Mukulu wa Bakulu
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 4,051
- 12,954
Asikwambie mtu kuhusu kupoteza uwezo wa kusikia. Imenitokea kidogo ila shida yake acha kabisa.
Nilipata matatizo ya sikio langu la kulia kupoteza uwezo wake wa kusikia bila sababu, ilianza taratibu kidogo kidogo ghafla nikajikuta sikio limepoteza karbu 75% ya uwezo wake wa kusikia.
Nikawa natumia sikio moja tu la kushoto. Ila asikwambie mtu, shida niliyokua naipata kwa kusikilizia sikio moja haina mfano, kwenye TV naweka sauti kubwa, naongea kwa sauti kubwa yani ilikua tabu tupu.
Nashukuru nilienda Muhimbili wakanipima, wakanipa dawa baada ya wiki moja nikarejea katika hali yangu ya kawaida.
Najiuliza kama mimi ilikua sikio moja tu na halikupiteza uwezo wake wa kusikia 100%, inakuaje wenye hali kama hiyo masikio yote au uwezo wao wa kusikia uko impaired?
Tulinde masikio yetu, pamba za kusafisha masikio tuachane nazo kabisa. Earphone na ujinga ujinga wote unaohusisha masikio.
Poleni sana wote wenye matatizo ya masikio. Ukisikia shida kidogo kwenye sikio kimbia umuone daktari, unawez kua kiziwi kabisa.
Kwa hapa Dar clinic karibu zote za masikio wataalamu wanatoka muhimbili, wafuate huko huko.