Tatizo la kupoteza uwezo wa kunusa (Kutosikia harufu): Fahamu chanzo na namna ya kutibu tatizo hili

Tatizo la kupoteza uwezo wa kunusa (Kutosikia harufu): Fahamu chanzo na namna ya kutibu tatizo hili

Habari wakuu,

Leo ni siku ya nane siskii harufu yoyote. Mwanzoni nilikuwa naona labda ni kawaida ila Leo nimeona huwenda litakuwa ni tatizo. Nimechukuwa dawa ya chooni ambayo harufu yake kawaida inakuwa kali sana,lakini baada ya kuimwaga chooni Mimi sijaskia harufu yoyote. Nikaamua kunusa iyo dawa kwa kuweka pua yangu kwenye mlango wa kigumu cha dawa hiyo lakini bado sijaskia harufu yoyote.

Siumwi, Niko fiti kabisa ila tatizo ndio hilo siwezi kuskia harufu ya kitu chochote.

Nisaidieni jamani kwa ambae alishawahi kupitia changamoto hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu ...Leo ni siku ya nane siskii harufu yoyote ..mwanzoni nilikuwa naona labda ni kawaida ila Leo nimeona huwenda litakuwa ni tatizo...
Hahaha hata mimi sijawahi KUSIKIA harufu, tumia pua siyo masikio kunusa harufu.
 
Wataalamu wanasema moja ya dalili ya corona ni kupoteza uwezo wa kunusa pia lakini muhimu nikuenda hospitali ukapate vipimo inaweza isiwe hata corona likawa ni tatizo lingine kabisa "sio kila homa ni malaria"
 
Hata hapa kijiweni kwangu kulikuwa na dada alikuwa hasikii harufu lakini siku hizi anasikia. Ni swala la muda litaisha tu korona inakuja na mambo mengi siyo lazima iwe covid 19
 
Siku ya Tatu Sina homa wala Nini hapo kabla sijapoteza uwezo wa kunusa na kutaste, nilipata kihoma hivi nikaumwa Sana na kichwa, Sema malimao na tangawizi nimeanza kujipigilia kitambo Sana Ila uwezo wa kunusa na kutaste ndio hola.

Mwanzoni kabisa sikusikia harufu ya sabuni flan hv huwa natumia kuogea nikahisi labda nimeuziwa Fake Sasa Ile nipo bafuni Nataka kuoga nikasogeza Hadi puani sisikii chochote nikamchukua kidole sugua Sanaa kwapa nikaleta puani Napo sisikii chochote ndio nikajua uwezo wa kunusa na kutaste hakuna kabisa...

Typed Using KIDOLE
 
Siku ya Tatu Sina homa wala Nini hapo kabla sijapoteza uwezo wa kunusa na kutaste, nilipata kihoma hivi nikaumwa Sana na kichwa, Sema malimao na tangawizi nimeanza kujipigilia kitambo Sana Ila uwezo wa kunusa na kutaste ndio hola...
Pole mkuu.
Utafika wakati...utanusa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilicho jifunza humu nikua mtu unaweza ukaumwa tumbo la kuharisha kisha uka avoid yale maumivu kwa kukajifariji kuwa siumwi tumbo la kuhara mimi ila nina upungufu wa maji mwilini. Ukaendelea na maisha yako na tumbo la kuhara lika disapper.
 
Back
Top Bottom