Taswira ya Yesu anayehubiriwa ni tofauti na Yesu halisi

Mkee Twende polepole na ningeomba uww na Religion Critic Torelace naona naona your patient rate inashuka samahani lakini mkuu tupo kwenye kuelimishna...
Hapana,huu ni muendelezo pia wa madai yako yanayoongozwa na hisia zaidi.
Halafu usichanganye kiswahili na kiingereza,chagua lugha moja itapendeza zaidi katika mjadala.
Ngoja Twende polepole...
Jina Miriam (Hebrew) au Mariam (Arabic version) au Mary (English version)

Ni jina lenye trace mpaka kwa nabii mke Miriam miaka 4000-3500 Iliyopita Limeitwa na wayahudi wengi sana..
So Mimi kusema kuna Yehoshua wengi sana waliozaliwa na Mama Aliyeitwa Miriam its mater of simple algorism tu...
Yehoshua (Hebrew) au yoshua (Kwa kiaramu) Halikuwa Jina Special sana miongoni mwa wayahudi na liliitwa saana Wakiwemo kina Yeshoshua Bin Nun, Yehoshua Bin sira na wengine wengi...
Ewaaaaaa,ndio maana nikakwambia mtaje Yehoshua mmoja aliyezaliwa na mariam bikira,na baba wa kufikia fundi selemala.akatenda miujiza katika umri mdogo kabisa.
Wewe wataje wote maelfu kama wapo.
Kuhusu watu wenye ufanano Wa maisha na Ujumbe Walioleta wa kwanza kabisa me ningekutajia Krishna na yesu kabla ya kwenda kwahao wengine ....
Krishna alileta ujumbe upi kutoka kwa Mungu,umeandikwa kwenye kitabu kipi ktk biblia??
Kitabu cha baghavad gita Kimekuwa kitabu cha mwaka 500Bc na kinaeleza exactly kama Ujumbe aliouleta Yesu wa aliyezaliwa 6 BC na kufafiki 27 AD..
Ujumbe kama wa Yesu yeyote aanweza kuuleta hata baada ya Yesu,je umetoka wapi??
Hata kwa sasa tuna manabii kibao.na wote wanaegemea katika ujumbe aina moja,nani katumwa kweli hapo ndipo mtihani.
Huu ni mfanano wa HORUS NA WENGINE NIKIWATJA KWENYE MYSTICISM ZINGINE ZA ZAMANI KULIKO YESU
View attachment 2798786
View attachment 2798787
View attachment 2798789
hili wala sio tatizo,ndio sababu nikakwambia hatandani ya bible yenyewe yapo matukio yaliyosimama kutabiri maisha na ukombozi wa Yesu.
 
Yesu ndio mwenye AD yake,ndio kipimo cha wakati.

Unapoamua kumfananisha na krishna lazima kwanza utambue hilo,swala la ufanano wa historia yao sio issue kabisa.
Hahahah unajua Hata AD ilikuwa inveted lini?
Yesu kazaliwa 6 BC na mwaka ulienda mpaka 1BC kwanini haukubadilika hiyo 6 BC na kuwa mwaka mwingine?

Ok Ngoja nikupe elimu kidogo...

Neno AD ni kifupi cha neno Anno Domino
Japo kirefu chake Jumla kilikuwa ni Anno Domini Nostri Jesu Christi.... Ambalo lina maana ya mwaka wa bwana wetu yesu kristu

SAsa mkuu system hii ilianzishwa mwaka 525 na Dionysius Exiguus lakini haikuwahu kutumika kwa ukubwa huo mpaka karne ya 9...yaani Mwkaa 1000s

Kwahiyo AD na BC.....Hazina muda mrefu wa Kutumika zaidi ya AH ya waislamu

hilo linatumiwa Baadhi ya Mabara na Kwa nchi zenye mcqhanganyiko na wakristo au wanaotumia Gregory calendar ila kwa Wengine wanatumia
BCE na CE..(Before Common Era na In Common era)

na hiyo ni njia ya kudetermine date tu wala isikuoe shida basi ntatumia BCE na CE

kwakuwa nishakupa historia hiyo sasa naenda kwa hao wengine

sio kwamba krishna kafnana na Yesu....ila Yesu ndo kafanana na Krishna ...
krishna ni wazamani sana 500BCE kuliko yesu So kuna uwezekani story za yesu wamekopy kwa krishna na wakazichuja...
 
Kuna wakati majIbu ya Yesu usipokuwa makini unaweza kuhisi jamaa alikuwa michosho sana, lakini alikuwa sahihi Mafarisayo walikuwa na maswali ya kiwaki sana ya kinafiki, kumjaribu na kejeli

Yesu ni mtu mmoja alikuwa mwana sana ila alikuwa straightforward
Huu uzi masela wachungaji wakae pembeni
 
Ukitaka kujua wayahudi hawakuwahi kumkubali Yesu kutokana na historia ya maisha soma the Talmud unmasked ambayo ndio mafundisho ya wayahudi
Katika kitabu cha The Talmud unmasked by Rev I.B. Ptanaitis chapter I.P 30
"Hayo ndio waliyotenda kwa mwana wa stada katika Lud na wakamsulubisha jioni ya pasaka .Kwani mwana huyo wa Stada alikuwa mwanaye Pandira. Maana Mwalimu Chasda anatuambia ya kuwa Pandira alikuwa mume wa Stada aliyekuwa mamake na yeye aliishi katika zama za Paphus mwana wa Jehuda "

Mwandishi wa The Talmud Unmasked Rev IB Pranaitis akifafanua maneno hapo juu anasema
"Hayo yanamaanisha ya kwamba Mariam ndie aliyeitwa Stada yaaan malaya kwani sawa na iliyovyofundishwa hapo Pumbadita yeye akamuacha mumewe na akafanya uzinzi.Hayo pia yameandikwa Katika Jerusalem Talmud na Maimonides
Hivyo ndivyo Talmud inavyosema juu ya Yesu wanazareti na hata ukiangalia Yesu alipata laaana ya torati maana yake amelaaniwa na Mungu
Rejea
"Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu ambalo sikumuagiza kulinena au atakayenena kwa jina la mtu mwingine nabii yule atakufa " kumbukumbu la torati 18:20

Kwa hivyo Yesu alikuja kunena neno la Mungu mwingine na kujifananisha na Mungu mwenyewe wakati yeye nabii na alikufa
Na mtu akitenda dhambi ipasayo kifa na ukifa kwa kuuwa nawe ukamtundika ktk mti hata mzoga wako usikae siku hiyo na wakakuzika basi ujue ww umelaaniwa na Mungu
"Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa akauawa nawe ukamtundika juu ya mti mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti lazima utamzika siku hiyo kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu " kumbukumbu la torati 21:22-23
 
Hapana,huu ni muendelezo pia wa madai yako yanayoongozwa na hisia zaidi.
Halafu usichanganye kiswahili na kiingereza,chagua lugha moja itapendeza zaidi katika mjadala.

Sorry Mkuu kwa kuchanganya kwangu lugha najitahidi sana kutokufanya hivyo ila nashindwa labda kwa sababu ni muda mrefu sipo nchini huenda kupata watu wanaoongea kiswahili ni wachache..
Ila najitahidi sana Asante...
Krishna alileta ujumbe upi kutoka kwa Mungu,umeandikwa kwenye kitabu kipi ktk biblia??
Krisha hawezi kuwa kwenye biblia Krishna yuko kwenye mysticism zingine kabisa ambazo zina umri mrefu zaidi ya biblia Huenda zaidi ya umri wa Dunia iliyoandikwa kwenye biblia (Umri wa Dunia kwenye Biblia ni Miaka 6004 mpaka sasa)
Ila kwenye mysticism ya Hinduism na budhism zina umri mrefu sana zaidi ya miaka 100k

Krishna alikuwa akimuelezea Arjun vitu vingi pamoja na wengine, Yote yameandikwa Katika bhagavad Gita na sio Biblia mwaka 500 BCE
Au kama upenavyo 500 kabla ya Kristo..
Sio kila kitu kimeandikwa kwenye biblia...
Na ndo maana kuna Book of mormones pia
Ujumbe kama wa Yesu yeyote aanweza kuuleta hata baada ya Yesu,je umetoka wapi??
Huo ulikuja kabla ya kristo so we huoni kuna mashaka. Hapo..Tena far before
 
Hahahah unajua Hata AD ilikuwa inveted lini?
sidhani kama ina uhusiano wowote na hesabu ya miaka AD BC.
Yesu kazaliwa 6 BC na mwaka ulienda mpaka 1BC kwanini haukubadilika hiyo 6 BC na kuwa mwaka mwingine?
Yesu kazaliwa 6 BC😄😄
Unaelewa hata ulichokiandika??
Ok Ngoja nikupe elimu kidogo...

Neno AD ni kifupi cha neno Anno Domino
Japo kirefu chake Jumla kilikuwa ni Anno Domini Nostri Jesu Christi.... Ambalo lina maana ya mwaka wa bwana wetu yesu kristu
Hii nilisoma form 1 history.
SAsa mkuu system hii ilianzishwa mwaka 525 na Dionysius Exiguus lakini haikuwahu kutumika kwa ukubwa huo mpaka karne ya 9...yaani Mwkaa 1000s
Cha msingi unatakiwa kujua kwamba kipimo cha hesabu ya miaka mpaka ni ujio wa Yesu.
Kwahiyo AD na BC.....Hazina muda mrefu wa Kutumika zaidi ya AH ya waislamu
Wala usiogope hata science na mahesabu husika vimeanza kuwa serious juzi tu.
hilo linatumiwa Baadhi ya Mabara na Kwa nchi zenye mcqhanganyiko na wakristo au wanaotumia Gregory calendar ila kwa Wengine wanatumia
BCE na CE..(Before Common Era na In Common era)
Tuzungumzie BC na AD
na hiyo ni njia ya kudetermine date tu wala isikuoe shida basi ntatumia BCE na CE
Hamna shida,mimi nitatumia standard rate BC au AD
kwakuwa nishakupa historia hiyo sasa naenda kwa hao wengine
Niende kwa krishna aliyeishi mwaka gani kutoka sasa??namba na rejea tafadhali.
sio kwamba krishna kafnana na Yesu....ila Yesu ndo kafanana na Krishna ...
Wala sio tatizo ni kipaumbele chako tu.
krishna ni wazamani sana 500BCE kuliko yesu So kuna uwezekani story za yesu wamekopy kwa krishna na wakazichuja...
Kuna uwezekano,haya ni madai.
 
Sorry Mkuu kwa kuchanganya kwangu lugha najitahidi sana kutokufanya hivyo ila nashindwa labda kwa sababu ni muda mrefu sipo nchini huenda kupata watu wanaoongea kiswahili ni wachache..
Ila najitahidi sana Asante...

Krisha hawezi kuwa kwenye biblia Krishna yuko kwenye mysticism zingine kabisa ambazo zina umri mrefu zaidi ya biblia Huenda zaidi ya umri wa Dunia iliyoandikwa kwenye biblia (Umri wa Dunia kwenye Biblia ni Miaka 6004 mpaka sasa)
Ila kwenye mysticism ya Hinduism na budhism zina umri mrefu sana zaidi ya miaka 100k
Vipi hizi zote mwandishi ni nani??
Mpaka umeifanya kuwa rejea ya hakika kwako tofauti na zile zilizoandikwa na mashuhuda juu ya Yesu miaka kadhaa baada ya kuondoka kwake??
Krishna alikuwa akimuelezea Arjun vitu vingi pamoja na wengine, Yote yameandikwa Katika bhagavad Gita na sio Biblia mwaka 500 BCE
Au kama upenavyo 500 kabla ya Kristo..
Sio kila kitu kimeandikwa kwenye biblia...
Na ndo maana kuna Book of mormones pia
Kabisa bible haikuandika kila kitu hata cha Yesu mwenyewe achia mbali watu wengine.

Huo ulikuja kabla ya kristo so we huoni kuna mashaka. Hapo..Tena far before
Mashaka niyatoe wapi mkuu??
 
Ukisoma na kutafakari kwa umakini kuhusu Yesu unagundua kwamba alikuwa ni wale watu ambao jamii inawachukulia kwamba wamepinda yani outcast.

Hata wale wanafunzi wake aliokuwa akiongozana nao jamii inaonekaan ilikuwa inawachukulia kama watu wasiokuwa na maadili waliopotoka yani waliopinda.

Ndio maana kuna sehemu hadi anaulizwa, inakuaje anakula na kunywa na wenye dhambi? Hii bila shaka haina tofauti na sasa unamuuliza, we jamaa unaonekana ni mwenye ehshima inakuaje unashinda na wazinzi na walevi?

Hebu fikiria mtu unayemheshimu sana anakuja kahaba analia miguuni mwake anampangusa kwa nywele anambusu miguu, assume huyo jamaa anayefanyiwa hivyo ni hakimu na huyo kahaba ana kesi. Halafu baada ya kufanyiwa hivyo hakimu anamwambia kesi yako utashinda!

Bila shaka utasema hakimu kasema hayo kwa sababu kahaba kamtamanisha kwa kumshika shika na kumbusu miguu huenda watamalizana huko mebeleni. Hiki ndicho kilichotokea kwa yule kahaba na bila shaka wale jamaa walisema moyoni huyu jamaa amelegea kwa kahaba atakuwa msela tu anatuigizia.

Ukichukulia hali hii kwakweli hata angekuja leo hapa TZ bado watu wangemkataa. Wangemwona msela Fulani hivi mwenye group la watu waliopinda. Yani kipindi anajiita kwamba yeye ni mfalme wa Wayahudi, huenda wale viongozi walikuwa wanamchukulia kama Ney wa Mitego anavyojiita raisi wa masela au Madee anayejiita rais wa Manzese hawakuwa wakimchukulia serious kihivyo mpaka alipoanza wazingua.

Kama akirudi kwa style hiyo hiyo sijui ni wangapi wataamini kuwa ni Yesu.
Yesu na Mohammed wote ni wale wale tu
 
sidhani kama ina uhusiano wowote na hesabu ya miaka AD BC.

Yesu kazaliwa 6 BC😄😄
Unaelewa hata ulichokiandika??
Naelewa ndo maana nimeandika so Ulitaka niandike BCE..
unajua hata kwanini Milenium zilikuwa zinabadili Date code..
Unajua mwaka 2000 uliitwaje kama tungekuwa tunafata bado codding era?
(Ungeitwa Y2K) Au hilo nalo hufahamu ?
Coding era ilikuwa system ya Tangu zaman na ndo maana hta kwenye Biblia yako utasikia wanasema zama za Mfalme dario ( ina maana Dario Era)

Kwahyo mimi sishangai Rumi Kutumia Neno BC na AD kwa sababu Ilikuwa ni Era ambayo kila mtu anazungumza kuhusu Yesu..

Tuzungumzie BC na AD

Hamna shida,mimi nitatumia standard rate BC au AD

Hakuna standard rate of Dating inategemea na uko wapi ikiwa bara la ASIA hawatumii BC au AD

Kuna uwezekano,haya ni madai.
Kama kweli unajua huwezi kusema madai kwa dini ambayo ina zaidi ya MIAKA 100K Kulinganisha na dini ambayo haina hta miaka 3000..
 
Vipi hizi zote mwandishi ni nani??
Mpaka umeifanya kuwa rejea ya hakika kwako tofauti na zile zilizoandikwa na mashuhuda juu ya Yesu miaka kadhaa baada ya kuondoka kwake??
India walikuwa na maendeleo ya Technolojia Tangu zamani hivyo vitabu vingi wanavyo vinaimri mrefu sana na hicho kitabu kimeandikwa na wahusika kwa kupass sequences Kizazi mpaka kizazi mwandishi akiwa ni Arjun

Kajaribu kusoma bhagavad gita Na historia yake...
Natumia vitabu vyote iwe vya greek mysticism na hata vya Christian mysticism na hata viwe ni Islam mysticism nilichukua muda mrefu kusoma phylosophy kwa undani
Hakuna rejea ya Hakika hata moja hata phylosophy yenyewe not even science (maana hata science huchage kwa kila wakati)

Nakupa ushauri mmoja Bado unahitaji kusoma sana kuna vitu vingi vinapungua kwako
 
Naelewa ndo maana nimeandika so Ulitaka niandike BCE..
unajua hata kwanini Milenium zilikuwa zinabadili Date code..
Unajua mwaka 2000 uliitwaje kama tungekuwa tunafata bado codding era?
(Ungeitwa Y2K) Au hilo nalo hufahamu ?
Coding era ilikuwa system ya Tangu zaman na ndo maana hta kwenye Biblia yako utasikia wanasema zama za Mfalme dario ( ina maana Dario Era)
Sasa hii ina uhusiano gani na kipimo cha miaka kuanza kuhesabiwa alipozaliwa Yesu!!!
Kwahyo mimi sishangai Rumi Kutumia Neno BC na AD kwa sababu Ilikuwa ni Era ambayo kila mtu anazungumza kuhusu Yesu..

Hakuna standard rate of Dating inategemea na uko wapi ikiwa bara la ASIA hawatumii BC au AD
Usiseme bara la ASIA,taja nchi baadhi.
Kama kweli unajua huwezi kusema madai kwa dini ambayo ina zaidi ya MIAKA 100K Kulinganisha na dini ambayo haina hta miaka 3000..
Sasa wewe unapata wasi wasi na dini yenye miaka chini ya elfu 3!!!nguvu ya kuamini story za miaka zaidi ya elfu 5 unazipata wapi!!!!😀😀😀
 
Sasa hii ina uhusiano gani na kipimo cha miaka kuanza kuhesabiwa alipozaliwa Yesu!!!
Nimeshajibu kuwa Yesu alikuwa Story ya Town kwenye miaka kuanzia 300 mpaka miaka 900 so walitrace alizaliwa lini wakapaga then ile Era roman wakaipa jina lake
Usiseme bara la ASIA,taja nchi baadhi.
Nitajie nchi ya Asia wanayotumia AD na BCE
Sasa wewe unapata wasi wasi na dini yenye miaka chini ya elfu 3!!!nguvu ya kuamini story za miaka zaidi ya elfu 5 unazipata wapi!!!!😀😀😀
Kama ingekuwa hivyo kwanini sijakuona ukiamni kuhusu story za Muendelezo wa Dini yako ya kikristo ya Mormones..
Au kwanini huamini uislmu ambao una miaka chini ya 1500
 
India walikuwa na maendeleo ya Technolojia Tangu zamani hivyo vitabu vingi wanavyo vinaimri mrefu sana na hicho kitabu kimeandikwa na wahusika kwa kupass sequences Kizazi mpaka kizazi mwandishi akiwa ni Arjun
Lakini wewe umekataa taarifa za bible kwamba hakuandika Yesu wala aliyeonana na Yesu😃😃

Kuhusu maendeleo sina shaka,hata hao mafarao hapo misri wamepiga hatua muda mrefu sana.
Kajaribu kusoma bhagavad gita Na historia yake...
Tofauti yangu na wewe ni moja,nikisoma nitasoma nielewe ili nikifate sio kutangaza kwama nimekisoma.
Natumia vitabu vyote iwe vya greek mysticism na hata vya Christian mysticism na hata viwe ni Islam mysticism nilichukua muda mrefu kusoma phylosophy kwa undani
Sijui ni undani upi???
Hakuna rejea ya Hakika hata moja hata phylosophy yenyewe not even science (maana hata science huchage kwa kila wakati)
Kwahiyo umenaki hewani kama bendera!!!!nini lengo lako kusoma hivyo vitabu!?
Nakupa ushauri mmoja Bado unahitaji kusoma sana kuna vitu vingi vinapungua kwako
Kusoma sana ni hatari,kama kichwa chako sio imara,ndio unaona wewe hapa hujui ushike jambo gani baada ya kusoma sana.

Soma kitu kwa malengo
 
Lakini wewe umekataa taarifa za bible kwamba hakuandika Yesu wala aliyeonana na Yesu😃😃

Kuhusu maendeleo sina shaka,hata hao mafarao hapo misri wamepiga hatua muda mrefu sana.

Tofauti yangu na wewe ni moja,nikisoma nitasoma nielewe ili nikifate sio kutangaza kwama nimekisoma.

Sijui ni undani upi???

Kwahiyo umenaki hewani kama bendera!!!!nini lengo lako kusoma hivyo vitabu!?

Kusoma sana ni hatari,kama kichwa chako sio imara,ndio unaona wewe hapa hujui ushike jambo gani baada ya kusoma sana.

Soma kitu kwa malengo
Baada ya kusoma nimekuwa huru sana nimegundua vingi sana hata hivyo Phylosophy na Dini yaani Theology niliisoma miaka mingi sna ilopita kama 20 hivi sema nilikataa kuwa mtumwa baada ya kuwa mchungaji kwa mda mchache...
Na baadaye nilisoma elimu zingine na nimekuwa huru kutokana na akili yangu kupanuka na Kuwa huru nje ya box (Raha sana )
 
Nimeshajibu kuwa Yesu alikuwa Story ya Town kwenye miaka kuanzia 300 mpaka miaka 900 so walitrace alizaliwa lini wakapaga then ile Era roman wakaipa jina lake
Ndio maana nikasema Yesu ndio mwenye BC na AD yake au ilifanywa rejea ya mtemi isike???
Nitajie nchi ya Asia wanayotumia AD na BCE
Nchi zote ASIA wanatumia huu mfumo,leo dunia nzima inahesabu 2023 au hutaki???
Kama ingekuwa hivyo kwanini sijakuona ukiamni kuhusu story za Muendelezo wa Dini yako ya kikristo ya Mormones..
Au kwanini huamini uislmu ambao una miaka chini ya 1500
Ukristo una madhehehu mengi tu,uislam si ktk madhehebu hayo,wapo wanaoamini huo mwendelezo hao mormones.
 
Baada ya kusoma nimekuwa huru sana nimegundua vingi sana hata hivyo Phylosophy na Dini yaani Theology niliisoma miaka mingi sna ilopita kama 20 hivi sema nilikataa kuwa mtumwa baada ya kuwa mchungaji kwa mda mchache...
Na baadaye nilisoma elimu zingine na nimekuwa huru kutokana na akili yangu kupanuka na Kuwa huru nje ya box (Raha sana )
Sasa mtafute Roho Mtakatifu zaidi...

Omba Toba na Rehema, kwako na familia baba na mama...

Jitakase kwa damu yake...

Muombee Roho Mtakatifu aje akujulishe juu ya Yesu na atakuja kwako...
 
Baada ya kusoma nimekuwa huru sana nimegundua vingi sana hata hivyo Phylosophy na Dini yaani Theology niliisoma miaka mingi sna ilopita kama 20 hivi sema nilikataa kuwa mtumwa baada ya kuwa mchungaji kwa mda mchache...
Na baadaye nilisoma elimu zingine na nimekuwa huru kutokana na akili yangu kupanuka na Kuwa huru nje ya box (Raha sana )
Una uhakika uko huru na akili yako imepanuka???
 
Back
Top Bottom