Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake

Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake

Kwa kawaida kama huna tatizo la kutopata choo kitalaamu tunaliita (constipation) inatakiwa kwa siku uende mara moja au mara mbili. Pia choo unachopata kinatakiwa kiwe lain na sio kama cha mbuzi na kigumu ambacho ukienda kujisaidia mpaka unaumia.

Namna ya kutatua tatizo kwa mara moja ni kutumia juice ya ukwaju.. glasi hata 3 au hata 1Lt zna ukwaju baada ya muda kidogo utaona tumbo lishaanza kua mdebwedo then nenda chooni.
But kwa kusove tatizo lisikutokee fanya yafuatayo.
1. Kunywa maji ya kutosha nusu saa baada ya kula.. hakikisha mpaka jua limetua atleast 3 lts kwa maeneo ya joto kama dar.
NB: Unywaji maji unategemea na hali joto pia ya mahali husika bt maji ni lazima unjwe no matter what. Usiruhusu usikie kiu maana apo mwili unakua umekualert umepoteza maji kwa 1% mwln mwako.

2. Kula vyakula vyenje nyuzi nyuzi ( fibers) za kutosha na mboga mboga za majani. Pia zile nyama nyama za matunda zina fibre nyingi ambazo husaidia pia kulainisha choo.. usipendelee kunywa juice yake tuu..

3. Nafaka zilizokobolewa ni chanzo pia cha constipation mfano ( unga wa sembe na ngano iliyokobolewa). Tumia ugali wa dona na ngano isiyokobolewa..

LEO NIMETHUBUTU KU APPLY FORMULA YA UKWAJU KAMA ULIVYOIFAFANUA HAPO JUU KWAAJILI YA KUFUNGUA CHOO.

AISEE!!!! BAADA YA KAMA SAA 2 HIVI,,,,,, NILIONA TUMBO LINANIAMBIA NIWAHI TOI.
NILISHUSHA MZIGO WA MAANA PASI NA KUTOA MACHOZI.

TAKRIBANI MWEZI MZIMA NASUMBUKA KWA TATIZO LA KUFUNGA CHOO.
SHUKRANI SANA KWA ELIMU ULIYOTUGAWIA HUMU JF.
 
Just imagine mtu amekaa week nne hajapata choo. Huyu akijamba kwenye dalala lazima asababishe ajali [emoji23][emoji23][emoji23]
Niliwahi kaa bila kujisaidia 4 weeks ila niliyoyapitia haikuwa rahisi siku napata choo ilibidi ni celebrate.
 
Hello Doctors/ members,

Nahitaji msaada wenu juu ya tatizo la choo kigumu, ama kutokupata kabisa, yaani huwa napata shida nikienda maliwatoni, napata long call kwa tabu na ni kidogo na maumivu naamua kuahirisha zoezi tu nahofia nisije kupata hemorrhoids bure.

Nimeshauriwa kula vegetables, fruits, maji na for sure najitahidi sana ila bado mpaka nahisi nina kitambi cha vyakula vichafu yaani, nimefikiria vyakula nilivyokula since January na nilivyovitoa mpaka sasa hivi, kidogo sana, sijui nakwama wapi?

Naombeni ushauri wenu wapendwa,
Jumapili njema.
=====

MAONI YA WADAU:

Pole sana.
Nilikuwa na hilo tatizo pia, nikaja kugundua ni vidonda vya tumbo ambapo mara nyingi nikiwa natumia dawa(antibiotics kama doxy au cipro) ndio tatizo linakua kubwa sana, na nilikua nakula vzur mboga mboga na matunda.

Solution kwangu ikawa kuziepuka hizo dawa lakini pia KUFANYA MAZOEZI. Trust me ukiwa unafanya mazoezi na unakula matunda vizuri lazima uende toilet almost kila siku.
Hii unatoka nyumban unaenda kazini unakaa kwenye A/C siku nzima na unakula mivyakula yetu hii ya kibongo ni tatzo.
Pia juice ya ukwaju ni kiboko( isiwe chachu sana kama una vidonda vya tumbo).
All the best!
-------------
kunywa maji mengi na mbonga mboga zenye fibre kwa wingi

mboga zenye fibre ni zipi hizo?

Ni mboga zote jamii ya kunde kama vile maharage, njugu mawe, kunde mboga za jamii hiyo
ukifanya hivyo constipation itapita mbali ila ukipuuza husababisha kitu kinachoitwa homorroid (Bawasili) kwa kiswahili
-------------
To cut the story short, nenda pharmacy au duka la dawa la kawaida tu nunua dawa moja inaitwa bisacodril na tatizo limeshatatuliwa.

Mimi kuna kipindi nilipata hilo tatizo ilikua kama wiki nzima hadi kukaa au kutembea nilikua naumia kwaule ugumu nikaenda hospitali wakanipa hiyo dawa.

ni tudonge tudogodogo dizain yake kama priton ila reaction yake balaaaa. .kamoja asubuhi kengine jioni ila nilimeza kamoja tu ka asubuhi sijarudia ka jioni ila niliendesha balaa. . na tatizo liliisha kadonge kamoja tu just imagine

Cc Smart911
-------------
financial services,
1. Punguza matumizi ya nyama ng'ombe na mbuzi au kondoo
2. Kula dona na punguza ulaji wa sembe na wali
3. Dawa za minyoo kutumia mara ya mwisho lini? Tumia dawa za minyoo, tumia ketrax baada ya siku saba rudia dozi.
4. Jitahidi matunda na mboga za majani
5. Ratiba ya kula uifuate.
6. Muda wa kwenda toilet uwe na ratiba
 
Tumia juice ya ukwaju changanya na ubuyu weka sukari kidogo.

20191208_130726.jpeg
 
Kulingana na maelezo yako kwa kiasi kikubwa shida sio unachokula,
Huwenda unakula diet vizur
Ila tatizo ikawa ni una high metabolic rate mwilini.

Kanunue CHIA SEEDS. itakusaidia sana.

Mim ni doctor wa tiba asilia,
 
Kunywa maji 75% of faces is water, kula matunda na mboga za majani difestion take ni rahisi kuliko nyama

Ukiishiwa na maji kidogo mzigo unakuwa mgumu.
Thank you Dada, ila Maji nakunywa sana tena kwa kujilazimisha sometimes labda niongeze zaidi, na matunda nakula mfano jioni dinner yangu ni matunda nakula sana embe, papai na parachichi na maji, ila ndiyo hivo[emoji30] [emoji30]
 
Kulingana na maelezo yako kwa kiasi kikubwa shida sio unachokula,
Huwenda unakula diet vizur
Ila tatizo ikawa ni una high metabolic rate mwilini.

Kanunue CHIA SEEDS. itakusaidia sana.

Mim ni doctor wa tiba asilia,
Thank you, hivi hizo chia seeds zinatumikaje huwa naona ni kama vimbegu mbegu hivi?, vinasagwa ama?
 
Fanya ulivyoshauriwa na huyo, zaidi jitahidi kunywa maji sana. Kingine jitahidi kupunguza vyakula vya ngano sana mfano mandazi, sijui chapati n.k. Kula nafaka zingine kwa kiasi kidogo na kiasi kikubwa cha mboga za majani. Pole mtaalamu wetu wa mambo ya fedha
 
Thank you Dada, ila Maji nakunywa sana tena Kwa kujilazimisha sometimes labda niongeze zaidi, na matunda nakula mfano jioni dinner yangu ni matunda nakula sana embe,papai na parachichi na maji,ila ndyo hivo
emoji30.png
emoji30.png
Nanasi na machugwa ni fibre
Thank you Dada, ila Maji nakunywa sana tena Kwa kujilazimisha sometimes labda niongeze zaidi, na matunda nakula mfano jioni dinner yangu ni matunda nakula sana embe,papai na parachichi na maji,ila ndyo hivo[emoji30] [emoji30]
nanasi na machungwa ni fibres yatakusaidia zaidi
 
Back
Top Bottom