Tarimba Abbas ataka sheria ya lazima watoto kutunza wazazi wao

Tarimba Abbas ataka sheria ya lazima watoto kutunza wazazi wao

Anieleze nini wakati mimi ndicho nilichosema hicho?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Mimi nakwambia hili si jambo la kuhitaji sheria, tena mkiliwekea sheria mnaliharibu, hata wanaotunza wazazi kwa hiyari itakuwa kama wanatekeleza sheria tu.

Huelewi wapi?
 
Mpumbavu tu huyu ni wa kumpuuza.
Kuna watu wengi wana kasumba ya kukimbilia kwenye sheria, kila tatizo wanakimbilia kwenye sheria.

Tatizo la kisiasa, wanakimbilia kwenye sheria.

Tatizo la kiuchumi, wanakimbilia kwenye sheria.

Tatizo la kiutamaduni, wanakimbilia kwenye sheria.

Matatizo haya ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, hayatatuliwi na sheria.

Ukitengeneza uchumi vizuri, hakutakuwa na wazee wengi wanaotegemea watoto, na kutakuwa na watoto wengi wanaohudumia si wazee wao tu, bali mpaka wazee wasio na familia za kuwajali.

Sasa mtu jobless uchumi wake mbaya, kwa sababu uchumi wa nchi mbaya, unamlazimisha kwa sheria amtunze baba yake, akishindwa utafanyaje? Utamfunga? Utamtoza faini?

Ukimfunga ndiyo baba yake atapata msaada? Ukimtoza faini atailipaje wakati hana hata pesa ya kumtunza baba yake?

Hili ni tatizo la kiuchumi.

Serikali imeshindwa kujenga uchumi mzuri wa kuwapa watu ajira na kipato na mafao ya uzeeni.

Inawatupia kazi watoto.

Serikali imeshindwa kutoa ajira za maana kwa watoto.

Inataka kutoza damu kutoka kwenye jiwe.

Jiwe haliwezi kutoa damu.
 
Wewe unaeleza dunia ya Waafrika ilivyo, ilivyo leo.

Mimi nakuonesha tatizo la dunia ya Waafrika ilivyo leo.

Kwa nini huelewi kuwa kuzaa ili kutegemea watoto wakutunze wakikua ni ulofa?

Katka dunia hii ya leo ambayo kuna mambo mengi sana, unategemea vipi mtoto akutunze uzeeni wakati mtoto naye anakuwa na maisha yake, anahama, ana matatizo yake, na yeye nafikiria maisha yake ya uzeeni yatakuwaje.

Huoni kuw ahii ni model moja ya kijimajima, kishambashamba, haifanyi kazi katika dunia ya leo?
Tatizo una mawazo finyu. Tatizo mnafikiria kutunza Mzazi ni kumgharamia Mzazi kifedha. Hapo ndipo mnakosea.
 
Anieleze nini wakti mimi ndicho nilichosema hicho?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Mimi nakwambia hili si jambo la kuhitaji sheria, tena mkiliwekea sheria mnaliharibu, hata wanaotunza wazazi kwa hiyari itakuwa kama wanatekeleza sheria tu.

Huelewi wapi?
Hakuna haki bila wajibu. Sheria ni muhimu kwani itaondoa utapeli ambapo MZAZI Ame invest kwa mtoto, mtoto akikua anakutapeli
 
Tatizo una mawazo finyu. Tatizo mnafikiria kutunza Mzazi ni kumgharamia Mzazi kifedha. Hapo ndipo mnakosea.
Huko kote nishafikiria.

Hata zaidi ya kifedha, kuhudumia mzazi ni suala la upendo mkubwa sana linatakiwa kufanywa kwa hiyari, si kwa kulazimishwa kisheria.

Unamlazimishaje mtu asiyepatana na mzazi wake amhudumie? Si ndiyo mwanzo wa kumuua huo?

Huelewi wapi?
 
Nakubaliana nawe kwa 100% mkuu.
Exactly.

Kuna watu wengi sana wanataka kuhudumia wazazi wao lakini hawawezi hata kumudu kujihudumia wao wenyewe.

Sasa hao unawatungia sheria kuwalazimisha wahudumie wazazi wao ili iweje?

Wape fursa ya kufanya kazi uone kwanza.
 
Mbunge wa Kinondoni (CCM), Tarimba Abbas amesema Serikali haioni haja ya kuweka sharti la kisheria la watoto wakubwa kuwatunza wazazi wao wasiojiweza.

Akizungumza Bungeni Leo Jumatano Januari 28,2025 Tarimba amesema katika mataifa mengine kuna sheria za lazima kwa watoto kuwalea wazazi wao lakini Tanzania ina sheria ya lazima kwa wazazi kuwalea watoto, hivyo akaomba ipelekwe haraka bungeni sheria hiyo ili iwalazimishe watoto kuwatunza wazazi wao. Huku akipendekeza pia Serikali ikajifunze hilo kwenye mataifa yanayotumia sheria hiyo namna inavyofanya kazi.

Zaidi: Mbunge Ndakidemi ataka kutungwe sheria ya kuwalazimisha watoto kuwatunza wazazi wao wakiwa wazee

Hii ni mara nyingine tena, hoja hiyo kuibuka bungeni, kwani katika Bunge la 12, hoja kama hiyo iliibuliwa na aliyekuwa Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba ambaye alitaka itungwe sheria kwa ajili ya kuwabana watoto wawatunze wazazi wao.

Kweli kabisa...Mimi mwanangu bilionea lakini anijalia kabisa baba yake kisa nna vijibanda uchwara vya Kodi na wake wanne
 
Hakuna haki bila wajibu. Sheria ni muhimu kwani itaondoa utapeli ambapo MZAZI Ame invest kwa mtoto, mtoto akikua anakutapeli
Mzazi ana wajibu wa kumhudumia mtoto, kwa sababu mzazi ndiye aliyeamua kumzaa mtoto.

Mtoto hana wajibu wa kumhudumia mzazi, hili ni suala la hiyari. Kwa sababu mtoto hajaamua kumzaa mzazi, amejikuta kazaliwa tu.

Mtoto naye atakuwa na wajibu wa kumhudumia mtoto wake, kwa sababu huyo ndiye aliyeamua kumzaa.

Una wajibu wa kumhudumia yule ambaye umeamua kumzaa. Yule ambaye umejikuta tu umezaliwa naye bila hata kuomba kuzaliwa huna wajibu wa kumhudumia, unaweza kumhudumia kwa hiyari tu. Huyo alitakiwa mwenyewe kujiandaa na maisha ya uzeeni.

Huelewi wapi hapo?
 
Kweli kabisa...Mimi mwanangu bilionea lakini anijalia kabisa baba yake kisa nna vijibanda uchwara vya Kodi na wake wanne
Sasa umekuwaje na wake wanne bila ya kujipanga kujitegemea kwenye maisha ya uzeeni?
 
Sasa umekuwaje na wake wanne bila ya kujipanga kujitegemea kwenye maisha ya uzeeni?
Hawa ni mama zake lazima atoe huduma! Mimi mbona nimemlea tangu mchanga,na magodoro yangu kibao kaozesha maana alikuwa kikojozi mashuhuri utotoni.
 
Hii sheria ni nzuri, watoto nao watunze wazazi kama wao walivyotunzwa wakiwa wadogo. Utakuta kuna wazee wanageuka ombaomba huku wakiwa na watoto wala bata hawajali wazazi wao. Umri unapokuwa mkubwa mzee hawezi tena kukimbiakimbia kufanya mishe za kupata mkate, huo ni umri wa kupumzika na kula shushu za watoto
Nitajie nchi Tano zenye sheria hiyo kama hazipo ni kwanini?
 
Nia yangu ni kukuonesha kuwa kuzaa na kulea watoto ni kuweka akiba ya uzeeni. Hakikisha mtoto unamlea na kumpata elimu bora, malezi bora, mwandalie Mazingira ya kujiajiri baadaye ili mwisho wa yote akutunze.
Huyo mtoto akifa kabla yako, huko uzeeni utalelewa na nani?
 
Huyo mtoto akifa kabla yako, huko uzeeni utalelewa na nani?
Una mawazo ya kimaskini wewe. Halafu nadhani katika maisha yako, hujawahi kujiajiri bali kuajiriwa.

Kujiajiri ni investment na ukiwekeza kuna risk ya kupoteza, siyo kila mwekezaji anafanikiwa ila mwekezaji haachi kujaribu mpaka afanikiwe.

Kujibu swali lako, ni kuwa akifa bahati mbaya. Na mwekezaji huwa na plan B. C etc

Kusema za ukweli kama ningekuwa kijana, ningehakikisha nina watoto 20, wavulana 2 wa kuzugia na 18 wasichana. Nikahangaika nao wote mpaka PhD level. Wakaingia katika family business. Kwenye hao mabinti zangu nisingekosa angalau 2 wa kunitunza uzeeni.
 
Kuna watoto wana ajira/wamejiajiri lakini hawasaidii wazazi wao, wanasema hawataki ujamaa.
 
Back
Top Bottom