Soma aya ya mwisho boss kwenye uzi wangu juu ya sekta ya afya. Hivi unadhani hizo kazi zingekua chache wangekua wanafanya hivyo wanavyofanya??
Nadhani hapo unazungumzia ajira za halaiki (zile za afya zinazopitia TAMISEMI pamoja na ajira za ualimu wao kutokua na interview).
Mimi binafsi naamini katika ushindani wa wazi. Natamani sana ajira zote zitolewe kwa minajili hiyo (ya ushindani). Interview is the best tool to serve this purpose.
Lakini kuna mazingira mengine huwezi kufanyisha interview kulingana na wingi wa watu wanaotakiwa, muda wa kukamilisha mchakato huo wa ajira kuwa mfupi, n.k
Katika mazingira haya, unaweka vigezo fulani (specific criteria) utakavyotumia kumchukua huyu na kumuacha yule.
Hivyo basi, ili kutofanya upendeleo, unapaswa kuweka vigezo kweli vinavyopima merit, na kuvifuata vigezo hivyo.
Kwa ujumla ni kwamba wahitimu wote wa kozi za afya, wanao uwezo wa kufanya kazi za afya (wakiajiriwa). Wahitimu wote wa ualimu, wanao uwezo wa kufundisha (wakiajiriwa). Hili ni suala ambalo halina mashaka kabisa. Ila unapotakiwa kupata watu 20 kati ya 1000 waliosomea kozi fulani na kuihitimu, na ukaweka vigezo vya kuwachuja, kamwe haitamaanisha wale 980 watakaobaki wasingeweza kufanya kazi hiyo.
Tukirudi specific kwenye suala lako.
Let say wewe una shahada ya kwanza ya "
kupika uji" yenye GPA 4.5 na baadae ukahitimu shahada ya umahiri katika "
kupika uji" na kupata GPA ya 4.4
Sasa hutaki kuhojiwa (kufanyiwa interview), bali unataka kuitwa na kupewa mkataba uanze kufundisha. (Kama nimekuelewa).
Maswali yangu kwako:-
What if kuna watanzania wengine wana vigezo kama vyako.... Huoni kama wao watakua wamenyimwa fursa kwa wewe kupigiwa simu personally ukaanze kazi. (Tuchukulie nafasi ni hiyo hiyo moja).
Je, mambo (ya kupigiana simu mtu ukaanze kazi moja kwa moja) yakienda against your favour, nikapigiwa simu mimi badala ya wewe, huoni kama huo utaratibu utakua umekunyima wewe fursa ?
Kama nauliza vitu irrelevant na hoja yako, naomba niambie boss wangu.
Kwa sasa niishie hapa.