Tatizo la mimba kwa wanafunzi Tanzania nini kifanyike?

Waache kuwa na viherehere.
 
Hapo unazungumzia kama aliyempa mimba ni mwanafunzi mwenzie au mbaba mwenye ukomavu wake? Namaanisha hiyo ya mtoto mwenye mimba na yeye afungwe walau miaka 10
Awe aliyempa mimba ni baba mwenye ukomavu wake ( kwa maneno yako) au mwanafunzi mwenziye.
 
Apo kwa mzazi napinga , inamaana mzazi atakua anakagua mtoto kua Ni 0 km Kila siku.
 
Unawaambiaje wanaume ambao ni wanafunzi na wanawapa mimba wanafunzi wenzao?
Tambua kwamba,hamu yakufanya mapenzi huongezeka mara baada ya mtu kubalehe na siyo baada yakumaliza shule.
Siwezi waambia kitu, ni tabia za mwanadamu zisizorekebishika
 
Ukweli Ni kwamba haitawezekana jamii kurudi kwenye mstari, dunia ndo kwanza inaenda kasi
 
Mwanafunzi wa kike unakuta anamiliki simu Mzazi hajui, wala Mwalimu hajui

Jiulize nani kamnunulia na huwa anaongea na nani na muda gani wana akili sana ktk hilo na ni wasiri kupindukia

Halafu wanapenda sana kuchat ni balaa wanaweza kuchat tangu asubuh had usiku wa manane
 
Hivi nchi za ulaya huwa wanasolve vipi tatizo la mimba kwa wanafunzi/utotoni? au hawana hilo janga?
 
Umaskini/Ufukara ni chanzo cha shida nyingi sana...
 
Wazazi waamke, kazi sio kuzaa tu ni malezi
 
Ingekuwa kuwafunga watu kunapunguza kasi ya utendaji wa makosa jela zingekuwa tupu.

Jela sio solution.
 

Nashauri CCM ibadili sera zake kuhusu mimba..vile vile libuniwe kofuli maalum kwa wanafunzi wa kike na funguo za kofuli husika ziwekwe B.O.T hadi binti ahitimu shahada ya kwanza chuo kikuu ndipo akabidhiwe
 
Mara nyingi wanafunzi wanaipata mimba wengi wao n wale ambao shule wanaenda tuu ilimradi sio kwa kusud la elimu. So utawakuta wao wanaongoza wa uhuni mashuleni na kwenda chimbo. Imagine mtoto wa kike anatoka nyumban kwenda shule lkn anaishia mtaan kwa vidume mwenyewe kabsa bila kulazimishwa.

Lkn kingine n hali za uchumi, mtoto anataman awe kama wenzake ambao wazaz wao wapo vizur kipesa, hicho ni chanzo cha kuanza kukubali kushawishiwa na vijana wa mtaan ili nae awe na nguo nzur, viatu na mengineyo.

Mwisho n huu utandawazi, sahz picha ngono mtadanoni zinapatikana kama nyanya gengeni. Sasa hawa watoto wa sekondar nao wanataman kuonja utamu mwishowe wanaishia huko.

Suluhisho, wazaz wajitahid kuwaelimisha watoto wao tangu wakiwa wadogo, lkn pia wazaz wajitahid kutafuta pesa ili watoto wao wasirubunike kirahis. Pia tuwaombee hawa watoto pepo la tamaa ya ngono liwatoke, Mungu awalinde na vishawishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…