Tatizo la upokeaji wa maombi ya wanafunzi Elimu ya Juu

Tatizo la upokeaji wa maombi ya wanafunzi Elimu ya Juu

ingia google eRITA Portal (https://erita.rita.go.tz/birth) utafanya registration kwa kuingiza detail zake, mfumo utakuelekeza kila kitu, uta upload cheti chake cha kuzaliwa watakupa control no. then utailipia (3,500 tzs), utasikilizia kama siku moja au mbili itategemeana na wao, itakuwa approved, kisha utaidownload.
ukirudi kwenye mfumo wa heslb, birth verification number ni namba ya kumbukumbu iliyopo kwenye risiti baada ya malipo inayoishia na BV (123...BV) sawa na Appplication code kwenye eRITA portal.
Shukran sana kiongozi
Ngoja nikaanze na hili leo then nitaleta mrejesho.
 
kwenye birth certification verification number,
Ingia kwenye eRITA portal (ilituyotumia kufanya verification ya cheti cha kuzaliwa) utaona Application code hiyo ndo verification number ya cheti cha kuzaliwa kwa mwisho inaishia na BV (eg 2323....BV).
Details zingine jaza kawaida, hii sehemu ya cheti inakuwa detected na system, ukikosea haitakubali.
Nilipata shida hiyo
 
Mtandao aupo sawa mi Huwa naifanya sana Kuna baadhi unabahatisha zinakubali ishu sio verification code Kuna mdah verfication code inaleta jina la muombaji na kunamda ina load ata masaa kumi bila kufech matokeo yoyote ni wao wenyewe bodi system Yao inashida sana
 
Hello.... kipengere cha Education info niki-reverse application kwaajiri yakukiedit taarifa haziongezeki... Nikimjazia mwanafunzi aliyemaliza form 6 nakumbana na "form six result not found" na nikimjazia mtu wa diploma system inaandika "diploma result not found"..... mabadiliko hayatokei kabisa kwa category ya EDUCATION INFO
 
Kwa heshima na taadhima, ninaandika kama mdau wa elimu nchini. Tangu kufunguliwa kwa dirisha la maombi ya mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, waombaji wanashindwa kuwasilisha maombi yao kwa wakati. Wengi wanaishia hatua ya demographic information tu.

Wanapowasilisha (submit) hakuna mrejesho wowote. Waombaji wanafuata hatua zote kama vile kufungua account OLAMS, kulipia shilingi 30,000/= za kitanzania, kuchagua Local Undergraduate n.k. kuset picha ukubwa wa pasi ya kusafiria 120px kwa 150px isiyozidi ukubwa wa MB1.

Kuweka Verification code inayotolewa na RITA inayoishia na BV kama ilivyo, kuingiza namba ya NIDA bila kuweka alama ya deshi (-). Yote haya waombaji wanazingatia. Ila hakuna wanashindwa kuendelea.

Jambo hili linahitaji uharaka na kushughulikiwa na HESLB mapema iwezekanavyo. Haiwezekani nchi nzima wapate tatizo kama hilo muda wote.

Pengine Computers (SERVER COMPUTERS) zinazopokea na kuchakata taarifa za maombi ya mkopo zina uwezo mdogo ukilinganisha na mahitaji, au kuna hujuma inayofanywa dhidi ya Bodi ya Mikopo, au kuna matatizo ya kimitambo (technical challenges) au kuna uzembe wa kibinadamu pahala.

Wanombaji wengi wanategemea mikopo ili waweze kufikia ndoto zao kitaaluma hasa wanaotoka kwenye familia zenye kipato cha chini, na waombaji wengine ni yatima wa wazazi wote au mmoja.

Hivyo, ninasihi mamlaka husika akiwemo ndugu Abdul- Razaq- Badru (Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB) na timu yake kulifanyia kazi jambo hili. Pengine mfumo huu mpya una changamoto ambazo ziko nje ya uwezo wa kibinadamu.

Ushauri wangu ni kuwa, ili kujiridhisha kama mfumo uko sawa, wangetathmini kwa mwaka jana tarehe kama ya leo 15/08/2022 ni wanafunzi wangapi walikuwa wamekwishakuwasilisha maombi, na tarehe kama ya leo 15/08/2023 ni wanafunzi wangapi wamekwishakuwasilisha maombi. Hii, itawasaidia watendaji wa HESLB kugundua tofauti na kujiridhisha kuwa kuna jambo halipo sawa.

Ninaamini kuwa watendaji wa HESLB ni binadamu na sio malaika, wanaweza kukosea kiutendaji na hata vifaa kama Server Computers zao zimeundwa na biinadamu, zinaweza kuwa na dosari.

Ninaamini Higher Education Students' Loan Board (HESLB) will do all humanly possible means to address this issue of national importance as adequately as possible so much that those who deserve can acquire loans to further their education for a better Tanzania than ever before.

Regards,
Julius E Julius (0712830357)
Hata mimi nimehangaika sana kufanya application ila kwa sasa nimefikia hatua ya Guarantor Details napo pana shida nina wiki sasa sijafanikiwa unajaza kila kitu na ku upload kinachohitajika ila system ina load muda mrefu bila mafanikio hadi sasa na hakuna response kama umekosea au lah ila ukiruka inakwambia lakini ina load muda mrefu sana hadi in log out. nimewaandikia email hawajajibu hadi leo
 
Hello.... kipengere cha Education info niki-reverse application kwaajiri yakukiedit taarifa haziongezeki... Nikimjazia mwanafunzi aliyemaliza form 6 nakumbana na "form six result not found" na nikimjazia mtu wa diploma system inaandika "diploma result not found"..... mabadiliko hayatokei kabisa kwa category ya EDUCATION INFO
Umefanikiwa?
 
Hata mimi nimehangaika sana kufanya application ila kwa sasa nimefikia hatua ya Guarantor Details napo pana shida nina wiki sasa sijafanikiwa unajaza kila kitu na ku upload kinachohitajika ila system ina load muda mrefu bila mafanikio hadi sasa na hakuna response kama umekosea au lah ila ukiruka inakwambia lakini ina load muda mrefu sana hadi in log out. nimewaandikia email hawajajibu hadi leo
jaza details zako kwa usahihi mkuu, Umetumia kitambulisho gani cha Guarantor
 
Ela wanakula na shida ni server zao uchwaraa.wasengee ngoja niende makao makuu Yao tukaelewane hukohukoo
 
Ninashukuru sana mtoa mada JEJ kwa kilisemea hili. Nimekuwa ninahangaika kwa muda wa mwezi mmoja sasa kumjazia fomu mtoto wa kaka aliye jeshini kwa mujibu wa sheria. Nimekwama kwenye hatua ya demographic information kwa muda wa wiki 3 sasa. Ni vema sasa HESLB wakachukua hatua.
Kaka ulifanikiwa hapa
 
nimejarbu kumjazia maomb mdogo wang hapa nmekwama kwenye Demographic inf msaada wenu tafadhal wakuu
thanks
 
Log out ulogin tena hakikisha internet iko stable
Kwenda birth verification number usisahau kuweka BV mwishoni
nimeenda erita nimefanya maombi ya verif wamenipa no mf xxxxxxxBV_xxxx pia hvo hvo na death cert vp hz tarakimu nne c ndo zinafaa kukaa mwsho au n mimi nakosea
thanks
 
Asante mkuu

Ila issue, the system inaload kwenye demographic info..

Hili ni kwa wote?
 
Asante mkuu..

Issue dogo kazaliwa unguja na mamlaka ya huko wamekicertify..je still anatakiwa ajaze taarifa rita kupata birt verification number?
Nadhani lazima uwe na birth verification number ya Rita ndio ujaze pale au mnajazaga nn
 
Back
Top Bottom