The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Hii ni ishara kuwa tatizo la ajira Tanzania ni kubwa sana.
Kati ya nafasi za ajira ya ualimu wa shule za msingi & sekondari 13,000 zilizotangazwa na serikali ikiwa ni kumjibu mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA ndugu, Tundu Lissu, takwimu zinaonesha kuwa mpaka kufikia leo Jumatatu tarehe 14.09.2020 feeder ilikuwa imeshapokea jumla ya maombi 80,000+!
Sijui itakuwaje tu kwa vijana hawa watakaoachwa.
Solution kubwa ya tatizo la ajira hapa nchini kwetu ni kwa serikali kutengeneza mazingira ya watu kuweza kujiajiri, kuilea na kuikuza sekta binafsi kwa sababu kwa vipimo vyote, serikali haiwezi na haina uwezo wa kuajiri watu wote wenye sifa za kuajirika. Hili katika sekta ya elimu linaithibitisha hoja hii.
Inasikitisha kuwa, tangu kuingia madarakani kwa ndugu John Pombe Magufuli 2015, ameitibua tibua sana sekta binafsi kiasi ambacho imetema watu wengi toka kwenye ajira rasmi na yenyewe kudorora kwa kiasi kikubwa.
Matokeo ya Sera za CCM ya Magufuli ni haya. Sasa hawa ni vijana wa taaluma ya ualimu tu waliozagaa mitaani.
Hatujui ni madaktari, manesi, wahasibu, wanasheria, wahandisi nk. Wangapi wamezagaa mitaani bila msaada wowote wa serikali kuwawezesha waajirike au wajiajiri.
Mzee Edward Ngiyai Lowassa kuna wakati fulani alionya kuwa, tatizo la ajira kwa vijana ni BOMU KUBWA linalosubiri kulipuka.