Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Nilikuwa na hili tatizo kwa miaka mitatu bila suruhu. Mwanzoni sikuwa nalo nakumbuka nikiwa safarini dodoma nilinyoa ndevu saluni moja ndipo lilipoanza. Ilikuwa ni kero kwani ilifikia wakati vinakuwa na usaha ndani na kidevu kinakuwa na magamba. Ukitoka kunyoa inakuwa ni balaa kwani kidevu kizima kinakuwa chekunduu! Ukichukulia ni light skined kila mtu atakuona na kuanza kukuuliza maswali. Nilipaka dawa mbali mbali lakini wapi,! Kuna siku mwaka huu mwanzoni nilisoma ushauri ndani ya JF kuhusu tatizo hili ambao ulisema, nunua mashine yako ya kunyolea, acha ndevu zikue kiasi aafu uzinyoe kwa mashine yako na uwe unakanda kwa maji ya moto kwa siku kadhaa baada ya kunyoa. Nilifuata ushauri huo na nikaanza kupata ufumbuzi wa tatizo taratibu. Mpaka sasa kidevu changu kiko laini kabisa. Jf imenisaidia kuondokana na hili tatizo kwani ilifika hatua nilichukia kuwa na ndevu.
 
Maduka mengi ya vinyozi ni balaa tupu, ni maduka machache sana utaingia kunyoa utoke bila kuondoka na gonjwa hasa kwa wale wanaonyoa ndevu na kunyoa nywele zote (kipara).

Usikubali kunyolewa bila ya vyombo kusafishwa kwa spiriti au chemical yeyote yenye uwezo wa kuwaua bacteria kwenye machine.

Usikubali kunyolewa kwa machine inayowekwa kwenye machine wanayoita sterilizer ingizwe kichwani kwako bila kusafishwa sana kwa spiriti.
 
Viva Jf...

nafikiri hapa tatizo linakuwaga usafi wa vinyozi. Vinyozi wengi hawathamini kabisa usafi wa machine zao na vitambaa wanavyotumia. Ni wachafu kama nini! Asante mkuu kwa taarifa, jf ni kila kitu.
 
Wa JF ninataka ushauri wenu kuhusu ndevu,
Mimi nimebahatika kuwa na ndevu nyingi sana, yaani nisiponyoa baada ya wiki nzima nakuwa na madevu balaa,Tatizo kazi yangu haniruhusu kuwa na ndevu, kwa hiyo nyoa kila mara
Swali langu ni hivi, kila nikinyoa ndevu mapele yanaota sana, nimejitahidi kutumia after shave haisaidii kabisa,
Vile vile nimegundua baada ya kunyoa hata kabla ya kunyoa kidevu changu kinakuwa kikavu kabisa
Je kuna mafuta ya kupaka kwenye Ndevu? na kama yapo yanaitwaje?
Msaada tafadhali
 
tumia dawa inaitwa magic powder, ni unga flani ambao ukichangaya na maji inakuwa kama cream unapaka kisha baada ya dakika chache ndevu zinatoka zenyewe kwa kufuta na kitambaa. saloon nyingi mjini wana hiyo huduma, vipele utavisikia kwenye bomba
 
Wadau-nimekuwa na ndevu kwa muda mrefu-lakini hazikuwahi kuwasha wala kuwa ma vipele-ila nina mwezi wa nne sasa nimekuwa nikipata vipele na kabla sijanyoa ndevu huwa vinawasha kwa utamu sana-sometimes nakuna sometimes sivikuni-
ningependa kujua kama kuna meansa yoyote ninayoweza kuitumia ili niachane na hivi vipele
 
nyoa tumia bump stop. ni nzuri sana!1
 
Naombeni msaada madaktari, nina ndevu nyingi kiasi zilizosongamana sana kiasi kwamba siwezi kunyoa kwa mkasi(scisors) nikinyoa kwa wembe navimba sana kiasi cha kutoweza hata kugeuza shingo na hata kuongea.

Nikinyolea mashine navmba pia japo sio kama nyembe. Nimewahi kumwomba ushauri daktari akasema hakuna dawa ila hiyo tabia itaisha yenyewe hivyo niwe ninajaribu kunyoa kwa wembe kila baada ya mwaka nione kama nitavimba.

Nilijaribu last week na hali yangu sasa ni mbaya sana. Tafadhali naombeni msaada wa aina ya dawa ninayoweza kutumia.
10052013.jpg
 
mkuu nyoa mara kwa mara. yaani kwa kuwa una ndevu nyingi nyoa kila baada ya siku mbili. kila ukimaliza kunyoa kidevu kioshe kwa medicated soap unayo iamini kama dettol ya maji. subili kwanza upele uishe. ukishaisha ndo unyoe. upele ukiisha nyoa kwa magic. Muhimu sana ni kutunza usafi wa kidevu kila baada ya kunyoa. hakika upele utaisha na utapona kabisa. mia
 
Usisumbuke, tafuta sabuni ya ubuyu. Bei ya kiwandani ni sh. 1000 na ya mitaani ni kama sh. 2000
 
Pole sana. Usisumbuke, tafuta sabuni ya ubuyu. Pakaza kidevu kabla na baada ya kunyoa. Kiwandani ni sh. 1000 na mitaani ni kama sh. 2000.

tafadhali nijulishe matokeo baada kuijaribu.
 
Huu ugonjwa ni common kwa watu wengi na sikushauri kutumia MEGIC nadhani itazidisha tatizo. Nenda katika maduka yanayouza dawa za kiarabu uliza jiwe moja linaitwa SHABU (inategemea na duka lenyewe na ukubwa wa jiwe bei itarange baina ya 1,000 - 2,500). Hili utalitumia kila baada ya kunyoa na siku mbili (2) zinazofuata kila baada ya kuoga na utakuwa unalitia maji na unasugua sehemu za vipele.

Watu wengi imewasaidia hii na huwa kila unapozidi kulitimia idadi za upele inazidi kupungu. Mara nyingi ukienda vinyozi wa kihindi huwa hawakosi hili jiwe na watu wengi wanatumia hili jiwe badala ya "After Shave"
 
pole sana. mara nyingi vipele vya ndevu vinatokea baada ya kunyoa ndevu zote (kukwangua) hapo ndo ambapo mashine au wembe unagusana na ngozi. jitahidi kutokuondoa ndevu zote. jaribu kwenda kwenye maduka makubwa ya cosmetics ueleze tatizo lako watakusaidia. ushauri wa Tuko ni mzuri pia
 
Last edited by a moderator:
Tumia mafuta yanaitwa BUMP PATROL ni mazuri sana kwa wenye tatizo kama lako unapaka kila siku itakusaidia ni nzuri sana bei yake ni sh.7OOO HADI 1OOOO
 
Pole sana ndugu yangu. Hilo tatizo si la peke yako, Hata mimi nilipata taabu hiyo. Kwanza niligundua vipele vinatokana na nyuwele kutopata chance ya kutoka nje, Yaani inakulia ndani ya ngozi, halafu infection.

Sasa dawa amabayo nina uhakika, na imenisaidia inaitwa BUMP STOPPER, Kuna aina mbili, mmoja ni kali, BUMP STOPPERS-2 ukipata hiyo anza na hiyo.

kwanza wacha ndevu siote kwa siku kama nne au tano, yaani ngozi ipumzike, basi ukisha nyoa tu, apply hiyo cream, na utumia kila siku. siku za mwanzo kila unapo oga, uvimbe ukisha potea unaweza tumia kila asubuhi unapoteka bafuni.

Hii cream sio kwamba inatibu mmoja kwa mmoja bali inabidi utumie kila unapo shave.
Sasa tatizo kubwa ni sijui kama inapatikana Tanzania,
 
Naombeni msaada madaktari, nina ndevu nyingi kiasi zilizosongamana sana kiasi kwamba siwezi kunyoa kwa mkasi(scisors) nikinyoa kwa wembe navimba sana kiasi cha kutoweza hata kugeuza shingo na hata kuongea. Nikinyolea mashine navmba pia japo sio kama nyembe. Nimewahi kumwomba ushauri daktari akasema hakuna dawa ila hiyo tabia itaisha yenyewe hivyo niwe ninajaribu kunyoa kwa wembe kila baada ya mwaka nione kama nitavimba. Nilijaribu last week na hali yangu sasa ni mbaya sana. Tafadhali naombeni msaada wa aina ya dawa ninayoweza kutumia.

Pole sana ndugu yangu. Hilo tatizo si la peke yako, Hata mimi nilipata taabu hiyo.
Kwanza niligundua vipele vinatokana na nyuwele kutopata chance ya kutoka nje, Yaani inakulia ndani ya ngozi, halafu infection.
Sasa dawa amabayo nina uhakika, na imenisaidia inaitwa BUMP STOPPER, Kuna aina mbili, mmoja ni kali, BUMP STOPPERS-2 ukipata hiyo anza na hiyo,
kwanza wacha ndevu siote kwa siku kama nne au tano, yaani ngozi ipumzike, basi ukisha nyoa tu, apply hiyo cream, na utumia kila siku. siku za mwanzo kila unapo oga, uvimbe ukisha potea unaweza tumia kila asubuhi unapoteka bafuni.

Hii cream sio kwamba inatibu mmoja kwa mmoja bali inabidi utumie kila unapo shave.
Sasa tatizo kubwa ni sijui kama inapatikana Tanzania,
 
I am waiting pia kwa solution as hata mie vinanitesa flan!bt mie nilipata after kunyolea blue magic @figaniga tangu hapo vimekuwa vikinisumbua time to time!
 
Back
Top Bottom