Nilikuwa na hili tatizo kwa miaka mitatu bila suruhu. Mwanzoni sikuwa nalo nakumbuka nikiwa safarini dodoma nilinyoa ndevu saluni moja ndipo lilipoanza. Ilikuwa ni kero kwani ilifikia wakati vinakuwa na usaha ndani na kidevu kinakuwa na magamba. Ukitoka kunyoa inakuwa ni balaa kwani kidevu kizima kinakuwa chekunduu! Ukichukulia ni light skined kila mtu atakuona na kuanza kukuuliza maswali. Nilipaka dawa mbali mbali lakini wapi,! Kuna siku mwaka huu mwanzoni nilisoma ushauri ndani ya JF kuhusu tatizo hili ambao ulisema, nunua mashine yako ya kunyolea, acha ndevu zikue kiasi aafu uzinyoe kwa mashine yako na uwe unakanda kwa maji ya moto kwa siku kadhaa baada ya kunyoa. Nilifuata ushauri huo na nikaanza kupata ufumbuzi wa tatizo taratibu. Mpaka sasa kidevu changu kiko laini kabisa. Jf imenisaidia kuondokana na hili tatizo kwani ilifika hatua nilichukia kuwa na ndevu.