Mkuu michango yako humu JF ni ya kiwango cha juu mno! Kwanza heshima kwa hilo. Hoja ya msingi kwenye kesi hii (cited) Lissu Vs Majaliwa, 2020 ni kwamba maadili ya uchaguzi mkuu 2020 yanakataza viongozi wa serikali (mawaziri, RC's, DC's, n.k.) kuwafanyia kampeni wagombea.
Sasa kama Kassim Majaliwa, uwaziri mkuu wake ulishakoma then Lissu atakuwa amepotoka ila kama Kassim Majaliwa bado ni Waziri Mkuu wa JMT, Lissu ana hoja ya msingi kwa kuzingatia maadili yaliyotolewa na NEC yenyewe na ambayo kila mmoja anatakiwa kuyazingatia.