Uchaguzi 2020 Tarime: Tundu Lissu ampiga marufuku Kassim Majaliwa kufanya kampeni, Yadaiwa anavunja maadili ya uchaguzi

Uchaguzi 2020 Tarime: Tundu Lissu ampiga marufuku Kassim Majaliwa kufanya kampeni, Yadaiwa anavunja maadili ya uchaguzi

Tatizo lipo hivi, Je anaweza kuihakikishia Tume kwamba anapokwenda mikoani anaachana na uwaziri Mkuu na anakwenda kama kada na Mjumbe wa kamati kuu? Je hii inawezekana?

Kama akisema yeye bado ni Waziri Mkuu na nakwenda kutimiza majukumu yake hilo ni sawa, lakini je huko kuwa haongelei masuala ya kumwombea JPM kura?

Wanasheria (baadhi) wa Tanzania kama wewe huwa mko kama watoto wadogo, ningeshauri Serikali ifanye IQ testing kabla ya kuwaruhusu kuwa wanasheria, mnaiabisha nchi.

Low IQ!
 
Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amemuonya Kassim Majaliwa kwa kitendo chake cha kufanya kampeni za Urais kote anakopita , kwa vile kitendo hicho ni kukiuka maadili ya uchaguzi .

Kwa mujibu wa Lissu, Waziri Mkuu Kikatiba hatakiwi kumpiga kampeni mgombea Urais wa chama chake nje ya jimbo lake la uchaguzi ambalo ni Ruangwa tu na ameonya kwamba NEC isipochukua hatua kwenye hili basi itajisimika rasmi kuwa TUMECCM .

Je, Wanasheria mliopo hapa JF hili jambo limekaaje?

Mjumbe wa kamati kuu ya Ccm, kuna tatizo kufanya kampeni? Mgombea wetu aweke kifungu cha sheria kinachomzui? Siasa za majitaka hazitakiwi dunia ya sasa.
 
Wakati wote anakuwa na vyote.
1. Maadam serkali bado iko madarakani na haijakoma hadi itakapotangazo serkali nyingine.

2. Maadam ni mjumbe wa Nec ya ccm na anevaa kijani

Hii ni complicated hata Lishu anajua ila anatafuta mahali ambabaishe kwa desturi ya wanasheria
Ratiba ya Tume ni kwa Wagombea tu , huyu ratiba yake ya kampeni imepangwa na nani ? matokeo yake ni kama kilichotokea Ukerewe , Majaliwa akavamia na mwenye ratiba yake Lissu akazimiwa kivuko na wahudumu wa kivuko hicho wakaamriwa kujificha ili Lissu asivuke
 
Majaliwa ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM

Wajumbe wa kamati kuu ya CCM wamesambazwa nchi nzima kufanya kampeni
Ratiba za tume ni kwa wagombea urais nchi nzima na wabunge na madiwani kwenye majimbo na kata zao , huyu Majaliwa huko anakoenda ni kama nani ? wajumbe wa kamati kuu waendelee na vikao vya ndani vya mikakati tu na kuhudhuria majukwaa ya wagombea basi , Huyu Majaliwa akiendelea na kiherehere chake atakamatwa baada ya uchaguzi
 
Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amemuonya Kassim Majaliwa kwa kitendo chake cha kufanya kampeni za Urais kote anakopita , kwa vile kitendo hicho ni kukiuka maadili ya uchaguzi .

Kwa mujibu wa Lissu, Waziri Mkuu Kikatiba hatakiwi kumpiga kampeni mgombea Urais wa chama chake nje ya jimbo lake la uchaguzi ambalo ni Ruangwa tu na ameonya kwamba NEC isipochukua hatua kwenye hili basi itajisimika rasmi kuwa TUMECCM .

Je, Wanasheria mliopo hapa JF hili jambo limekaaje?

ccm wanavunja sana sheria
 
Ratiba za tume ni kwa wagombea urais nchi nzima na wabunge na madiwani kwenye majimbo na kata zao , huyu Majaliwa huko anakoenda ni kama nani ? wajumbe wa kamati kuu waendelee na vikao vya ndani vya mikakati tu na kuhudhuria majukwaa ya wagombea basi , Huyu Majaliwa akiendelea na kiherehere chake atakamatwa baada ya uchaguzi
Na Mbowe alikuwa akizunguka na Lisu kama nani wakati na yeye Mbowe ni mgombea ubunge Hai

Mbona alizunguka na Lisu majimbo kibao na kuhutumia kumfanyia kampeni Lisu kwa nini hakubaki jimboni kwake Hai?
 
Key word CONSTITUENCY = Jimbo la Uchaguzi. Hivyo ni sahihi na kweli Kassim Majaliwa ukomo wake ni jimboni. Hakuna jimbo linalojulikana kama Taifa.

Hivyo mgombea John Magufuli siyo mgombea wa jimbo lolote la uchaguzi ndani ya Tanzania na hawezi kumteua mtu kumuwakilisha kumfanyia kampeni ya urais.

Maana yake waziri Mkuu, mawaziri, wakuu wa mikoa , wilaya hawaruhusiwi kumfanyia kampeni ya Urais John Magufuli .

Wakuu wa mikoa na wilaya walioingia kuomba ubunge waliachia nyadhifa zao ili washiriki kugombea ubunge jimboni.

Waziri Mkuu yeye anaruhusiwa tu kufanya kampeni za kisiasa ktk jimbo lake tu la Ruangwa alikoombea ubunge na huko Ruangwa ndipo pekee anaweza kumnadi mgombea wa urais John Magufuli.
 
Ni wakati gani anakuwa PM na wakati gani anakuwa mjumbe wa kamati kuu ?
Pale anapokuwa katika ziara za kikazi haruhusiwi kufanya kampeni kwasababu atakuwa anasimama kama PM.
Kuna wakati mwaka 2015 Magufuli alikosea, aliomba kura wakati akiwa katika mkutano wa kuwaaga wakandarasi wa ujenzi kama waziri wa ujenzi. Lakini mwaka huu alirekebisha, tulitegemea angeomba kura wakati wa kutia saini makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta kule Chato lakini hakufanya hivyo.
 
Je, kwenye ratiba ya Tume ya Uchaguzi Waziri Mkuu yumo?mda na mahali? Kwanini Tume imekaa kimya? Huyu anatumia vyombo vya wananchi kunadi mgombea mahali popote! Kwanini Tume hawajawa fair katika hili?
Anatumia ratiba za ubunge za majimbo anayotembelea, in kama ilivyokuwa jana nilimwona Makongoro Nyerere akimfanyia kampeni Magufuli kupitia mikutano ya kampeni ya ubunge pale Chato.
 
Wakati wote anakuwa na vyote.
1. Maadam serkali bado iko madarakani na haijakoma hadi itakapotangazo serkali nyingine.

2. Maadam ni mjumbe wa Nec ya ccm na anevaa kijani

Hii ni complicated hata Lishu anajua ila anatafuta mahali ambabaishe kwa desturi ya wanasheria
Ni complicated kwako tu. Sheria ya taifa ya uchaguzi inamruhusu waziri kufanya kampeni maadamu asichanganye ziara za kikazi na mikutano ya kampeni.
 
Ni wakati gani anaongea na kutenda kama waziri mkuu?
Kila mkutano una makusudio na malengo yake, na hata vibali vya mikutano hiyo na ratiba za mikutano hiyo hutolewa kwa kuzingatia malengo na makusudio hayo ambayo huwa kwa maandishi, ikiwa lengo la mkutano ni kampeni basi atasimama kama waziri mkuu na kada wa chama, lakini haruhusiwi kufanya mkutano wenye malengo ya kazi za kiserikali na kuuchanganya na kampeni.
 
Namaanisha kama mkutano ni wa kiserikali ktk maandishi, itakuwa ni makosa kufanya kampeni ndani ya mkutano huo. Lakini mkutano ukiwa wa kampeni kimaandishi anaruhusiwa kuchanganya shughuli za kiserikali ndani yake kwani wakati wote nafasi yake ya kiserikali atakua nayo kwa mujibu wa sheria.
 
Huu ni mwiba mpya kwa mgombea wa chama kimoja cha siasa. Daktari amemshauri kusimama kwa dakika zisizozidi 20 akiwa anafanya kampeni. Sasa wale right men wake wakipigwa spana sijui atafanyaje kampeni.
Kichekesho anayetembea na spana ni nani na mara ngapi ameshaanguka jukwaani mwili mzima umejaa misumari
 
Huo hana uwezo wa kumpiga marufuku Majaliwa kufanya Kampeni, na kwa taarifa yako Majaliwa leo yuko Bukoba.

Lissu anauwezo wa kuwapiga Maruku akina mnyika na siyo waziri mkuu.
 
Back
Top Bottom