Tatizo la Tanzania ni kudhani kwamba Watoto wa viongozi nao wanaweza kuwa viongozi

Tatizo la Tanzania ni kudhani kwamba Watoto wa viongozi nao wanaweza kuwa viongozi

Haya ni matusi makubwa tu dhidi ya Nchi yetu. Jamii zetu, mila zetu, jadi zetu, yaani Tamaduni zetu.

Ni watu wa Nchi gani hizo ambazo hawawaandai watoto zao kuwa Viongozi?

Ni mzazi gani huyo ambaye hataki mwanae apate mafanikio?

Hatahivyo

Uingereza? Huko ndiko mambo haya yapo zaidi likija la 'nepotism' The Churchills, The Johnsons hata Wajerumani...The Merkels

Marekani ndio usiseme: Historia haiozi-Familia za Raisi wa pili wa Marekani John Adams mwanae baadae akawa Raisi, kuna Bill Clinton na Mkewe na mtoto wao Chelsea nae yumo mumohumo. The Bushes, The Kennedys, The Roosevelts, hata Donald Trump yumo. Kuanzia wanawe mpaka wakwe...na listi ni kubwa tu tunaweza kesha hapa kuwataja wote.

Chakushangaza zaidi....

CHADEMA kupitia mamluki wao kutoka nje ya nchi yetu Erythrocyte wanaleta siasa za Nje kutuvuruga. Deflecting and Blaming matatizo ya nepotism ya kwao na kuyafanya ya kwetu.

I say BOGUS.

Ukweli ni huu, ukilinganisha na Afrika utaona tulikuwa na mwenendo tofauti kabisa.

Mifumo yetu ya kijimuiya au ya kikabila haikuruhusu 'Nepotism'

Nani anabisha?

Itoshe, wakoloni walivyokuja, walivuruga mifumo yetu ya jadi. Mifumo ya Kiserikali, Mifumo ya Demokrasia... Sio hivyo tu, wakoloni ndio walioleta mifumo hii ya upendeleo na athari zake zinaonekana sasa.

Nani anabisha?

Ni hivi, mizizi ya Nepotism yametokea Ulaya, na ndipo huko mnataka tufuate mpaka tamaduni na jadi zao, eti ndio tupate maendeleo, sasa haya yanatokea, mnatukana Jamii zetu! Hamtaki mliyotufundisha?

Hata neno nepotism limetoka Ulaya🙌🏾

Nyie CHADEMA na mamluki wenu wacheni kuleta za kuleta.

Uzeni Sera msikilizwe na sio kulalama lalama wakati wote.
 
Natofautiana na wewe kwa hili. Siyo kweli kuwa watanzania tunadhani watoto wa viongozi nao wanaweza kuwa viongozi wa kesho. Sema viongozi wenyewe ndivyo wanavyofikiri hivyo na wanataka iwe hivyo. Na wanaweka wigo watu nje ya hapo hawaymtakiwi kusogelea kabisa.
 
Ery vipi mbona hupaparikiii ya kibu Denis kama unavofanyaga Kwa taarifa zenye sintofahamu kuhus Yanga?
 
Tatizo ni katiba bovu, Nyerere alifikiri kila mtu ana akili kama yake na hakuna mtu ata take advantage ya mfumo kujineemesha, was a big mistake na hawa wa sasa wakipata cheo wanafikiri wako anointed na vizazi vyao vyote vijavyo, tunahitaji check and balance kuzuia huu ujinga
Ni muhimu sana kubalance mambo
 
Hapo ndipo tunapojikuta tunataabika na kuokota Magarasa na kuyapa uongozi.

Uongozi ni Karama kutoka kwa Mungu, haujawahi kuwa urithi wa Ukoo, sasa hapa ndipo ambapo Mamlaka za Uteuzi zinapoboronga

View attachment 3050462
Ishu sio kwamba tanzania kudhani, ni mfumo. Mtu akiwa madarakani anamtengenezea mwanae njia... wewe pia u.gefanya hivyo, hata mie wala nisiwe mnafiki. Namtengenezea njia aingie, akiboronga kivyake..
 
Natofautiana na wewe kwa hili. Siyo kweli kuwa watanzania tunadhani watoto wa viongozi nao wanaweza kuwa viongozi wa kesho. Sema viongozi wenyewe ndivyo wanavyofikiri hivyo na wanataka iwe hivyo. Na wanaweka wigo watu nje ya hapo hawaymtakiwi kusogelea kabisa.
Uko sahihi mkuu, Viongozi wao ndio wanadhani watu wengine hawana sifa ya kuongoza hii nchi.
 
Hapo ndipo tunapojikuta tunataabika na kuokota Magarasa na kuyapa uongozi.

Uongozi ni Karama kutoka kwa Mungu, haujawahi kuwa urithi wa Ukoo, sasa hapa ndipo ambapo Mamlaka za Uteuzi zinapoboronga

View attachment 3050462
Aisee ila kwa vile ni Wanyiramba wenzie hamna shida ila kiukweli huo si utaratibu mzuri mimi ningekua Mwigulu mwanangu angekua kwenye shule za kishua abroad huko halafu isitoshe Mwigulu tayari hakubaliki kwa Wabongo wengi sembuse mtoto wake?
 
sisi watanzania hatudhan kuwa watoto wa viongoz wanaweza kuwa viongoz bali viongozi ndio wanaowapa watoto wao nafasi za uongozi kama wewe sio mtoto wa kiongoz ni ngumu kupata nafasi ya uongozi maana wanapeana wao kwa waoa
 
Back
Top Bottom