Tatizo la kununua Umeme wa LUKU: Waziri Kalemani amsimamisha kazi kwa siku 10 Meneja wa TEHAMA wa TANESCO

Mbona wanamlaumu Madam wetu eti sauti yake ya upole?
 
Kuna wakati serikali hutafuta hasara sijui kwa faida ya Nani.

Serikali isitujaribu ktk huduma hii mhimu.
 
Hivi hiyo ndio solution yakuwasimamisha kazi.
Huko nikukariri kuwasimamia watumishi.
 
Siku 3 mtandao unasumbua
Hawa wakichekewa wanaweza
Kutupeleka hadi mwezi mzima
Na tatizo hili la mtandao

Ova
 
Hivi mama Samia miaka yako yote mitano ya kukaa chini ya JPM hukujifunza lolote? Pale siyo pahala pa kupendwa na kila mtu, usicheke na uzembe.
Huu ndio ushauri ambao mama anatakiwa kuufata.
 
Hapa bwana mbunge wa chato anajaribu tu kumdondoshea jumba bovu huyo mtu wa tehama, if it happened under his watch kwanza mhangaike kusort na kuli solve tatizo, kumsimamisha kazi ni sehemu ya uwajibikaji when the crisis is over. Gone are the days when ministers hold their responsibility kama mzee Mwinyi kipindi cha sukari iliyokwisha muda.
Umeme bado saa 9 hii mchana wa tarehe 19 may 2021 haununuliki na hela hazijarudishwa.
 
Kwanini wasielezee ndani ya masaa matatu? Siku kumi ni kuwapa mwanya kupanga mengi ya kudanganya tu..
TEHAMA ni papo papo.. hakuna ya masiku


Poleni msio na umeme majumbani kwenu.

Kazi iendelee..
Naona wewe unapeta siyo

Ova
 
Ingekua bora aturudishie huduma baadae mengine kuwafukuza kazi yafuatilie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…