Wakati mwingine siyo kupinga kila kitu. Mzazi anapozaa na kumtunzq mtoto anawekeza fao la uzeeni. Hivyo ni haki ya Mzazi kuvuna matunda ya alichopanda.Huyu mbunge haelewi mantiki rahisi tu kwamba mzazi ni lazima amhudumie mtoto kwa sababu mzazi anachagua kuwa na mtoto, lakini mtoto kumhudumia mzazi haipaswi kulazimisha kwa sababu mtoto hajachagua kuzaliwa, mtoto naye atawajibika kwa mtoto wake, ikiwa atachagua kuwa na mtoto?
Hiyo mantiki ndogo tu imemshinda?
Utoto unawasumbua! Sisi tulipokuwa shule, nia yetu kubwa ilikuwa kutafuta uwezo wa kuendeleza nyumbani. Sisi ndiyo tulibadilisha maisha ya wazazi wetu Vijijini . Tukawajengea nyumba nzuri hata kuwanunulia magari. Tuna kumbukumbu maana wazazi wetu walihangaika sana kutusomesha. Waliuza mashamba yao, wakauza Mifugo ili hapo baadaye tuwafae na tumetekeleza.Ulitumwa kumwagia ndani?
Si ungevaa kondomu.
Au usingezaa kabisa.
Wewe kama umeshindwa kutafuta hela za kujihudumia mwenyewe uzeeni. Subiri ufe tu.
Usiwatwike watoto wako, ujinga wako.
Kila mtu atawajibika na maisha yake, hadi anaingia kaburini.
Wakuhudumiwa ni mtoto tu, from 0 to 18 years.
Baada ya hapo kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.
Wazazi wako walikuwa wajinga ndio maana waliwazaa nyie kwenye umaskini, mkahangaika na mkapitia shida.Utoto unawasumbua! Sisi tulipokuwa shule, nia yetu kubwa ilikuwa kutafuta uwezo wa kuendeleza nyumbani. Sisi ndiyo tulibadilisha maisha ya wazazi wetu Vijijini . Tukawajengea nyumba nzuri hata kuwanunulia magari. Tuna kumbukumbu maana wazazi wetu walihangaika sana kutusomesha. Waliuza mashamba yao, wakauza Mifugo ili hapo baadaye tuwafae na tumetekeleza.
Mtoto akifa je?Wakati mwingine siyo kupinga kila kitu. Mzazi anapozaa na kumtunzq mtoto anawekeza fao la uzeeni. Hivyo ni haki ya Mzazi kuvuna matunda ya alichopanda.
Pole sana! Watoto wapo pengine kukuzidi umri.Wazazi wako walikuwa wajinga ndio maana waliwazaa nyie kwenye umaskini, mkahangaika na mkapitia shida.
Hao wazazi wako walioshindwa kujitengenezea maisha bora na kubadilisha maisha yao wenyewe ni malimbukeni.
Na wewe zaa watoto wako, halafu subiri wakue waje wabadilishe maisha yako. Kama mwendo ndio huo.
Una mentality ya kimaskini kwa vile umekulia kwenye umaskini. Unadhani ni sifa kukulia Vijijini.Pole sana! Watoto wapo pengine kukuzidi umri.
Tatizo kubwa ni mitoto ya kiume iliyozaliwa na kukulia mijini. Kijana yeyote aliyezaliwa kama mimi, akamaliza darasa la saba Kijijini na kwenda mjini kusoma sekondari, hawezi kuwasahau wazazi na kuendeleza kwao.
Malezi hata mjini hapo. Inategemea na namna unavyo wafundisha watoto wako.Issue ni malezi, maana Vijijini tulikuwa tunaona jinsi wazazi walivyokuwa wanatuhangaikia. Na baba ndiye mkuu wa kaya.
Kwa nini hukuzalia watoto wako kijijini wakapitia shida ulizopitia?Mitito yetu tuliyoizalia mijini, inaona jinsi mama anavyoifanya kaya yenu kuwa kaya ya ndugu zake kiasi baba anakuwa kama houseboy. Nadhani ndo maana mnakuwa na mawazo finyu.
Kwa nini unategemea watoto waje wakutunze uzeeni?Kusema za Ukweli uzoefu wangu unaoneaha, kijijini mtoto wa kiume Mali, ila mjini mtoto wa kike Mali . Kwa sasa usipozaa mtoto Angalau mmoja wa kike, mwanaume umeliwa. Mitoto ya kiume, mawazo yao kutuma nauli kwa minungaembe. Lakini kimjini, mtoto wa kike hamtupi baba yake. Mpaka litakapooa ndipo linajua umuhimu wa Baba.
Mtoto akishafika umri wa 18 years na yeye anaanza kuchakarika na maisha yake.Nikupe Mfano mmoja. Nina watoto wawili, dume na jike. Siku moja dume ambaye ni first born, akanipa ushauri kuwa nijitahidi kuwekeza kwa ajili ya uzeeni I maana nikizeeka lazima nijitunze ila kazi yake ni kumtunza mama yake. Kwa vile Nilijua ni akili kama zenu wengi humu, nilimkubalia kwa sharti moja kuwa nami asinitegemee kifedha ili niweke akiba.
Usidhani humu kila mtu ni mtoto.Mfano wa pili ni binti ambaye siku moja mwaka jana alinitumia message kuwa walikuwa wanajadiliana na mume wake na kufikia makubaliano kuwa kama nikizeeka nikaishiwa nguvu, wapo tayari kunichukua wanilee.
Mkikua ndipo mtaona umuhimu wa kutunza wazazi wenu, pengine itakuwa too late, washatangulia mbele ya haki
Hiyo hoja ya mzazi kuzaa na kumtunza mtoto kama fao la uzeeni ni ya kijinga, ya kimasikini, ya kuachwa.Wakati mwingine siyo kupinga kila kitu. Mzazi anapozaa na kumtunzq mtoto anawekeza fao la uzeeni. Hivyo ni haki ya Mzazi kuvuna matunda ya alichopanda.
Nia yangu ni kukuonesha kuwa kuzaa na kulea watoto ni kuweka akiba ya uzeeni. Hakikisha mtoto unamlea na kumpata elimu bora, malezi bora, mwandalie Mazingira ya kujiajiri baadaye ili mwisho wa yote akutunze.Una mentality ya kimaskini kwa vile umekulia kwenye umaskini. Unadhani ni sifa kukulia Vijijini.
Halafu si kila kijana aliyetoka kijijini akaja mjini, hukumbuka wazazi wake.
Vijana wengine wakishafika mjini, hupotea mazima.
Malezi hata mjini hapo. Inategemea na namna unavyo wafundisha watoto wako.
Kwa nini hukuzalia watoto wako kijijini wakapitia shida ulizopitia?
Kwa nini unategemea watoto waje wakutunze uzeeni?
Hujui kwamba na wao watakuwa na familia zao zinazo hitaji matunzo?
Sasa kwa nini uwa ongezee watoto wako mzigo mwingine?
Mtoto akishafika umri wa 18 years na yeye anaanza kuchakarika na maisha yake.
Masuala ya kutegemeana tena, yanapungua.
mtasapotiana tu kwenye shida kubwa.
Sio kuleta ule utegemezi wa kila kitu.
Usidhani humu kila mtu ni mtoto.
Wewe sio mtu mzima pekee hapa JF.
Kufa kila mtu atakufa.
Utunzwe, usitunzwe kifo ni kwa wote.
Jukumu la kutunzana ni lako wewe na mke wako.
Usiwabebeshe watoto wako mzigo wa kukulea wewe.
Na wao wana familia zao za kuzilea.
Mnakosea sana! Tunafuga Ng’ombe ili tupate samadi na Maziwa tuuze, tupate fedha. Tunazaa watoto, tunahangaika kuwalea, kuwapeleka shule, kuwajengea uwezo wa kutafuta pesa ili baadaye, watutunze.Hiyo hoja ya mzazi kuzaa na kumtunza mtoto kama fao la uzeeni ni ya kijinga, ya kimasikini, ya kuachwa.
Kwa sababu.
1. Hakuna uhakika kwamba mtoto atakuwapo mzazi akiwa mzee, inawezekana mtoto akatangulia kufa.
2. Hakuna uhakika kama mtoto atakuwa karibu na mzazi na kuwa na interest ya kumjali.
3. Hata kama mtoto atakuwa karibu na kujali, hakuna uhakika kwamba mtoto atakuwa na uwezo wa kumhudumia mzazi. Inawezekana mtoto ndiye akawa anahudumiwa.
4. Dhana nzima ya kuzaa mtoto na kumhudumia utotoni ili naye aje kumhudumia mzazi uzeeni ni ya kizamani, ni ya kufanya taasisi adhimu ya familia kuwa ni biashara ya utumwa, biashara ya nipe nikupe, nifae nikufae.
5. Kuna wazazi wegine hawastahili kabisa msaada wa watoto, mfano mzazi hajajishughulisha kabisa na malezi ya mtoto, huyo naye utalazimisha ahudumiwe na mtoto? Utaweka kiwango gani kusema huyu anastahili na huyu hastahili? Ni haki kumlazimisha mtu amhudumie mzazi wake mwenyewe?
6.Kuna mifumo mingi mizuri ya watu kujiwekea mafao ya uzeeni na kuacha kutegemea watoto.
7. Watoto wana wajibu wa kujipanga kuhudumia watoto wao, mkiwapa kazi ya lazima ya kuhudumia wazazi mnawapa kazi mbili mbili zitawazidi.
8. Watoto hawakuamua kuzaliwa, wala hawakuamua kuzaliwa na wazazi wao, hivyo hawana wajibu wa kuwatunza wazazi.
9. Wazazi ndio wanaoamua kuzaa watoto, wao ndio wana wajibu wa kuwahudumia watoto.
10. Wafrika acheni ubinafsi wa kuangalia familia kama chanzo cha uchumi. Kila kitu cha kifamilia mnataka kukifanya cha uchumi, mnataka watoto wasio na mbele wala nyuma wahudumie wazee, mnataka kuuza binti zenu kwenye ndoa na kupata mahari. Acheni hizi biashara za utumwa.
Wewe ndiye unakosea kumfananisha mtu na ng'ombe. Unamfananishaje mtoto wako na ng'ombe?Mnakosea sana! Tunafuga Ng’ombe ili tupate samadi na Maziwa tuuze, tupate fedha. Tunazaa watoto, tunahangaika kuwalea, kuwapeleka shule, kuwajengea uwezo wa kutafuta pesa ili baadaye, watutunze.
Angalia Mifano hai ya familia ambazo ziliwekeza kwa watoto zikitegemea Kivina kutoka kwao kama Hospital ya Kairuki, Nakitte etc. Ona Wahindi kama MO na baba yake Dewji ambavyo aliinvest kwa Mohamed na anafaidi matunda ya mwanae yeye akila pension. Acheni mawazo finyu
Nikupe sasa mfano halisi. Hivi Unajua huko moshi kaya isiyokuwa na mtoto nje ya moshi inaishi katika hali ngumu?Wewe ndiye unakosea kumfananisha mtu na ng'ombe. Unamfananishaje mtoto wako na ng'ombe?
Na inaonekama huwezi kuelewa somo langu kwamba, mzazi akiwekeza vizuri kwa mtoto, huyo mtoto akikua ataondoka katika mnyororo wa kuzaana kama watumwa atajiwekea mafao ya uzeeni.
Hao uliowataja kina Kairuki na wengine, hao hawakuzeeka na kutegemea watoto wao, walivunja hiyo chain ya kutegemea watoto.
Mimi baba yangu ana assets za millions of US dollars, more than 5 million US dollars by a conservative guess.
Leo mtu kama mimi kumsaidia baba yangu ni kama suala lakuonesha upendo tu. Kwa sababu huyo ni mtu anayeongelea kutoa shilingi milioni 100 kanisani kama sadaka ya shukurani, mambo yake yako poa.Hana shida ndogo ndogo.
Sasa, mzazi kama huyo, amepita shaka ya kuwa tegemezi kwa watoto wake, kawalea watoto, na watoto tunalea watoto, tumeona somo kwamba mzazi anapaswa kujiandaaa.
Mzazi alikuwa ananunua real estate sana miaka hiyoo ambayo vitu viikuwa cheap, sasa hivi ana portfolio kubwa.
Huyu mzazi ni mfano wa kuigwa wa Waafrika wanaojiondoa katika biashara ya utumwa ya kuzaa ili kutegemea watoto uzeeni.
Tujenge utamaduni wa kujitayarisha wenyewe kwa maisha ya uzeeni, watoto wasipewe masharti ya kutusaidia. Kama wanasaidia, wasaidie kwa hiyari. Kulazimisha jambo hili la upendo ni kulichakachua, kuliondolea maana yake ya upendo.
Pia, msaada wa kulazimishana ndiyo mwanzo wa watoto kuua wazazi wao kwa sababu wanawaona mzigo na wamelazimishwa kuwasaidia.
Wazazi wajiandae kwa maisha ya uzeeni, kama kusaidiwa kuwe kwa hiyari si kwa lazima.
Hamuelewi wapi?
Mweleze Kiranga Hoja dhaifu kuwa mara huwezi jua mtoto atakuwa vipi. Hiyo itakuwa bad investment. Kwani ni wangapi wameanzisha Biashara ikafa? Risk ni nyingi Lakini haiwezi zuia mtu kuinvest.Haihitaji sheria mtoto mwenye utimamu lazima atamtunza mzazi wake
Wewe unaeleza dunia ya Waafrika ilivyo, ilivyo leo.Nikupe sasa mfano halisi. Hivi Unajua huko moshi kaya isiyokuwa na mtoto nje ya moshi inaishi katika hali ngumu?
Soma papers za caldwell kuhusu sababu za waafrika kuwa na watoto wengi, ni fao la uzeeni. Acheni mawazo ya kimaskini, kuzaa na kulea ni kuwekeza.