Nadhani lengo la usaili ni pamoja na yafuatayo:-
1. Kutenda haki ya uwazi na usawa (fairness and openness). Ukipigiwa simu watu watasema "ujomba ujomba" umetumika.
2. Kuchuja baina ya wengi (kama mko wengi mnaokidhi vigezo) ili kumpata aliye bora zaidi kwa ajili ya kazi husika.
3. Kujiridhisha juu ya uwezo wako wa kufundisha, kuelewesha, kulimudu darasa pamoja na kiwango chako cha kujiamini. Hivi ni vitu muhimu sana katika mkufunzi/mhadhiri lakini huwezi kuvitambua kwa kutumia ufaulu wa kwenye cheti (GPA).