impongo
JF-Expert Member
- Feb 18, 2015
- 8,764
- 7,758
Pole Sana kabla sijanunua nitahangaika kuweka mazingira Kwanza Asante sana
Kaka utaratibu ni kununua kwanza then unaomba kibali cha kumiliki silaha. Mimi nipo kwenye hatua hizo lakini ni ngumu sana siku hizi na kuna urasimu sana. Nimenunua silaha toka July pale Tanganyika Rifle, nikajaziwa fomu pale nikaenda kwa kamati ya ulinzi na usalama ngazi ya mtaa na kata walinitembelea nyumbani kukagua na kurithika kisha walisaini na kuniidhinishia. Mwezi huohuo nikawakilisha kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya. Nilifika polisi Wilaya nikajaza fomu , nikaenda polisi makao makuu nikachukuliwa alama za vidole na kurudisha fomu wilayani, zikaenda kwa afisa usalama wa wilaya kazipitia kwa sasa zipo chini ya mkuu wa wilaya fulani alkini amezikalia hadi leo. Anapaswa apange tarehe ya mimi kuitwa kuhojiwa laini hadi leo hajafanya hivyo ni miezi mitano sasa. Ikitoka hapo inabidi iende mkoani napo nadhani itakaa mwaka mzima. Ingawa nafahamu umuhimu wa vetting kuhakikisha kuwa anayemiliki silaha anastahili bila kuiweka silaha kwenye mikono isiyostahili ila muda inayochukua kulifanya hilo inasikitisha sana ni muda mrefu sana. Mimi nimetumia tshs 6,500,000 kununua silaha tu, pesa zimelala pale Tanganyika Rifles sijapata kibali na wala sitegemei kupata chini ya mwaka mmoja bila sababu za msingi. There is something wrong somewhere!!!!