Tathmini fupi baada ya tamko la Mzee Kinana kuhusu kero ya Polisi wa Usalama Barabarani

Tathmini fupi baada ya tamko la Mzee Kinana kuhusu kero ya Polisi wa Usalama Barabarani

MICHAEL JACKSONN

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
226
Reaction score
229
Ni kama wiki sasa imepita mara baada ya naibu mwenyekiti ccm taifa, Dkt. Abdulahman Kinana, zimeshatokea ajali mbili za magari na kuondoka na roho za watu kadhaa, sababu ni mwendokasi.
IMG_4051.jpg

IMG_4052.jpg



Tukiangalia kisiasa na kimihemko,traffic police hawana cha maana wanachofanya barabarani zaidi ya kujinufaisha na kuineemesha serikali inayowalipa.

Lakini kwa jicho la tatu, wana kazi kubwa sana ni kama ile kazi ya dini zetu katika kuchangua amani na utulivu katika kizazi hiki chenye kila aina ya uthubutu.Bila hizi dini hali ingekuwa mbaya zaidi.

Ukiangalia malalamiko ya wahanga wengi wa traffic polisi ni,rushwa na kupotezewa muda wawapo safarini au barabarani kwa ujumla.

Hii ni kama kusema huwaona traffic kama nzi katika chakula. Maana yake kama isingekuwa traffic police bas humo barabarani ingekuwa ni sehemu rasmi ya kuokolea muda lakini pia kupima uwezo wa vifaa vyetu,hoja yangu iko hapo juu.

Fikiria mtu timamu,msomi,umri mkubwa kabisa analalamika kuhusu kuviziwa na traffic kichakani,maana yake huwa anafanya uhuni asipowaona[emoji28][emoji28].

Yaani anasimama na sheria anapojua kuna traffic atamkamata. Sasa wamepunguzwa kwa tamko la jamaa wa ccm,ni mwendo wa kujidai barabarani. Kwa sababu walikuwa wananenepa kwa elfu 2 zetu,bora tu waondoke.

Lakini wanatuachia msimamizi ambaye hachukui rushwa bali roho yako,ukivunja sheria.

Neno langu sio sheria maana ajali hazijaanza wiki iliyopita,bali neno langu ni mood anayokuwa nayo dereva baada ya kujua road hakuna traffic,kila mtu na awe msimamizi wa mwingine.
 
Tuache kukimbia kimbia. Magari yetu ni chakavu na barabara si salama. Gari zimetengenezwa 2000 unakimbiza speed 140 kwenye barabara zisizoaminika.
 
Acha uongo afande ajali zilikuwepo kila siku
 
Nilidhani angeshauri ni namna gani jeshi letu litengeneze HIMARS zetu wenyewe au silaha kali za kisasa. Cha ajabu akaibukia huko🤠🤠🤠🤠
 
Nasikia turaffiki saivi wanakupetea mkono ili ukimbie sana! 🤣🤣🤣 walitii haraka, ngj tuishe.
 
Leo nimesikia tena newforce ya mbeya imepoteza mmoja na majeruhi 6. Niliwahi kusema kuwa, pamoja na mapungufu ya police, ila wakigoma hata kwa nusu saa tutacheki picha , saivi wamepunguzwa tu ndo ajari kila cku. Siasa za kufurahisha watu zisipoachwa basi yajayo yanasikitisha.
 
Mzee Kinana ni sawa lkn inatugharimu uhai wetu.Kutotii Sheria ni kirusi hatari maisha na Mali zetu.Kama trafiki wakiondolewa basi njia mbadala za kielectroniki zibuniwe ama sivyo hii ni gharika.
 
Leo nimesikia tena newforce ya mbeya imepoteza mmoja na majeruhi 6. Niliwahi kusema kuwa, pamoja na mapungufu ya police, ila wakigoma hata kwa nusu saa tutacheki picha , saivi wamepunguzwa tu ndo ajari kila cku. Siasa za kufurahisha watu zisipoachwa basi yajayo yanasikitisha.
Alisema wapunguzwe, binadamu bwana yaan manynyaso kaishayaona ni sehemu ya maisha yake au hamjui uwepo wao wengi barabarani wanadumaza uchumi? Hao hawana tofauti na kuwa na kuwa na majaji au hakimu wachache.
 
Trafiki polisi mmejiandikia uzi kutaka mhakalishiwe zile za kubrashia viatu?
 
Uzi wa traffic huu baada ya kuona mapato ya kubrashia viatu yamekata. Hata mkae kila baada ya mita 100 still ajali zitatokea tu.

Cha muhimu kila dereva awe na nidhamu binafsi. Ila traffic officers kurundikana barabarani ovyo ni uhuni na njaa kali. Hatuwataki mliendekeza njaa sana.
 
Tuache kukimbia kimbia. Magari yetu ni chakavu na barabara si salama. Gari zimetengenezwa 2000 unakimbiza speed 140 kwenye barabara zisizoaminika.
Waambie ukweli hawa mapimbi! Magari mabovu tbs wanakula rushwa magari yanaingia hata ya miaka ya 90!
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Waambie ukweli hawa mapimbi! Magari mabovu tbs wanakula rushwa magari yanaingia hata ya miaka ya 90!
Acha tu mkuu. Magari yetu ni chini ya viwango halafu barabara nyembamba.
 
kwamba kabla ya kinanakutoa ule ushauri mwezi julay wote hakukuwa na ajali? itakuwa wewe ni trafiki tu unajitetea
 
Tatizo watu wamemnukuu kinana vibaya. Alisema wapunguzwe. Wapewe elimu. Na watumie vifaa vya kisasa ili kuondoa usumbufu wa upotevu kwa wenye magari.
 
KINANA ALIPASWA KUPUUZWA.


Sisi Watumiaji wa Barabara zetu ndio Wachawi wenyewe , ni wachaw ambao tunahisi madhaifu yetu, madhaifu ya vyombo vyetu sio inshuuu Bali Inshu ni Trafiki barabarani.


Ukweli nikwamba, Kitendo Cha Madereva kujua kua Mahali Fulani, Mahali Fulani ,Mahali Fulani Kuna Trafiki, wanajiongeza na hukuti akienda Kwa speed kubwa .


Hata Wapumbavu huzeeka nao huitwa "Mzee".
 
Uzi wa traffic huu baada ya kuona mapato ya kubrashia viatu yamekata. Hata mkae kila baada ya mita 100 still ajali zitatokea tu.
hizi ni kauli za mtu aliyekata tamaa kuchukua wajibu wake.
Cha muhimu kila dereva awe na nidhamu binafs
nidhamu binafsi ni kutolalamika unapoona traffic ni wengi,bali kujisimamia mpaka wakose kosa dhidi yako.
. Ila traffic officers kurundikana barabarani ovyo ni uhuni na njaa kali.
njaa za traffic zimekaa kwenye mtizamo wako,kama akichukua buku yako usiyejijali na za wengine 100 kwa siku kwa mwezi ni 2.7 milion wastan.
yeye anapiga hela wewe ukiwa busy kuuza roho.
Hatuwataki mliendekeza njaa sana.
hawawezi kutoka sababu wewe huwapendi.
 
Back
Top Bottom