Tatizo la vijana waliosomea mafuta na gesi kuzagaa mtaani wakati kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa na Serikali

Tatizo la vijana waliosomea mafuta na gesi kuzagaa mtaani wakati kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa na Serikali

Boss hii ni mada technical tusiwaseme watu au vyama vya watu. Bali tuchangie mambo technical. Tulinganishe miradi iliyopo na idadi ya ajira na idadi ya hao vijana. Angalia hata capital investment ya hiyo Miradi.
Na actually si wahandisi wa mafuta na gesi tu wanaosugua kitaa uhandisi in general ni majanga tu sasa hivi ni kama ualimu ulivyo tu , ajira hamna watu wachache ndio wanajishikiza Kwa kanjibai kuganga njaa hata kozi za afya napo hali si nzuri ,asikudanganye mtu kuna madaktari , manesi , maabara nk wanasugua kitaa vile vile
 
Labda serikali iwalazimishe wenye vituo vya mafuta kuajiri hao wasomi bila hivyo wakauze mitumba popote walipo, kama shuleni kuna upungufu wa walimu na walimu wanamiaka 4 mtaani je hao wa gesi na mafuta itakuwaje?
 
Nimeona hili leo niliseme pengine viongozi wetu hawalifahamu swala hili:

Kweli kumekua na tatizo la vijana wetu waliosomea fani za mafuta na gesi kuzagaa mtaani tangu fani hizi zilipo anzishwa mwaka 2013. Asilimia 80 ya vijana waliosomea fani hizo hawaja ajiriwa mpaka sasa. Na walianza kuhitimu mwaka 2016.
Najua wewe ni mmoja wa Wadau wanaoifuatilia sana hii sekta...

And am certain unafahamu baada ya JPM kuingia madarakani, kila kitu ni kama kilisimama kwa upande huo...

Sasa unashangaa nini kuona wengi wao wapo mtaani wakati kazi hasa zinazowahusu wao hazijaanza?!

Kama Petroleum Companies waliweza kufanya exploration kabla madogo hawajapelekwa nje kusoma hizo bachelosr, it means, as of now wakati development bado haijaanza rasmi, basi hata demand ya hao graduates wetu bado ni ndogo!

I know you know kwamba baada ya wao kumaliza zile bachelor, wasingeanza kwa kuwa decision-makers!! Sasa how come unashangaa?!

Hivi karibuni nilipita kuchungulia pale Likong'o wanapotarajia kujenga LNG Processing Plant, na kazi ambayo ilitarajiwa kuanza kufanyika back in 2016 ndo inaanza sasa huku wakati ule tukiambiwa "Gesi yote ameuziwa Mchina" na watu wakawa wanaamini tu!!

I feel sorry for them...

Wawe na subira

Hapa ndipo naona nilimshauri vizuri sana my nephew ambae back in 2018 alitaka akasome Bachelor ya Industrial Engineering!

Nilipomuuliza kwanini anataka akasema Industrial Engineering, kiwepesi tu akasema "Uncle, si unajua hii ni Serikali ya Viwanda"!

Nikamuuliza kama kuna watu walisoma kilimo kwa kuona Serikali ya JK ilikuwa Kilimo Kwanza, je hivi sasa watarudi tena wakasome Industrial Engineering kama wewe au wasubirie rais mwingine wa Kilimo Kwanza?!

Haya ni Madhara ya Serikali ya Kila Rais na Lwake!!

Anyway, wenye uwezo warudi vyuoni wakasome graduate programs za Oil, Gas, and Petroleum Management. Wasio na uwezo, wa-fight kupata scholarship! Kama vp, wajaribu kutafuta connection and recommendation kupitia LinkedIn kwa ajili ya fursa Middle East!
 
Wazazi hamtumii Akili course za maana zinajulikana sasa mnakuwa na over expectations Hadi mnaboa


Soma udaktari
Soma kilimo
Somo ualimu

If wewe Ni mtoto wa masikini
Mnaongea msivyo vijua hao wa kilimo ,afya na ualimu wanasugua Gaga kitaa kama Kawa siku hizi na ni wengi huwezi amini , kama unabisha fanya utafiti uone
Mimi ni mhandisi na what I can tell you , labour market ya Tz ni utopolo kwa sasa , watu watoke wakapambane nchi za nje hapa Tz ni michosho tu kwa wasomi
 
Chief Eng. pale anakunja 300k basic/month qmmmq
Halafu wale wahuni wa ERB wapo tu ,kazi kuvimbisha matumbo yao kwa pesa za fees za wahandisi , hamna majitu ya ovyo kama haya majamaa ya bosi ya wahandisi ,yaani ni takataka ,mimi huwa yana kutumia mimeseji mpaka nilishachoka .
Ukiangalia cha maana wanachofanya pale ni zero . Yaani hii nchi hii
Hii fani ya engineering hapa Tz halipewi heshima inayostahili .

Screenshot_20221101-012203.jpg
Screenshot_20221101-012156.jpg
 
Boss hii ni mada technical tusiwaseme watu au vyama vya watu. Bali tuchangie mambo technical. Tulinganishe miradi iliyopo na idadi ya ajira na idadi ya hao vijana. Angalia hata capital investment ya hiyo Miradi.
Unasema tusiwaseme watu na vyama vya watu [emoji849][emoji849][emoji849]
Hii mada ungeipeleka kwenye jukwaa la ajira
Sasa umeileta kwenye jukwaa la siasa
Subiri ujibiwe kisiasa

Makampuni mengi ya oil & gas, basic salary zao inanzia $3500-$5000 kulingana na ngazi ya elimu wanayoitaka wao Kama kigezo cha waombaji

NB. {Kama umepitia kwenye system kutoka kwenye chama hata kama elimu yako ilikaribiana na elimu wanayoitaka hayo makampuni bado utapitishwa}

Sasa wewe mtoto mkulima kule kwetu kibwegiza uje uchukue nafasi hiyo wakati watawala wanajua wapi watoto wao waingie na wale mema na kuishi vizuri

Sisi wote wa kibwegiza tukajaze nafasi hizi ili maisha ya songe
_polisi
_Ualimu

Pole sana rafiki yangu ....kwa kuondolewa BOT kisa haujapelekwa na chama na hautambuliki na chama cha walamba asali
 
Thinking yako ni ya Industrial Revolution Age! Tuko kwenye Information Age!
Mnaosoma ili mkaajiriwe kwenye miradi ya Serikali mmepitwa na wakati!
Kuna wenzenu darasa la saba wamejiongeza wanauza petrol na diesel vijijini kwenye shughuli za kilimo na migodi!
Ukipita njia inayotoka Kahama hadi Masumbwe kuna madumu yamening'inizwa maporini kuashiria biashara ya "kupiga nyoka" katika magari yaendayo Rwanda na Burundi inafanyika!
Jitu lina degree ya petroleum na gas linapiga miayo mtaani hata mia halina!
Elimu ya kijinga ya kukariri theories ( tena mengi yanatamka seori)!
Kama akili zenyewe za watanzania ndio hizi kama zako ni bora muendelee kujengewa vyoo tu kwa misaada wa USAID na mminywe tozo tu na mbogamboga hamna namna ,
 
Mtoto wa masikini Anabidi kusoma fani tatu tu
Udaktari
Ualimu
Kilimo

Kila siku nawaambia lakini mnashupaza shingo
Pia Ufundi wa aina mbali mbali katika vyuo vya VETA.

Ni rahisi kujiajiri huku ukisibiri fulsa za ajira
 
Kitu kingine cha kuangalia ni hiki hapa
Kwenye fields za oil and gas,wanajali sana ''certification"
kitu ambacho hapa kwetu hakuna mamlaka inayofanya hiyo kazi hata kwa kushirikiana na taasisi
za nje,badala yake unakuta mtu anatoka msumbiji ,congo au Australia ni wa VETA lakini
yuko certified na mamlaka husika anakuwa boss wako wewe na degree yako
na anapiga pesa ndefu kichwani pako.

Tufike pahala,Taasisi kubwa kama UDSM zianze kufanya certification.
Hii itasaidia sio wenye degree tu bali hata watu wa veta waliothibitishwa kwenye fani fulani.
Mfano ni mafundi welder,ambaye hajathibitishwa hata kama huku
mtaani anafanya kazi nzuri ya welding,hawezi kuruhusiwa kuunga bomba la gesi.
Kwanini ,kwa sababu kampuni zote za bima zinaweka hicho kuwa kigezo cha mtu kufidiwa
au kutofidiwa endapo miundo mbinu yako itapata ajari ili ulipwe.
Yah ! We umeongea issue ya Maana ingawa Kwa issue ya certification inafanywa na bodi ya engineers ERB , Ila ni pale unspomaliza masomo ya chuo then unatakiwa kufanya STEM program ambayo hii unakuwa umeajiriwa au kama trainee WA internship ambapo unaandika technical reports Chini ya usimamizi wa Professional Engineer kama supervisor wako na kuzituma kule ERB kwa miaka mitatu ,then baadaye ndio kuna mchakato mingine inafuata then unakuwa certified ,kitu ambacho ni unfeasible Kwa ambao hawajapata sehemu ya kufanya hizo internships au kazi .
 
Magufuli alipambana haya mafisadi yaache kugawa keki ya taifa kwa familia zao mkawa mnamtukana. Haya sasa.
 
Mtoto wa masikini Anabidi kusoma fani tatu tu
Udaktari
Ualimu
Kilimo

Kila siku nawaambia lakini mnashupaza shingo
Ongezezea civil +eletronic engineering hauwezi kukosa Hela ya kuendesha maisha
 
Achana na haya mawazo. Unatakiwa kuiambia serikali jambo la kufanya. Usijiangalie wewe kama wewe. Hapa tunatajadili kwa mstakabali wa taifa letu.
Unamjua muasisi wa msemo wa Mkono mtupu haulambwi?

Unaweza ukanipatia walau jina lake alikua anaitwa nani?
 
Yah ! We umeongea issue ya Maana ingawa Kwa issue ya certification inafanywa na bodi ya engineers ERB , Ila ni pale unspomaliza masomo ya chuo then unatakiwa kufanya STEM program ambayo hii unakuwa umeajiriwa au kama trainee WA internship ambapo unaandika technical reports Chini ya usimamizi wa Professional Engineer kama supervisor wako na kuzituma kule ERB kwa miaka mitatu ,then baadaye ndio kuna mchakato mingine inafuata then unakuwa certified ,kitu ambacho ni unfeasible Kwa ambao hawajapata sehemu ya kufanya hizo internships au kazi .
Asante kwa ufafanuzi,ila mimi sina uhakika na hilo,siweziongelea nyanja nyingine ila kwa upande wa oil and gas
sijaonana na mtu yeyote wa hapa Tanzania aliyesaidiwa na ERB kuwa certified kwa viwango vya kimataifa(huenda ni mimi tu sina taarifa ),Kingine ni hawa watu wa VETA nawafahamu baadhi waliosaidiwa na waajiri wao kwa kutuma kazi zao uingereza zinafanyiwa uchunguzi wanasajiriwa na kuruhusiwa kufanya kazi hizo.Kwa ERB sijawahi kuwasikia wakijihusisha na watu wa VETA kama pia wanajihusisha ni vema wakaliweka wazi,maana nchi za wenzetu upande wa engineering VETA ina nafasi kubwa pia.
 
Hapo labda kilimo tu, labda na course za kujiendeleza kama computer programming na software development.
Hii kilimo hii, inalipa sana ila uangalifu muhimu mno, usije ukaingia mazao serikali inatolea macho, lazima ukate mtaji!
 
Tuchangie mada inavyotaka jamani. Mada inazungumzia ukubwa wa miradi yenyewe. Swali la kujiuliza kwenye hiyo miradi wakina nani wanakaa. Ndio mada ilenge hapo.
Miradi ilisimama Magufuli alikataa kuna mambo haya kuwa sawa kwenye mikataba ya utafutaji na uchimbaji wa gas naafuta kwaiyo kampuni nyingi ziliondoka, kwa saa zimeshaanja kurudi tena uko Mtwara, Magufuli aliwaambia Makubaliano yao na awamu ya 4 yeye hatambui, alikataa hizo kampuni kama alivyo kataa ujenzi wa Bandari ya Bagomoyo.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kuna dogo jirani yangu anasomea petroleum engineering field chuo kiliwapeleka karakana ya tazara wakawa wanafanyishwa kazi za kuosha train
 
Kama akili zenyewe za watanzania ndio hizi kama zako ni bora muendelee kujengewa vyoo tu kwa misaada wa USAID na mminywe tozo tu na mbogamboga hamna namna ,
Wewe ndo akili yako ndogo kwani umeshindwa kuelewa theme ya submission yangu!
Nimetoa Mfano wa darasa la saba wanavyojiongeza kukabiliana na changamoto ya ajira! Wasomi mnalilia ajira za Serikali .
Dunia ya leo yeyote anaweza ku-create ajira siyo lazima Serikali!
Tatizo lenu mmekuwa mentored kuwa job seekers badala ya job creaters! Poor you!
 
Kama akili zenyewe za watanzania ndio hizi kama zako ni bora muendelee kujengewa vyoo tu kwa misaada wa USAID na mminywe tozo tu na mbogamboga hamna namna ,
Wewe ndo akili yako ndogo kwani umeshindwa kuelewa theme ya submission yangu!
Nimetoa Mfano wa darasa la saba wanavyojiongeza kukabiliana na changamoto ya ajira! Wasomi mnalilia ajira za Serikali .
Dunia ya leo yeyote anaweza ku-create ajira siyo lazima Serikali!
Tatizo lenu mmekuwa mentored kuwa job seekers badala ya job creaters! Poor you
 
Mkuu huyo kijana ni bright na skilled?.mbona kazi za gas&oil zimejaa dunia nzima mwambie aombe nje ya tz..inashangaza sana vijana potentials kukomaa na kuajiriwa na Gov ambapo malipo ni kidogo wakati nchi nyingine fursa ni nyingi sana kwa skilled people.
Huyo hata aende Somalia tu hapo hatoboi,elimu yetu ya kumeza madesa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom