Wakuu, natumai mu wazima.
Kwa muda wa miezi miwili sasa nasumbuliwa na miguu ambapo inawaka moto na joints za vidole vya miguu zinauma balaa, maumivu yanaanzia kwenye angle lakini kuanzia hapo kurudi juu (hadi kichwani) niko sawa.
Nimeenda hospitali tatu tofauti mara tano lakini hawaoni ugonjwa na nimepima damu,stool na haja ndogo lakini majibu yanaletwa ni kwamba hawaoni tatizo. Siwezi kuvaa viatu kwani ni kama moto unawaka haswa huku kwenye kucha zinapootea miguu haina uvimbe wowote.
Kwa yeyote mwenye wazo la kunisaidia anakaribishwa ili mwenzenu niendelee na masomo vizuri kwani mimi ni mwanafunzi wa chuo mwaka wa kwanza.
Naomba kuwasilisha.