Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Asikwambie mtu kuhusu kupoteza uwezo wa kusikia. Imenitokea kidogo ila shida yake acha kabisa.

Nilipata matatizo ya sikio langu la kulia kupoteza uwezo wake wa kusikia bila sababu, ilianza taratibu kidogo kidogo ghafla nikajikuta sikio limepoteza karbu 75% ya uwezo wake wa kusikia.

Nikawa natumia sikio moja tu la kushoto. Ila asikwambie mtu, shida niliyokua naipata kwa kusikilizia sikio moja haina mfano, kwenye TV naweka sauti kubwa, naongea kwa sauti kubwa yani ilikua tabu tupu.

Nashukuru nilienda Muhimbili wakanipima, wakanipa dawa baada ya wiki moja nikarejea katika hali yangu ya kawaida.

Najiuliza kama mimi ilikua sikio moja tu na halikupiteza uwezo wake wa kusikia 100%, inakuaje wenye hali kama hiyo masikio yote au uwezo wao wa kusikia uko impaired?

Tulinde masikio yetu, pamba za kusafisha masikio tuachane nazo kabisa. Earphone na ujinga ujinga wote unaohusisha masikio.

Poleni sana wote wenye matatizo ya masikio. Ukisikia shida kidogo kwenye sikio kimbia umuone daktari, unawez kua kiziwi kabisa.

Kwa hapa Dar clinic karibu zote za masikio wataalamu wanatoka muhimbili, wafuate huko huko.
 
Twambie sababu ya we we kupata tatizo hilo tujilinde na ulipewa dawa gani? Kuna mtoto hapa alipata homa kali mpaka aka pata stroke akaenda muhimbili hapo hapo. hasi kii mpaka akutazame usoni na anaongea kwa sauti kubwa. Uwezo wake darasani umeshuka alikuwa anaenda mwenyewe hivi sasa lazima umpeleke na kumrudisha.
 
Pole mkuu ila hata ukijikwaa kidoleni kuna utofauti utausikia within a second au hata dakika kadhaa kwenye jeraha.Kuhusu matatzo ya uziwi vivyo hivyo kwa walioupata ukubwani lazima wapate shida siku za mwanzoni ila kwa sisi ambao tumezaliwa nao hatuoni tabu tena tunajihisi tupo ulimwengu maridhawa kuliko ninyi wazima.
 
Twambie sababu ya we we kupata tatizo hilo tujilinde na ulipewa dawa gani? Kuna mtoto hapa alipata homa kali mpaka aka pata stroke akaenda muhimbili hapo hapo. hasi kii mpaka akutazame usoni na anaongea kwa sauti kubwa. Uwezo wake darasani umeshuka alikuwa anaenda mwenyewe hivi sasa lazima umpeleke na kumrudisha.
Mkuu tatizo lilianza baada ya kupata mafua. Siku kadhaa mbele nikaanza kuhisi sikio halisikii vizuri.

Nikaenda pharmacy wakanipa zile dawa za matone ila sikio likaanza kuuma kwa ndani mara gafla uwezo wa kusikia ukaanza kupungua ghafla.

Dawa nilizopewa zinatokana na jinsi dokta alivyoona.
 
Asante kwa kutupa pole wale tusikiao kwa sikio moja. Sikuwa najua kwamba Binadamu husikia kwa masikio yote mawili na hivyo sikuwa na wasiwasi hadi pale nilipoanza shule ndio nikagundua matatizo niliyozaliwa nayo. Namshukuru Mungu kwa kunifikisha hapa nilipo leo ingawa kwa sasa uwezo wa kusikia unazidi kupungua.
 
Hiyo shida noma mie nilipata ukubwani asee ni kasheshe.
Sehemu nyingi unabaguliwa hususani kwny mambo ya ajira wakijua tu wanakutema fasta.
Na pia inaumiza sana ndugu wakiona zaman mlikua mnaongea vizuri afu ghafla husikii ni shida kwa kweli.
 
Sijui uje uwaambie hawa watoto hapa chuo, maana naona kila mtu ameweka vitu masikioni
 
Hata mimi liliwahi nisumbua zaidi ya miaka mitano ila nilipata dawa na sasa nimepona kabisa. Fuata maelezo haya hapa: Chukua kinyesi cha kobe na cha kinyongakwa uwiano wa 1/1 yaani kama kinyesi cha kinyonga ni nusu kilo basi cha kobe nacho kiwe nusukilo, vilivyo kauka zaidi ya siku nne weka katika kitwangio unaweza tumia grander twanga hadi upate unga laini changanya huo unga na maji lita tatu(kwa unga kilo moja), tia asali robo kilo chemsha hadi yabaki maji maji kiasi ya lita moja chuja kunywa robo glasi mara mbili kwa siku na dondeshea matone mawili ya hio dawa mara mbili kwa siku kwa muda wa siko nne utapona kabisa. Kama utashindwa kutengeneza hio dawa wasiliana na mimi kwa namba 0762155947
Na ile ya kutokusikia vizuri unayo mkuu?
 
Kinyesi cha kobe duh. mtakuja toboa ngoma afu unakuwa kiziwi moja kwa moja. kutibu uambukizo sugu wa sikio tumia Ciprofloxacine ear drop mara mbili kwa siku. na kabla ya kuweka dawa safisha sikio vizuri kwa kitambaa safi unatengeneza kama utambi. au unaweza tumia cotton buds.
 
Habari wakuu,

Naamini Mungu bado anatupenda na kutupa uzima ndo maana tunakutana hapa

Samahan naomba kuuliza hii hali ya kusikia kelele nyingi masikioni( kama mashine ya kusaga mahindi) n hali ambayo natakiwa kuikubali na kuishi nayo?

Hali hii ilianza mwaka juzi(2016) na nmetumia dawa nyingi lakin sion mafanikio. Kuna wakat nashindwa hata kufanya kazi kwa sababu ya usikivu kuwa mdogo kwa sababu ya kelele hizi. Hivi naandika uzi huu ikiwa ni siku chache tangu niache kibarua changu kwa sababu ya shida Hii

Najaribu kufikir kama swala hili n halipon (kama wengi wasemavyo) bas nitaishi maisha ya namna gan
Najikuta nakata hata tamaa ya kuishi

Naomben mtazamo wenu ndugu zangu kama kuna mtu anaijua hii shida au alishawahi kukutana nayo na aliipona vipi

Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anza maombi na nivizuri ukaanza kwa kujifungua mwenyewe kwanza hiyo hali itapona kwa imani kwa kuwa MUNGU wetu hakuna analoshindwa.
 
Back
Top Bottom