Uchaguzi 2020 Tarime: Tundu Lissu ampiga marufuku Kassim Majaliwa kufanya kampeni, Yadaiwa anavunja maadili ya uchaguzi


Kama ni kizunguzungu wamekipata. Kila kona wanavurunda, alafu tume imekaa kimya kama vile hawaoni.
Mambo yamepamba moto. Ni mwendo washeria na siasa. Sasa huyu vyote anaviweza. Kamatia hapo na ongeza makali kidoo. HAPA NI MWENDO WA KANYAGA TWENDE TU.

Watajitetea anatekeleza majukumu yake ya kazi kiserikali, wakati huo ni kijani kitupu na chopa inayotumika ni hile iliyokodiwatoka kule--------.

Mahera hiyo kamati ya maadili ina meno kwa wapinzani tu au ndo maagizo toka juu?
 
Kweli kabisa
 
Ndo maana nikashangilia Lissu kuitwa na Tume.
 
Kwamba Lissu ndiye peke yake anajua tafsiri ya sheria? Kama nawe unaamini hivyo iweje ahamasishe wapiga kura kuingia barabarani iwapo hatatangazwa mshindi?
Kwahiyo akishinda halafu asitangazwe unataka afanyeje? Bila shaka inajua kabisa kwa sheria zetu rais akitangazwa na tume hakuna mahali popote utakapokwenda kukata rufaa. Usijifanye hamnazo kwa sababu ya ushabiki wako. Kwanza hajasema yeye atangazwe akishindwa ila akishinda kusiwe na kigugumizi cha kumtangaza vilevile.

Jitahidi kuushirikisha ubongo wako.
 
Majaliwa anatembea jimbo kwa Jimbo na akifika kwenye Jimbo mwenyeji wake nimgombea wa ubunge wa Jimbo husika.
Inawezekana mgombea ubunge wa jimbo jingine kwenda kumpigia kampeni mgombea wa jimbo jingine?
Kiongozi wa Chama kwenda kumpigia kampeni mgombea wa jimbo jingine.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Tumefikia patamu sasa, ni dk ya 15 tu ya mchezo mambo ndiyo yanazidi kunoga mnogage! Twende Lissu twende !!
 
Amesema "Kikatiba" Waziri Mkuu haruhusiwi kutumia cheo chake na resources za Serikali kufanyia kampeni zake binafsi au za mgombea wa udiwani, ubunge au urais.
Je maana yake hata JPM, kama Rais, nae asifanye hivyo?
Mazoea yana tabu kidogo!
 
Si kweli. Anakwenda kama mjumbe wa kamati kuu
 

Nani kawakataza?
 
Nyani haoni kendezake, mbowe si ni kub ana hadhi ya waziri mkuu kivuli
Sheria inazungumzia Mawaziri, Wakuu, wa Mikoa na Wilaya ........... KUB hayuko kwenye hilo group!!
 
Tatizo lipo hivi, Je anaweza kuihakikishia Tume kwamba anapokwenda mikoani anaachana na uwaziri Mkuu na anakwenda kama kada na Mjumbe wa kamati kuu? Je hii inawezekana?

Kama akisema yeye bado ni Waziri Mkuu na nakwenda kutimiza majukumu yake hilo ni sawa, lakini je huko kuwa haongelei masuala ya kumwombea JPM kura?
 
Lissu The Greatest
Lissu nilimwamini kwamba ni NGULI pale tu alipowafundisha watu Sheria kwamba UGAIDI hadi uitwe ugaini lazima uhusishe watu zaidi ya wawili - wakati kale ka Clip ketu ambako kangepita ilikuwa CDM ifutwe kakawa na sauti za watu wawili.

Lissu ni darasa tosha la hata wana Lumumba kujichotea weredi tena bila malipo.
 
Returning officer ni nani kwa mujibu wa hii sheria?Na je,katika ngazi ya uraisi, kuna returning officer mwenye mamlaka ya kupanga/kupokea ratiba ya mikutano ya wagombea uraisi au kuidhinidsha watu wa kumpigia kampeni mgombea uraisi?

Kwa maneno mengine,mtu mwenye wadhifa wa returning officer, anatakiwa/ana uhalali wa kisheria wa kupewa taarifa za nani atampigia kampeni mgombea uraisi katika eneo lake?
 
Wewe humuoni anavyofanya; anakagua na kuzindua miradi kwa mwamvuli wa Waziri Mkuu halafu hapo hapo anajigeuza mjumbe wa kamati kuu ya CCM kupiga kampeni!
 
Ile dhana ya Great Thinker kwa wana Jamii Forum inapotea kabisa maana yanatoka majibu kama ya Facebook. Mleta uzi kauliza sheria inasemaje kuhusu Kassim Majaliwa kumpigia kampeni JPM? Nimeona ni kawoli tu ndo kaweza kutoa jibu. Wanasheria tuisaidieni, imekaaje hiyo?
 
Wewe ni mwalimu mzuri sana wa grammar, sasa mbona humfundishi bosi wako baba Jeska???
Hadi anakimbia vikao vya SADC kisa lugha..teh teh teh

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…