Tatizo la vijana waliosomea mafuta na gesi kuzagaa mtaani wakati kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa na Serikali

Boss mtu anayesomea hizo fani hasomei kuuza petroli na dizeli kama unavyoeleza hapa.
Kuuza petroli na dizeli kila mmoja anaweza kufanya na wala haihitaji mtu awe na degree ya petroleum. Ni mtaji wako tu.
 
Wazazi hamtumii Akili course za maana zinajulikana sasa mnakuwa na over expectations Hadi mnaboa


Soma udaktari
Soma kilimo
Somo ualimu

If wewe Ni mtoto wa masikini
Sure kk.. uzur wa udaktar uez kusota muda mrefu, pia kilimo na ualimu kujiajili ni rahisi..

Kuna jamaa kagraduate ualim wa sayansi ana kituition centre chake mtaan apa ana madogo kama 200 iv na wanalipia 20k kwa mwezi piga hesab kwa mwez ana sh ngp...
 
Kitu kingine cha kuangalia ni hiki hapa
Kwenye fields za oil and gas,wanajali sana ''certification"
kitu ambacho hapa kwetu hakuna mamlaka inayofanya hiyo kazi hata kwa kushirikiana na taasisi
za nje,badala yake unakuta mtu anatoka msumbiji ,congo au Australia ni wa VETA lakini
yuko certified na mamlaka husika anakuwa boss wako wewe na degree yako
na anapiga pesa ndefu kichwani pako.

Tufike pahala,Taasisi kubwa kama UDSM zianze kufanya certification.
Hii itasaidia sio wenye degree tu bali hata watu wa veta waliothibitishwa kwenye fani fulani.
Mfano ni mafundi welder,ambaye hajathibitishwa hata kama huku
mtaani anafanya kazi nzuri ya welding,hawezi kuruhusiwa kuunga bomba la gesi.
Kwanini ,kwa sababu kampuni zote za bima zinaweka hicho kuwa kigezo cha mtu kufidiwa
au kutofidiwa endapo miundo mbinu yako itapata ajari ili ulipwe.
 
Achana na haya mawazo. Unatakiwa kuiambia serikali jambo la kufanya. Usijiangalie wewe kama wewe. Hapa tunatajadili kwa mstakabali wa taifa letu.
Wasomi ambao hamna ajira tumien elimu zenu kuwapa maarifa madogo wa kitaa mpige hela...
 
Boss mtu anayesomea hizo fani hasomei kuuza petroli na dizeli kama unavyoeleza hapa.
Kuuza petroli na dizeli kila mmoja anaweza kufanya na wala haihitaji mtu awe na degree ya petroleum. Ni mtaji wako tu.
Nimetoa tu Mfano kuwa kusomea kitu si lazima uajiriwe tu!
Unaweza kuji position kwenye angle tofauti tofauti si ajira tu!
Roman Abromavich aliwahi kuuza tairi (tyres) chakavu, midoli na mafuta ya kupima mitaani! Baadaye ndo akaja kununua Kampuni kubwa ya Mafuta Urusi ya Sibnef!
 
Hainihusu
 
Tunachozungumzia ni ukubwa wa miradi iliyopo kwenye sekta ya mafuta na gesi. Na idadi ya ajira zinazotoka. Ukiangalia sekta ya mafuta na gesi ndio sekta yenye miradi mikubwa kote duniani.
Hawana elimu sahihi. Walisoma kwa kukariri ili kujibu maswali ya mtihani. Wangekuwa na elimu sahihi dunia yetu imekuwa kijiji, wangeenda nchi nyingine wakaajiriwa. Chema chajiuza, kibaya chajitembeza.
 
Mkuu mimi ni mkongwe kwenye shughuli kwa miaka mingi katika mataifa mbali mbali hasa kwenye ukanda wa Bahari ya Pacific offshore.
Ningependa uni box kwa maelezo zaidi kidogo.
Ila hapa nitaweka mambo ya msingi kwa ajira za Mafuta na Gesi.
Shughuli za mafuta baharini ambako namimi nimekuwepo kwa muda mrefu sana.
Kunahitaji vitu vya msingi.
1.Shughuli hizi zina mwanzo,na mwanzo ni pale ukiwa chuoni au baada ya kumaliza chuo kufanya mafunzo au maelekezo ya kazi kwa vitendo nje ya chuo.Practical Training.
2.Lakini ili uende kule kuna Cardinal Rule of engagement nayo ni safety.
Mazingira ya bahari yana changamoto nyingi.
Kwa hiyo utaigia kujifunza kozi fupi kwenye vyuo vinavyotambuliwa kimataifa, kufanya kozi fupi za safety, yaani HUET yaani Helicopter under water Escape,First Aid,Fire Fighting,
Security na mambo mengi.
3.Lazima ufanya Medical Examination, usipofaulu medical exam hutaweza kwenda huko.
4.Drung and Alcohol Test.Lazima upimwe mara kwa mara tena kwa kushutikia.Hivyo vitu havikubaliki kabisa.Na jihadhali usiwekwe kwenye black list.
5.Kuna swali mmoja kubwa kama unaweza kufanya na watu wa mataifa mengine bila kubagua.

Kazi hizo ni hatari zinahitaji umakini utakuta kule kazi labda ya kuchukuwa nusu saa kule offshore itatumia mwingi kutayarisha kuifanya kazi hiyo kwa kupitia vifungu vyote vya kuipa au kuinyima uhalali.
Yapo mengi.Ila offshore inakupa nafasi ya kufanya na muajiri wako popote duniani si Tanzania tu.
 
Vijana wewe na extra soft skills za kuwasaidia endapo changamoto za ajira zinapotokea.ni fikra potofu kusoma ili kuajiriwa ni lazima vijana watafute njia mbadala endapo wakikosa ajira mfano ujasiliamali, uandishi sanaa kilimo nk
Hizi akili ni za kiduwanzi sana yaani serikali iingie gharama kubwa kumsomesha mhandisi wa gesi na mafuta mpaka chuo ,then a graduate na kufanya kazi za ukulima ,una akili wewe ? , Nini maana ya kupoteza pesa zote hizo za walipa kodi ?
 
Boss nimeandika uzi huu kuwasemea vijana wa mafuta na gesi ili serikali ifanye jambo. Yaani serikali yetu ndio yenye maamuzi linapokuja swala la ajira. Na hii ni mass employment boss. Ni tatizo kubwa hili tunapokua na miradi yetu mingi tu ndani lakini vijana hawapewi nafasi. Nafasi za kazi za mafuta na gesi zipo nyingi sana bongo. Ila zimekamatwa na wageni. Tatizo hilo linahitaji mkono wakisela. Yaani tunawaona wazungu na wahindi wana ajiriwa kwenye sekta ya mafuta na gesi Tanzania basi hizi nafasi zipo nyingi hapa nchini na wala haitaji vijana wetu waondoke nchini.
 
Mkuu bila kumungunya maneno kuna sintofahamu kubwa.
Mimi nimefanya South East Asia yaani Thailand,Malaysia,Vietnam,India,Mymar,Indonesia, Papua New Guinea, kama Chief Engineer kwenye offshore construction vessels,sub sea marine Engineering, commissioning projects,demolishing of oil rigs na uchafu mwingi mno.Hakuna kubebwa.Ila kitu muhimu ni kuwatayarisha vijana hawa ili wapate viwango vya kimataifa.
 
Basi wakaajiriwe kt vituo vya mafuta yaani wahache nyodo hawa madogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…