Tarimba Abbas ataka sheria ya lazima watoto kutunza wazazi wao

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Kinondoni (CCM), Tarimba Abbas amesema Serikali haioni haja ya kuweka sharti la kisheria la watoto wakubwa kuwatunza wazazi wao wasiojiweza.

Akizungumza Bungeni Leo Jumatano Januari 28,2025 Tarimba amesema katika mataifa mengine kuna sheria za lazima kwa watoto kuwalea wazazi wao lakini Tanzania ina sheria ya lazima kwa wazazi kuwalea watoto, hivyo akaomba ipelekwe haraka bungeni sheria hiyo ili iwalazimishe watoto kuwatunza wazazi wao. Huku akipendekeza pia Serikali ikajifunze hilo kwenye mataifa yanayotumia sheria hiyo namna inavyofanya kazi.

Zaidi: Mbunge Ndakidemi ataka kutungwe sheria ya kuwalazimisha watoto kuwatunza wazazi wao wakiwa wazee

Hii ni mara nyingine tena, hoja hiyo kuibuka bungeni, kwani katika Bunge la 12, hoja kama hiyo iliibuliwa na aliyekuwa Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba ambaye alitaka itungwe sheria kwa ajili ya kuwabana watoto wawatunze wazazi wao.

Mbunge wa Kinondoni (CCM), Tarimba Abbas amesema Serikali haioni haja ya kuweka sharti la kisheria la watoto wakubwa kuwatunza wazazi wao wasiojiweza.

Akizungumza Bungeni Leo Jumatano Januari 28,2025 Tarimba amesema katika mataifa mengine kuna sheria za lazima kwa watoto kuwalea wazazi wao lakini Tanzania ina sheria ya lazima kwa wazazi kuwalea watoto, hivyo akaomba ipelekwe haraka bungeni sheria hiyo ili iwalazimishe watoto kuwatunza wazazi wao. Huku akipendekeza pia Serikali ikajifunze hilo kwenye mataifa yanayotumia sheria hiyo namna inavyofanya kazi.

Zaidi: Mbunge Ndakidemi ataka kutungwe sheria ya kuwalazimisha watoto kuwatunza wazazi wao wakiwa wazee

Hii ni mara ya pili hoja hiyo kuibuka bungeni, kwani katika Bunge la 12, hoja kama hiyo iliibuliwa na aliyekuwa Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba ambaye alitaka itungwe sheria kwa ajili ya kuwabana watoto wawatunze wazazi wao.
Is this level of stupidity taught or natural?
 
Hii sheria ni nzuri, watoto nao watunze wazazi kama wao walivyotunzwa wakiwa wadogo. Utakuta kuna wazee wanageuka ombaomba huku wakiwa na watoto wala bata hawajali wazazi wao. Umri unapokuwa mkubwa mzee hawezi tena kukimbiakimbia kufanya mishe za kupata mkate, huo ni umri wa kupumzika na kula shushu za watoto
 
Huyu mbunge haelewi mantiki rahisi tu kwamba mzazi ni lazima amhudumie mtoto kwa sababu mzazi anachagua kuwa na mtoto, lakini mtoto kumhudumia mzazi haipaswi kulazimisha kwa sababu mtoto hajachagua kuzaliwa, mtoto naye atawajibika kwa mtoto wake, ikiwa atachagua kuwa na mtoto?

Hiyo mantiki ndogo tu imemshinda?
 
Sheria za kijinga jinga kama hizo zitawaibua wazazi wa hovyo kwa kasi .
 
Muswada wa kitahira kama huu ukipitishwa nakuambia wahuni wote wataanza kufyatua mitoto kama tofali lengo waje kulelewa uzeeni .

Hiyo sheria sio kabisa ,nawaza leo kuna wazazi watoto wao wasipowatumia hela ni ugomvi vipi sheria ikiwapa nguvu kudai hiyo haki mbona vijana watafia jela wazee
 
Inabidi ipitishwe na sheria kali , kama hauna uwezo wa kumjengea mtoto mazingira mazuri ya kufanikiwa ni marufuku kuzaa.
 
Upuuzi mtupu,
Hili taifa lina safari ndefu sana kwa aina ya vihoja vinavyoendelea kwenye bunge la kuchongwa na CCM.
 
Hii sheria ni nzuri, watoto nao watunze wazazi kama wao walivyotunzwa wakiwa wadogo. Utakuta kuna wazee wanageuka ombaomba huku wakiwa na watoto wala bata hawajali wazazi wao. Umri unapokuwa mkubwa mzee hawezi tena kukimbiakimbia kufanya mishe za kupata mkate, huo ni umri wa kupumzika na kula shushu za watoto
Wee msaidie mzee wako, tusipangiane matumizi
 
Is this level of stupidity taught or natural?

Huu ujumbe una wenyewe, ujinga mwingi ulianza hivi baadae ukawa sheria.

Unakumbuka "mafao wa spouses"? Ilianza hivi hivi, leo hii ni sheria
 
Back
Top Bottom