Hili swala ni gumu sana kumaliza kuliko watu wanavyolichukulia. Niwape mfano hai . Nikiwa mwaka 2 chuoni 2003 hakukuwepo badoo,facebook, whatsap...enzi hizo. Nilibahatika kupata temporary employment shule moja ya kanisa kijiji fulani. Nilikua nafundisha form2 & 4. Shule ilikua kijijini kweli km 60-70 kutoka mjini. Kulikua na usafiri wa bus linatoka saa 11 alfajiri kwenda mjini na kugeuza saa saba kurudi kijijini. Shule ilikua ya boarding. Wanafunzi wa kiume walikua wanatupenda maana na sisi tulikua wadogo ,ila walikua wanatuheshimu sana. Wanafunzi wa kike ilikua shida . Alikua anaweza kukufuata anakwambia mwalimu nimechoka kukaa huku porini naomba ijumaa nauli niombe permission kwamba naumwa naenda mjini kwa mama mdogo ,halafu unipe number uniambie nikukute wapi,tukae mpaka j'pili turudi kila mtu kivyake. Na hii was very popular sana .A-level was more worse kwa sababu mpaka wengine ile recess ya pasaka walikua wanaenda kukodi vyumba guest mjini na kujiuza.Na vijana wa vyuo tuliokua pamoja walifanya yao ,na wengine hawakuta kujichafua. Kwa hali hii kama alivyosema ndugu yangu hapo juu,sheria ikate pande zote wanawake kwa waschana. Maana wanafunzi hao walikua wanataka mtu wa kuwapeleka kula chips na kubadili mazingira ya shuleni tu. Wanafunzi wako victims kwa sababu hawaombi hata hela nyingi . So Serekali iweke ugumu kwa pande zote ,watoto ,wazazi wa kike na wakiume .Angalau wataweza kupunguza.Mtoto akipewa mimba afungwe na mzazi wake , wa kiume pia iwe hivyo. Ni maoni yangu kama mdau