Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Pole Sana kabla sijanunua nitahangaika kuweka mazingira Kwanza Asante sana
Kaka utaratibu ni kununua kwanza then unaomba kibali cha kumiliki silaha. Mimi nipo kwenye hatua hizo lakini ni ngumu sana siku hizi na kuna urasimu sana. Nimenunua silaha toka July pale Tanganyika Rifle, nikajaziwa fomu pale nikaenda kwa kamati ya ulinzi na usalama ngazi ya mtaa na kata walinitembelea nyumbani kukagua na kurithika kisha walisaini na kuniidhinishia. Mwezi huohuo nikawakilisha kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya. Nilifika polisi Wilaya nikajaza fomu , nikaenda polisi makao makuu nikachukuliwa alama za vidole na kurudisha fomu wilayani, zikaenda kwa afisa usalama wa wilaya kazipitia kwa sasa zipo chini ya mkuu wa wilaya fulani alkini amezikalia hadi leo. Anapaswa apange tarehe ya mimi kuitwa kuhojiwa laini hadi leo hajafanya hivyo ni miezi mitano sasa. Ikitoka hapo inabidi iende mkoani napo nadhani itakaa mwaka mzima. Ingawa nafahamu umuhimu wa vetting kuhakikisha kuwa anayemiliki silaha anastahili bila kuiweka silaha kwenye mikono isiyostahili ila muda inayochukua kulifanya hilo inasikitisha sana ni muda mrefu sana. Mimi nimetumia tshs 6,500,000 kununua silaha tu, pesa zimelala pale Tanganyika Rifles sijapata kibali na wala sitegemei kupata chini ya mwaka mmoja bila sababu za msingi. There is something wrong somewhere!!!!
 
nenda kituo chochote cha polisi kilicho karibu na wewe hata p[ost utapewa utaratibu naamini hapo haipiti dk 20 utakuwa umekiona kituo cha ndugu zetu polisi
 
Naomba mwenye ufahamu vigezo jin
umiliki silaha maduka yanayouza Bei na Aina ya silaha nzuri Bastoral inayobebeka kirahisi na ya kisasa walau risasi 15
Duh.!
Ukihitaji bunduki kubwa nistue nna Gobore 1 la kienyeji ambalo hata ukikosa risasi linatumia vipisi vya nondo au golori za chuma
Pia nina Ak-47 ina mkanda wa risasi 36
Hizi zote nilirithishwa na marehemu babu alikuwaga mjeshi wale wa zamani.
Hata ukihitaji za kukodi nakodisha karibu.
 
Hizo hapana Mimi nataka halali
 
Pole Sana kabla sijanunua nitahangaika kuweka mazingira Kwanza Asante sana
It is okay, ni kuwa mpole tu, ila chunga asije mtu akakwambia utoe pesa ili akuharakishie, hakuna kitu kama hicho, kwa kuwa utaratibu uko very systmatic hakuna mtu mmoja anayeweza kufanya maamuzi. siku hizi wapo strict kwakuwa silaha nyingi zinaishia mikononi mwa maharamia hivyo wako makini sana. Mimi ninavijua vyombo vyote vya usalama lakini nime stuck nasubiri nakuwa mpole.
 
nenda kituo chochote cha polisi kilicho karibu na wewe hata p[ost utapewa utaratibu naamini hapo haipiti dk 20 utakuwa umekiona kituo cha ndugu zetu polisi
Nimepata maelekezo ya kutosha nimeelewa kilichobakia ni kuanza process
 
It is okay, ni kuwa mpole tu, ila chunga asije mtu akakwambia utoe pesa ili akuharakishie, hakuna kitu kama hicho, kwa kuwa utaratibu uko very systmatic hakuna mtu mmoja anayeweza kufanya maamuzi. siku hizi wapo strict kwakuwa silaha nyingi zinaishia mikononi mwa maharamia hivyo wako makini sana. Mimi ninavijua vyombo vyote vya usalama lakini nime stuck nasubiri nakuwa mpole.
Asante Sana nitafuatilia kwa umakini bahati nzuri nilipo na makazi Kuna ofisi zote mtaa Hadi mkoa na wananifahamu huenda hichi kitakuwa kigezo Cha mimi kufanikiwa haraka
 
Back
Top Bottom