Uchaguzi 2020 Tathmini yangu juu ya Uchaguzi Mkuu 2020: Hakuna sababu nzuri ya kukataa kuteua wabunge wa Viti Maalum CHADEMA

Hoja ya mleta mada imefia hapa. Ngoja niendelee kupata [emoji485] wine yangu.
 
Wewe sii miongoni mwa mnaosema wanachelewesha maendeleo, sasa mnahangaika nao wanini, je nyie hamyataki maendeleo, au ndio mnazuia maendeleo kwa kuweka vigingi?
 

Mtazamo wako hizo kura zinazodaiwa walipata CDM na ACT ni zile ambazo walizopigiwa. Unasahau kuwa mojawapo ya madai ya CDM ni kuwa kura ama hazikuhesabiwa kabisa au zilipuuzwa na zikajazwa namba ambazo wasimamizi wenye ndio wanajua walizitoa wapi. Kwa sbabu hii basi hata hizo kura zinazosemekana ni za vyama vya upinzani ni haramu kwa sababu hakuna uhakika kuwa zilitokana na zile zilizopigwa kwenye vituo. Ndio maana wanakataa kutambua zoezi zima na kukataa hesabu zote zilizotokana na huu uchaguzi ( ikiwa pamoja na zile wanazoambiwa walipata). Ukitaka kutenda haki ungewashupalia NEC wapitie upya hesabu zao na kura zilizopigwa mbele ya mawakala wa pande zote husika pamoja na namna wagombea walivyopatikana. Pale ambapo itaonekana dhahiri kuwa kuna kamchezo, uchaguzi ufutwe na urudiwe upya. Hiyo itasaidia kupunguza presha.

Amandla...
 
Sijui kiingeleza vizuri, Ila swala la mabadiriko huwa halizuiriki labda kuchelewesha tu.... Mabadiriko huwa yanakuja kwa either kuratibiwa/organized and coordinated au mapunduzi/uprise revolutions.. Mara zote aina ya pili huwa na madhara ya kudi stabilize nchi/taifa mfano ya hivi karibuni Misri,Libya.. pia Kuna ileya Kati ya hizo mbili SEMI organized and coordinated revolutions eg Tunisia, Jordan, Zimbabwe

It's certain oppression and injustice entually turn into a revolution. Kwa hiyo kazi kwetu kuchagua tunataka aina ipi hapa Tz,

Note; siwapendi ccm kwa kui masikinisha hii nchi, lakini kwa katiba tuliyonayo God forbid ikatokea ccm ikapoteza uchaguzi kwa ngazi Rais(na lazima itakuja tolewa/poteza Tena siyo miaka mingi ijayo) taifa lipaitia kipindi kigumu/distabilize kwa muda (mfupi,Kati, au mrefu)... Because ccm hii Ni mfumo (mahakimu Kama wote, majenerali wajeshi na usalama, wakuu wa juu/Kati wa Kila Kona ya serikali Ni ccm,dc,rc,ded.... Sasa u can image kuwabadirisha hawa wote kwa muda mfupi chame a kingine kikichuwa madaraka Tena kwa katiba hii ilivyotoa nguvu na madaraka makubwa kwa rais
 

Ndugu, ukiwa na bahati ya kuhudhuria mahakamani utasikia mawakili wanasema:

Your honor, this is vexatious, yaani, Mhe, huu ni utukutu mahakamani.
Your honor, this frivolous, yaani, Mhe, huu ni utundu mahakamani.

Maana yake ni kwamba, kuna mtu anajifanya kujenga hoja, hana ushahidi, lakini anaing'ang'ania kiasi cha kuifanya mahakama ishindwe kutekeleza majukumu yake.

Ushauri wangu kwako: waulize hao wanaoyasema hayo maneno maswali haya:

  • Kama kura hazikuhesabiwa kabisa, zile zilizotangazwa zilitoka wapi? Kama wanajua zilikotoka wanaweza kuweka ushahidi mbele ya mahakama na kuthibitisha kauli hizo?
  • Katika vile vituo ambako Chadema wanakiri kwamba waliweka mawakala, nako kura hazikuhesabiwa? Kama zilihesabiwa mawakala wanazo takwimu tofauti?
Haya ni baadhi ya maswali, napenda yakusaidie kufikiri kama mtu mzima.

Ukiacha mlango wazi, mwizi akaiba, halafu ukaenda polisi kusema mwizi kavunja mlango, polisi wakija na kukuta mlango uko salama, wanakwambia wewe umeshirikiana na mwizi kujiibia! Hakuna mazingira kama haya kwenye maeneo mengi nchini?

Tuzidi kutafakari pamoja.
 
Safi saana kwa majibu mazuri swali la mwisho. Umesema "alafu chama kiendelee kushughulikia masuala hayo mengine kuhusu kura zinazodaiwa kuibwa na watu wasiojulikana!" Kushughulikia wapi? kivipi? nani atakuwa tayari kuwasikiliza? (unapeleka kesi ya Chui kumla mnyama swala kwa mzee wa nyika Simba!?). Nadhani ni bora kuendelea kushughulikia hili tatizo kwa style hii watumiayo sasa kwani hii ndiyo pia imekusukuma wewe na wengine wengi duniani kulipigia kelele swala hili, vinginevyo wangefuata ushauri wako hii habari ingekuwa ni historia na watu (walioko madarakani) wangeendelea kujipanga na style nyingine mpya ya kufanya maangamizi makubwa zaidi katika uchaguzi ujao wa 2025. Acha Chadema waendelee na wanachokifanya kwa sasa kwani wanaoumia zaidi ni hao walioko madarakani kuliko wao Chadema. Kwani hata kwenye ndoa hakuna kitu kinauma kama kumfanyia ubaya mkeo, akaondoka nyumbani kwako arafu ukawa unambembeleza arudi home bila mafanikio huku yeye anapiga mark time aisee usithubutu mwanaume utakonda mpaka utaisha.... lakini akirudi kirahisi kirahisi hata wewe usahau yoote yaliyotokea kirahis rahisi na anayeishia kujuta ni mwanamke na ikitokea tatizo ilo ilo mara ya pili mwanamke akajaribu njia hiyo ya hapo mwanzo huishia kupoteza sijui kwanini? nadhani hii inatokana na ile theory ya "marginal utility of wants"
 
Yafaa tuwaulize walioyaratibu,tukiwauliza wengine tunawaonea.
 
Hilo si ndo litakua bora zaidi kwa CCM, kwa sababu wapinzani wanachelewesha maendeleo.
 

NImekuelewa. Kitabu hicho nilichokinukuu nitakitafsiri kwa kiswahili na kukiweka hapa katika siku za karibuni ili kila mtu asome na kuelimika.
 
Kama mnaona CDM wanachelewa jipitisheni nyie muongeze idadi si mlisema 28 walipita bila kupingwa na hakuna mgombea wa CCM alienguliwa na tume kwenye mchakato!
 
Nikupongeze kwa kuweza kuweka hicho kitabu hapa. Wale tusiotaka kuijua siasa wala kuifuatilia tuwapongeze kwa moyo mliokuwa nao
 
Mimi napenda mnavyopenda kuwatukana watu ili mjione kuwa ni werevu zaidi. Maneno vexatious na frivolous ni maneno ya kawaida tu ingawa labda wanasheria wetu wanapenda kuyatumia ili watu kama nyie muone kuwa kweli wamesoma.
Madai ya wapinzani ni kuwa sehemu nyingine wasimamizi walijiandikia matokeo waliyoyataka wenyewe. Mfano ni vituo ambako kura za wagombea zilifanana kiasi cha kutia shaka. Malalamiko mengine ni kuwa hata hizo sehemu chache ambako wakala wao walikuwepo, hawakupewa nakala ya matokeo kama ilivyokuwa kawaida. Ndio maana kama kweli figisu hazijafanyika, NEC wangeweka wazi hesabu zao na kuwakaribisha watu wakague na wawasimamie watakavyohesabu upya kura zinazotiliwa shaka. Wanaogopa nini kufanya hivyo?
Mimi sio mwanasheria lakini najua huwezi kujitetea kuwa niliingia kwenye chumba kisichokuwa changu na kuchukua luninga kwa sababu mlango ulikuwa wazi. Na ninavyojua, breaking and entering haina lazima uvunje mlango. Hata ukiusukuma mlango ambao ulikuwa haujafungwa inahesabiwa kuwa ume break na kuingia. Aidha, kutokuwa na dalili yeyote ya kuvunjwa mlango hamna maana kuwa mwenye chumba alishirikiana na mwizi maana mwizi anaweza kuwa amechongesha ufunguo wake. Polisi wakimsumbua aliyeshitaki watakuwa hawajatenda haki.

Amandla...
 
Kama mnaona CDM wanachelewa jipitisheni nyie muongeze idadi si mlisema 28 walipita bila kupingwa na hakuna mgombea wa CCM alienguliwa na tume kwenye mchakato!
Tabia ya kushindwa kutofautisha hoja na mleta hoja ni dalili kwamba Watanzania wenye elimu iliyo chini ya kidato cha nne wanafikia 90%, na wewe ni miongoni mwao.

Sio lazima uandike chochote. Ukimya nao unakubalika.
 
Katika mawakala 80000+ ambao CHADEMA waliweka.

Mpaka kufikia muda wa kuhesabu kura walikuwa wamebaki 10000 tu vituoni huku wengine walitolewa na wengine kukamatwa.

Hao 10000 wenyewe waliobaki vituoni hawakupewa nakala za matokeo hivyo hata matokeo ya uchaguzi CHADEMA hawana.

Sasa tuseme kuwa hao 10000 waliweza kusimamia kura za chama chao je kura walizopata CHADEMA zinaweza kuwa zimetoka kwenye vituo hivyo 10000 tu ?

Ndiyo maana nimesema hoja ya CHADEMA siyo wingi wa kura zinazowapa nafasi za viti maalumu bali ni uhalali wa kura zao zote walizopewa.
 
Asante kwa ushauri ambao pia hutuko tayari kuufata.

kukubali ushauri huu ni kuunga mkono ufedhuli uliofanywa na CCM na vijibwa vyake.
Acha uongo mmeshindwa kihalali. Mngekuwa na ushahidi magenta mahakamani
 
Kwa utawala huuu,,waache wajiendeshe wenyewe,, nafikiri sasa Tunduru itakuwa kama New York
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…