Tatizo la mimba kwa wanafunzi Tanzania nini kifanyike?

Tatizo la mimba kwa wanafunzi Tanzania nini kifanyike?

Kwa upande wako wewe unashauri serikali ifanye nini ili iondoe au ipunguze hiyo kadhia ya wanafunzi kupewa mimba?

Mkuu kwanza tatizo hapa kwa upande wangu siyo serikali ifanye nini bali jamii ifanye nini. Hili ni tatizo la kijamii zaidi kuliko la kisiasa japo wanasiasa (serikali) wana la kufanya pia. Kwa upande wa serikali ni muhimu shule zikawa karibu na maeneno ya wanafunzi hebu chukulia mtoto anatoka chanika kwenda kusoma Buguruni na usafiri ulivyo wa shida lazima baadaye kondakta au dereva apate mke. Shida uhamisho kwa wanafunzi wa mitihani yaani drs la 4, drs la 7 , form 2 na form 4 imekuwa kanakwamba haiwezekani bado ila nadhani serikali ingefanya kila linalowezekana shule ziwe karibu mno na wanafunzi. Shule za kata halijaweza kutatua tatizo hili maana mfano kijijini kwetu kata yetu ina vijiji 5 bado shule ya kata iko mbali mno na vijiji vingine.
 
Amin amin nakwambia ukiona tunda limeliwa ujue lishaiva ya nini uteseke

Mkuu tunda la mwanafunzi wa primary au secondary linaivaje? hebu chukulia hilo tunda ni mwanao au mdogo wako. Hivi jamii yetu inaelekea wapi kwa fikra kama hizi zako?
 
Wa

Wanaume badilikeni acheni kutembea na wanafunzi. Solution ndio hiyo hakuna nyingine.
Hili tatizo halitaisha milele.

Aksante sana dada lazima jamii irudi kwenye mstari yaani mtoto wa mtu awe wa jamii nzima. Kama unaona mtu anatembea na mwanafunzi jamii ikemee bila kujali nani ni mzazi au ndg wa huyo mwanafunzi. Jamii iwe na haki ya kumkemea mwanafunzi yeyote anayefanya uhuni na wazazi wake wakileta mbwembwe wawekwe selo kwanza masaa 24 akili ziwakae sawa.
 
Mkuu tunda la mwanafunzi wa primary au secondary linaivaje? hebu chukulia hilo tunda ni mwanao au mdogo wako. Hivi jamii yetu inaelekea wapi kwa fikra kama hizi zako?
Usishangae. Probably hata yeye alilawitiwa akiwa ana umri mdogo ndio maana anaonesha tabia za ajabu za kingono as a traumatic effect!
 
Bint anamiaka 16
ashatoa mimba zaidi ya 7....!!!!

Hatari sana
Uswahilini vitoto vingi miaka 14 hadi 16 inatiana sana na vinatoa sana mimba na vingine vinagawa nyuma....
 
Wanafunzi wote wa kike wachomwe sindano maalumu ya kuchelewesha balehe kwa miaka 10 mbele. Yani mtoto wa kike abelehe akiwa na umri wa miaka 20. Namuomba mkuu wa nchi asimamie hili jambo kama alivyopambana kusimamia Tanzania ya viwanda. Utawala wake huu amefanya mambo makubwa sana hawezi kushindwa na hili.


Mkuu nini inaweza kuwa side effects za hiyo sindano? na je hii haitakuwa kukiuka haki za msingi za binadamu za kubalehe na hata kuvunja katiba ya nchi kwa kuingilia privacy za mtoto wa kike?. Usije ukawapa ulaji watetezi wa haki za binadamu
 
Haya mambo yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na jamii yenyewe. Unakuta binti mwanafunzi amepewa mimba na familia zinaamua kuyamaliza bila kuyafikisha kwenye vyombo vya sheria au wakati mwengine suala linafika hadi mahakamani lakini familia ya mhanga (binti) wanakataa kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa aidha kumtorosha binti au kumrubuni asitoe ushahidi kwa ushawishi wa familia au mtuhumiwa mwenyewe. Kigezo kinachotumika kwa hizo familia ni je, kama baba wa mtoto atafungwa, mtoto atalelewa na nani ikiwemi huduka muhimu. So familia hujikuta zikiyamaliza haya mambo nyumbani na ndio chanzo cha visa hivi kutoisha maana watuhumiwa wanajua watayamaliza tu

Pamoja na hiyo ya mtoto kulelewa na nani pia kuna kuoneana aibu na kutotaka uhasama, yaani familia ya muathirika wanafikiri wataleta uhasama na familia ya mtenda kosa si unajua vijijini watu wanaishi kama ndugu na kwa asilimia kubwa watu wa kijiji kimoja wanaweza kuwa na uhusiano wa kindugu kabisa kwa % kubwa sasa wanaona ni bora wafunike kombe. Hapa inatakiwa wazazi wakigundulika walihusika kwa namna yeyote wapigwe jela mwaka au miezi sita wakirudi wawe shuhuda
 
Wa

Wanaume badilikeni acheni kutembea na wanafunzi. Solution ndio hiyo hakuna nyingine.
Hili tatizo halitaisha milele.
Unawaambiaje wanaume ambao ni wanafunzi na wanawapa mimba wanafunzi wenzao?
Tambua kwamba,hamu yakufanya mapenzi huongezeka mara baada ya mtu kubalehe na siyo baada yakumaliza shule.
 
Pia elimu izidi kutolewa kila sehemu,majumbani,shuleni nk..
Pia serikali iandae mikutano ya mara kwa mara kwaajili ya kuelimisha jamii kuhusu hii ishu.
 
Wanataka wenyewe. Wakati mwingine wanaomba hela tunawapa,lift tunawapakia,mwisho wanaomba pen...zi tunawakatalia,wanaanza kulia tunawahurumia tunawapa.

Mkuu acha uongo watu wenye tabia kama zako ndiyo hurubuni watoto kwa lift na vipesa vya maandazi kisha mnawapa mimba then mnawatelekeza. Kwanini ukubali kufanye naye mapenzi huku ukijua ni mtoto bado?
 
Elimu juu ya uzazi wa mpango itolewe mapema na wazazi wasione aibu kuzungumza na watoto wao.

Mtoto wa mwenzio ni wako pia tusaidiane kwenye malezi.
 
Serikali kuna sehemu inakosea hasa kwenye upande wa hukumu kugusa wanaume peke yao,ni muda sasa serikali nayo kuwaangalia hawa wanawake.

Kama nao wanawake wangekuwa kwenye sehemu ya hukumu hata kidogo nao wangeogopa zaidi,ila kwakuwa wanajua hukumu ipo kwa wanaume tu so wao hawajali sana

Mkuu nadhani iko hivyo kwasababu mtoto wa miaka chini ya 18 anahesabika kabakwa ,kwahiyo ile hukumu ni kwasababu wewe ni mbakaji. Hakuna mkataba kwa minor , kwahiyo ni ama ulimrubuni, ulimtishia au ulitumia nguvu maana ni mtoto mbele ya macho ya sheria hivyo yeye hawezi kufungwa maana inaonekana alibakwa
 
Sheria katika suala la hisia za ngono bado nitatizo.
Tatizo ni chanzo cha malezi nyumbani na changamoto ya utandawazi .

Mkuu nini kifanyike sasa maana kwakweli sheria kwenye mambo ya hisia ni changamoto
 
Hali ni mbaya kiukweli selikali iingilie Kati suala hili

Serikali ifanye nini ambacho unadhani hawajakifanya? nini nafasi ya taasisi za dini kwenye hili? nini nafasi ya jamii kama wewe kutokomeza mimba za utotoni? Je, wewe mwenyewe huwarubuni wanafunzi wa kike ?
 
Mkuu tunda la mwanafunzi wa primary au secondary linaivaje? hebu chukulia hilo tunda ni mwanao au mdogo wako. Hivi jamii yetu inaelekea wapi kwa fikra kama hizi zako?
Ukiona hii situation imetokea ujue kulikuwa na makubaliano otherwise binti aweamebakwa. Sasa huyo wa sekondari au primary anafanya kitu hiko akijua fika kuna side effect ukiachana na uroda ambao anaupata aidha kwa kujitakia au kukubali kushawishiwa. Kinacho matter hapa sanasana ni malezi, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo elimu katika ngazi ya familia ni muhimu sana kama unamuacha binti yako anazurura ovyo ovyo si mchana si usiku what do yo expect. Pia binti mwenyewe akijielewa kwa kumshtaki anaye mrubuni haraka iwezekanavyo haya mambo yata pungua kwa kasi kubwa

Pia na hili swala la kumfunga aliye tia mimba pekeyake naona si sahihi mi naona na aliye pewa mimba yane awajibike kwasababu swala la mapenzi ni makubaliano ya watu wawili hivyo pia wote wawili wawajibishwe kikamilifu.
 
Usishangae. Probably hata yeye alilawitiwa akiwa ana umri mdogo ndio maana anaonesha tabia za ajabu za kingono as a traumatic effect!

Unajua ni ajabu sana mtu mzima mwenye akili timamu kushabiakia ujinga na kitu ambacho kinasababishia jamii maumivu . Kuna watoto wanafariki wakati wa kujifungua halafu mtu anasapoti ujinga bora umemjibu
 
Mkuu umeongea uhalisia,cha kwanza kinacho takiwa kulaumiwa ni serikali kwa sababu binti anapopata mimba wao wanakimbilia kumtafuta muhusika wampate na baadae wamhukumu miaka 30 huku malezi ya mama na mtoto yakiachwa kwa wazazi wa binti,nadhani hata kama ni wewe usingekubali jambo hili,

Kinachotakiwa kwa sasa ni kutunga sheria ambayo eidha serikali iwajibike kwa malezi ya mama na mtoto au na binti naye ahusike katika adhabu hili litasaidia kuhamasisha mabinti wajichunge wasipate mimba

Lakini pia kwa kuongezea niseme kuwa Mimi ni mwalimu , tangu niaze kufundisha, mimba zilizotokea nikiwa kama mwalimu si chini ya 50 lakini hakuna hata mmoja wa watia mimba ambaye amewahi kuhukumiwa kwa kosa la kumpatia mimba binti hiii ni kutokana na serikali kukwepa kuhudumia gharama za malezi kwa binti na mtoto baaba ya kupata mimba ,wazazi wengi wamekuwa wakikaa meza moja na watia mimba na kumalizana kimya kimya,hebu jiulize binti yako ametiwa mimba na kijana akiwa masomoni, umetumia gharama kubwa na baadae mtia mimba anakuja na kutaka myamalize japo kwa malipo kidogo ,nadhani Mimi kama mzazi nitakubali ili nipunguze gharama na baadae baba wa mtoto ataendelea kumhudumia mtoto sio kumfunga mtia mimba na baadae jukumu la malezi ya mtoto na mjukuu linaachwa kwangu.
Haya mambo yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na jamii yenyewe. Unakuta binti mwanafunzi amepewa mimba na familia zinaamua kuyamaliza bila kuyafikisha kwenye vyombo vya sheria au wakati mwengine suala linafika hadi mahakamani lakini familia ya mhanga (binti) wanakataa kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa aidha kumtorosha binti au kumrubuni asitoe ushahidi kwa ushawishi wa familia au mtuhumiwa mwenyewe. Kigezo kinachotumika kwa hizo familia ni je, kama baba wa mtoto atafungwa, mtoto atalelewa na nani ikiwemi huduka muhimu. So familia hujikuta zikiyamaliza haya mambo nyumbani na ndio chanzo cha visa hivi kutoisha maana watuhumiwa wanajua watayamaliza tu
 
Wafute mtaala wa somo la biolojia maana vijana wanaenda field sana
 
Elimu juu ya uzazi wa mpango itolewe mapema na wazazi wasione aibu kuzungumza na watoto wao.

Mtoto wa mwenzio ni wako pia tusaidiane kwenye malezi.

Everhurt hawa watoto wetu wakifundishwa elimu ya uzazi wa mpango si ndiyo itakuwa balaa kubwa, kuna mama ndugu yangu juzi kampata mwanaye na vidonge vya uzazi wa mpango na vingine wanaita P2 akaishia kuzimia maana mtoto mwenyewe yuko form 3
 
Back
Top Bottom