
Habari nizilizonifikia hivi punde Mwana Mama mahiri katika fani ya utangazaji na baadae kuzawadiwa ukuu wa wilaya amefariki dunia nusu saa iliyopita.

Nawasilisha.
 
Ni kweli hizi habari zimeletwa hapa tokea jana usiku
 
Oh!. Mama wa watu!. Pole sana kwa familia, ndugu na jamaa. Mungu atusaidie tuliohai bado tuache uovu na kuishi maisha safi mbele za Mungu, tukijua kwamba tumekumbushwa ipo siku ya kufa ambayo haijulikani. Kufa ni mara moja na baada ya kufa ni hukumu. Kila mtu atahukumiwa sawa sawa na alivyoishi akiwa hai duniani. Baada ya kufa hakuna kubadili maandishi ya maisha ya mtu. Ibada za wafu hazifanyi mwovu awe msafi huko aliko baada ya kufa. Maandalizi ya umilele wetu ni hapa hapa duniani.

Narudia tena, kusema "Kufa ni mara moja na baada ya kufa ni hukumu". Hakuna tena kuombewa toba nk. baada ya kufa.

MUNGU IFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU. WAPE FARAJA WATOTO WAKE, NDUGU YA JAMAA. JINA LAKO BWANA NA LIBARIKIWE. AMIN!
 
Ooh nakumbuka hadithi ya ua jekundu....Mungu awape faraja wafiwa.
 
Aiyaaaaaaaaaa, yani namkumbuka huyu mama enzi za RTD, Anyway nadhani si kweli.
Ngoja tusubiri.
 
Sarah Dumba ndiye alikuwa anasimulia hadithi za mama na mwana kwenye redio R.T.D. Mzaliwa na amekulia Kigamboni Dar es salaam. R.I.P.
 
Back
Top Bottom