Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Mkuu BAOSITA mdogo wangu anasema akikojoa kawaida anajisikia maumivu kwambaali kama vitu vinachoma choma kwenye uume nimepeleka regancy mpaka kafanya kipimo kinaitwa culture wapi katumia dawa wapi unaweza kuwa na dawa yake?
 
Nilisumbuliwa na mimi tumbo miaka kibao.Nimejaribu leo kama siku ya tatu sisikii maumivu tena,kwa kweli ndugu uliyetoa tiba kupitia jf Mungu akubariki sana.

Nafuu uliyopata inaitwa "placebo effect."

Asilimia 99 ya Watanzania hawajawahi kusikia kitu kinachoitwa "placebo effect."

Nchi ya watu ma-primitive tulionyimwa elimu, masikini weee, yani inaniuma kweli kweli nchi yangu.
 
Nafuu uliyopata inaitwa "placebo effect."

Asilimia 99 ya Watanzania hawajawahi kusikia kitu kinachoitwa "placebo effect."

Nchi ya watu ma-primitive tulionyimwa elimu, masikini weee, yani inaniuma kweli kweli nchi yangu.

Acha sifa za kijinga wewe...kwa kuwa wewe umechelewa kujua maana ya placebo basi unajua woote walikua hawaijui.

Kitunguu swaumu ni dawa,achilia mbali huu uzi!!!tena ukome kabisa kutu'underestimate wabongo.Baba yangu amekua akitumia vitunguu swaumu kwa muda mrefu sasa,na vimemsaidia saana,ingekua temporarily healing,ningeona matokeo yake,but he's fit na anendelea kuvitumia mpaka leo...
Punguza kuropoka.....................
 
Jinga hilo achana nalo, wewe labda ndio humjui. mipumbavu ipo mingi humu JF.
 
Asante mkuu Matola kwa kunifumbua macho..........!!!
Sasa mtu anayekwambia 99% hawajui kitu fulani halafu yeye 1% ndio anajuwa huwezi kugunduwa kama ana kaswende ya Ubongo!! huo utafiti aliufanya lini wapi na kwa sample zipi mpaka ajiridhishe hiyoo 99%
 

kaka sasa hiki kitunguu unakisaga chote baada ya kumenya?
Maana hujasema kama ni chote kizima? Mimi nakwenda leo kukitengeneza kisha nitakwambia
asante
 
kaka sasa hiki kitunguu unakisaga chote baada ya kumenya?
Maana hujasema kama ni chote kizima? Mimi nakwenda leo kukitengeneza kisha nitakwambia
asante
Siamini mtu anayeweza kuandika kiswahili akashindwa kusoma kiswahili.
 
Asante sana Mkuu BAOSITA, na mie ngoja nipite sokoni nipate hii kitu.Nafikiri pia ungepitia kule jukwaa la mapenzi, hii dawa naimani itawasaidia sana wale wote wanopenda kwenda UVINZA.
 
Acha sifa za kijinga wewe...
Bora nipate 'sifa za kijinga' lakini zikasaidia kuamsha jamii ya Watanzania wenzangu, kwamba jamani eeeh, tuanze kuondokana na waganga wa vitunguu na matabibu wa kienyeji! Tujijengee uwezo wa kieledi wa karne ya 21.

Baba yangu amekua akitumia vitunguu swaumu kwa muda mrefu sasa,na vimemsaidia saana,ingekua temporarily healing,ningeona matokeo yake
Hapana, baba yako peke yake hawezi kuwa kigezo cha "ningeona matokeo yake"! Ilibidi uchukue baba yako na wajomba zako na ukoo wenu mzima na majirani na ushee mle "dawa" na wengine wanywe placebo na wengine wawe control group na mpimwe kwa muda unaorekodiwa kieledi. Vinginevyo observation yako ni ya ki "profesa maji marefu"!

kwa kuwa wewe umechelewa kujua maana ya placebo basi unajua woote walikua hawaijui.
Bora mimi niliechelewa kujua kuliko mamilioni ambao mpaka leo hawajui, ndo maana akitokia kibabu kimoja ambacho kuandika jina lake hajui akawaambia amewagundulieni dawa ya kutibu kila ugonjwa basi Watanzania wote rrrrrrrrrr... kwa kibabu!... placebo effect ikiisha mnaanza kukisakama kibabu kiwalipe!.... kizazi kilichonyimwa elimu, a wasted generation!

Jamani, zaidi ya hisabati hakuna somo ambalo kila Mtanzania lazima alisome mpaka Form IV, isipokuwa Biology, lakini watu kwa mamilioni bado hawaelewi the basic fundaments of microbes and diseases.... kizazi cha babu wa Liliondo, mnaenda kupewa dawa ya kipindupindu na minyoo halafu mkiwa kwenye foleni kusubiri dawa mnalala pembeni ya kinyeshi na inzi halafu wagonjwa wote wenye kuhara na kutapika wanakunywa dawa kwenye kikombe hicho hicho! dawa nini? maji ya imani! A primitive generation!
 

Usinitafutie BAN ya rejareja!!!!Kila la heri mwanasayansi wa ukweeenhee!!
 

mkuu nashukuru kwa msaada wa dawa napenda kuuliza je naweza kuitumia kama kinga labda kila mwezi msaada tafadhali
 
Nimetumia hii dawa kwa kweli ni dawa.Mara ya kwanza nilitaka kutapika,lakini sikutapika.Nina wiki sasa na mabadiliko nayaona,nilikuwa na tatizo la fungus miguuni,naona sasa wanakauka.Asante sana mkuu
 
samahani mkuu haina madhara kwa mwenye vidonda vya tumbo mana kuna mtu ametumia imemsaidia lakina anasema imemchoma sana tumbo
 
Kiongozi nashukuru kwa ushauri wako. Kitunguu saumu ni dawa ya vitu vingi sana jamani msidharau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…