Tatizo kubwa siyo "Nyongeza ndogo" ya mshahara, tatizo kubwa kukatwa mpaka na vyama vya wafanyakazi (Rais Samia ondoa makato ya lazima ya vyama)

Tatizo kubwa siyo "Nyongeza ndogo" ya mshahara, tatizo kubwa kukatwa mpaka na vyama vya wafanyakazi (Rais Samia ondoa makato ya lazima ya vyama)

 
Ujinga ni huu Kuna ofisi za mahr sijui huduma za shirika au taasisi Kuna vyama ambazo unaweza kukaa mwaka usihudhurie hata kikao wala uongozi haujilikani sema wanalipana pesa nyingi


Utapelj mkubwa sana na dhulma vyana vyote eti mtu alipe ada kila mwezi na miongoni ni wafanyakazi wanakuwa na vyeo huko wanalipana mara mbili

Yaani Hr kazi yake ni nn kufuatilia performance tu na sio maslahi ya wafanyakzi
 

Walimu 347 Kigoma ruksa kujitoa CWT​

TUME ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), imekubali ombi la walimu 347 wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kujitoa kutoka katika Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ili kuanzisha chama kitakachotetea maslahi yao kutokana na madai kwamba chama hicho cha walimu hakikuwa na msaada kwao katika kutetea maslahi yao.

Akitoa uamuzi wa shauri hilo mjini Kigoma, mwamuzi wa shauri hilo, L.L Mwakyusa alisema baada ya mlolongo mzima wa uamuzi wa pande zinazohusika, Tume imeamua kuwa walalamikaji si wanachama wa CWT tena na kitabaki kuwa wakala kwa walalamikaji kwa kuwa ni chama pekee kinachotambuliwa na mwajiri.

Aidha, Mwakyusa alisema suala la makato kwa walimu hao linapaswa kuangaliwa upya kwa kuwa pande hizo zimeshaingia kwenye mgogoro na kwamba walimu hao hawatafaidi matunda halisi kama wanachama.

Pamoja na uamuzi wa kujitoa kwa walimu hao na kujiunga na chama kingine, alisema walimu hao wataendelea kukatwa ada ya uwakala ili kufaidi matunda ya masuala ya jumla kama walimu yatakayosimamiwa na CWT kwa mujibu wa kifungu cha 72 (c) cha Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini ya Mwaka 2004.

Akizungumzia hukumu hiyo, kiongozi wa kundi hilo la walimu, Kalimwabo Sabibi alisema pamoja na Tume hiyo kuridhia kujitoa CWT, wanakusudia kuanzisha chama kingine cha walimu kitakachosimamia maslahi yao.

Sabibi alisema kwa muda mrefu, walimu wamekuwa kama watoto yatima kutokana na CWT ambacho machoni kinaonekana kama kinasimamia maslahi yao, kudai hakifanyi chochote kwa ajili ya maslahi ya walimu.

Alisema walimu wamekuwa kwenye malumbano ya kudai maslahi yao kutoka kwa mwajiri badala ya chama hicho kuwa upande wao, wakati mwingine kimechangia kuwafanya wakose hata kile kidogo wanachodai.

Pamoja na hukumu hiyo, hata hivyo walimu hao wamesema hawajaridhishwa na uamuzi wa Tume kuruhusu kuendelea kukatwa kwa makato kutoka katika mishahara yao kwa ajili ya kuchangia CWT kwa kigezo cha ada ya uwakala wakati wao si wanachama wa chama hicho.
 
Labda itakuwa dunia yako tu
Vyama vya wafanyakazi ndio vinavyofikisha vilio vya wafanyakazi kwa waajiri
Sasa ukiviondoa mwajiri atapata maoni humu jamii forum??
Vyama vile vipo kisheria ingawa ni wazo la msingi kupunguza fee zao kutoka 2% hadi 1%
Ila vyama ni vya muhimu sana unaweza usielewe ila huo ndio ukweli

Ni kweli hivyo vyama vinafikisha vilio vya wafanyakazi? Kwa taarifa yako hizi kelele za mitandaoni kwa sasa zinasikilizwa kuliko kinachowasilishwa na hivyo vyama vya wafanyakazi. Hayo mavyama yako kutimiza formalities tu lakini hayana meno tena. Sana sana yako kuwafundisha wafanyakazi uoga.
 
Vyama vya wafanyakazi wasichukue pesa kwa asilimia bali wachukue kwa kiasi sawa bila kuzingatia asilimia

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hoja yako ni msingi kabisa kwani inasikitisha walimu wawili wanakatwa ada ya mwezi kwa viwango tofauti wakati huduma waipatayo kutoka kwenye cwt ni ya aina moja yenye kiwango sawa.Walimu waamke kwani wanaibiwa mchana kweupe
 
Back
Top Bottom