Tatizo la ajira Tanzania: Nafasi za Ajira ya Ualimu 13,000, waliotuma maombi kuziomba wafikia 80,000+ hadi leo!

Tatizo la ajira Tanzania: Nafasi za Ajira ya Ualimu 13,000, waliotuma maombi kuziomba wafikia 80,000+ hadi leo!

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Hii ni ishara kuwa tatizo la ajira Tanzania ni kubwa sana.

Kati ya nafasi za ajira ya ualimu wa shule za msingi & sekondari 13,000 zilizotangazwa na serikali ikiwa ni kumjibu mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA ndugu, Tundu Lissu, takwimu zinaonesha kuwa mpaka kufikia leo Jumatatu tarehe 14.09.2020 feeder ilikuwa imeshapokea jumla ya maombi 80,000+!

Sijui itakuwaje tu kwa vijana hawa watakaoachwa.

Solution kubwa ya tatizo la ajira hapa nchini kwetu ni kwa serikali kutengeneza mazingira ya watu kuweza kujiajiri, kuilea na kuikuza sekta binafsi kwa sababu kwa vipimo vyote, serikali haiwezi na haina uwezo wa kuajiri watu wote wenye sifa za kuajirika. Hili katika sekta ya elimu linaithibitisha hoja hii.

Inasikitisha kuwa, tangu kuingia madarakani kwa ndugu John Pombe Magufuli 2015, ameitibua tibua sana sekta binafsi kiasi ambacho imetema watu wengi toka kwenye ajira rasmi na yenyewe kudorora kwa kiasi kikubwa.

Matokeo ya Sera za CCM ya Magufuli ni haya. Sasa hawa ni vijana wa taaluma ya ualimu tu waliozagaa mitaani.

Hatujui ni madaktari, manesi, wahasibu, wanasheria, wahandisi nk. Wangapi wamezagaa mitaani bila msaada wowote wa serikali kuwawezesha waajirike au wajiajiri.

Mzee Edward Ngiyai Lowassa kuna wakati fulani alionya kuwa, tatizo la ajira kwa vijana ni BOMU KUBWA linalosubiri kulipuka.
 
Anayetakiwa kuajiriwa ni yule aliyefaulu kuanzia daraja la kwanza mpaka la tatu, walimu wengi ni watu waliofeli mitihani, tatizo wanazoa zoa tu. Na pia serikali haiwezi kuajiri kila anayehitimu, mambo mengne ni kudanganyana tuu. Vijana wanatakiwa wawe tuned kupambana na mtaa.
 
Anayetakiwa kuajiriwa ni Yule aliyefaulu kuanzia daraja la Kwanza mpak la tatu , walimu Weng ni watu waliofeli mitihan , tatizo wanazoa zoa tuu.... Na pia serikali haiwez kuajiri kila anayehitimu, mambo mengne ni kudanganyana tuu,....vijana wanatakiwa wawe tuned kupambana na mtaa
Una maanisha nini? Hivi kwa nini watu wanakuwa na mtazamo hasi kuwa walimu ni watu walioshindwa kufanya vizuri katika mitihani yao! Hili jambo si sahihi kabisa
 
Anayetakiwa kuajiriwa ni Yule aliyefaulu kuanzia daraja la Kwanza mpak la tatu , walimu Weng ni watu waliofeli mitihan , tatizo wanazoa zoa tuu.... Na pia serikali haiwez kuajiri kila anayehitimu, mambo mengne ni kudanganyana tuu,....vijana wanatakiwa wawe tuned kupambana na mtaa

We kweli akili huna, tangu lini serikali ikazoazoa? Mtu anayesoma ualimu si amedahiliwa na NACTE? NACTE si inafata vigezo vilivyowekwa na serikali?
 
Hii ni ishara kuwa tatizo la ajira Tanzania ni kubwa sana...

Kati ya nafasi za ajira ya ualimu wa shule za msingi & sekondari 13,000 zilizotangazwa na serikali ikiwa ni kumjibu mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA ndugu, Tundu Lissu, takwimu zinaonesha kuwa mpaka kufikia leo Jumatatu tarehe 14.09.2020 feeder ilikuwa imeshapokea jumla ya maombi 80,000+...
Historia inaonesha kiongozi pekee duniani aliyewahi kuwa na asilimia sifuri (0%) ya wasio na ajira akiwa madarakani ni Adolf Hitler pekee.
 
Anayetakiwa kuajiriwa ni Yule aliyefaulu kuanzia daraja la Kwanza mpak la tatu , walimu Weng ni watu waliofeli mitihan , tatizo wanazoa zoa tuu.... Na pia serikali haiwez kuajiri kila anayehitimu, mambo mengne ni kudanganyana tuu,....vijana wanatakiwa wawe tuned kupambana na mtaa
Umeelewa hoja ya mtoa mada?
 
Ccm ni ile ile

FB_IMG_16001027125266499.jpg

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Anayetakiwa kuajiriwa ni Yule aliyefaulu kuanzia daraja la Kwanza mpak la tatu , walimu Weng ni watu waliofeli mitihan , tatizo wanazoa zoa tuu.... Na pia serikali haiwez kuajiri kila anayehitimu, mambo mengne ni kudanganyana tuu,....vijana wanatakiwa wawe tuned kupambana na mtaa
Kikwete alikuwa ajiajiri walimu wote
 
Back
Top Bottom