Kwenye hili sidhani kama Lissu yuko sahihi.
Godbless Lema alikuwepo kwenye uzinduzi wa kampeni za Lissu Dar na alimpigia kampeni wakati ni mgombea Arusha.
Lakini, Kassim Majaliwa bado ni mtanzania, kwa mujibu wa katiba ya nchi ana haki ya kwenda mahali popote nchini.
Na kwa mujibu wa katiba ya nchi Kassim Majaliwa ana haki ya kufanya kazi ya kisiasa aliyotumwa na chama chake kwa sababu chama chake ni chama halali kilichosajiliwa nchini.
Kazi ya kuomba kura ni kazi ya wanachama wote, siyo wagombea peke yao!. It is not about individuals, it is about the party
Miaka michache iliyopita Chadema walikuwa wakilalamika kuzuiwa kufanya siasa nchi nzima, yaani mbunge wa Jimbo X kushiriki siasa za Jimbo Y, Leo Lissu anakubaliana na katazo lilelile la Magufuli ambalo walilipinga kipindi kile?
Labda Lissu anukuu vifungu vya sheria tujionee otherwise hoja yake hii naona haina mashiko