Nimeusoma na waraka pia. Nakiri ni kweli katika awamu hii kumekuwa na bias kubwa ya kijinsia, kikanda na hata kidini hasa katika teuzi za kazi za uongozi wa serikalini, na ninapenda niseme labda ni bias (probably unintended) kwa sababu wakati yote hayo yanaonekana sijapata kuona wala kusikia waathiriwa wakilalamika na badala yake nawaona wakiwa mstari wa mbele kumwaga sifa tuuu! Awamu zilizopita pia nilisikia malalamiko lakini nashangaa sana kwani awamu zilizopita hali hii ya 'bias' haikuwa mbaya hivi lakini malalamiko yalikuwa makubwa disproportionately.
Lakini niseme pia katika ule waraka kuna malalamiko mengine nadhani watu walishauriwa tu vibaya. Mfano ile kesi ya UDOM iliyozungumzwa, kwanini watu walalamikie kuondolewa watu wa qualifications ndogo na kuwekwa wa better qualifications (nimeona majina yaliyochukua nafasi ni professors na doctors, na waliotolewa ni chini ya hapo), hayo mbona ni maboresho ya kawaida? Ningesikitika kama system inafanya purging ya watu kwa udini na kuingiza watu wa inferior qualifications alimradi tu ni wa dini wanayotaka! Hilo la UDOM nitawaomba ndugu zagu waislam walitafakari tofauti.
Huko kwenye mambo ya teuzi na kwingineko, wacheni mambo ya kusifia tu badala yake leteni data (kuna sheria ya takwimu siku hizi, kuweni waangalifu), wekeni data mbele ya wanaohusika (siyo hapa mtandaoni, hapa njooni kuleta taarifa ya jitihada na matokeo), semeni waziwazi mbele ya anayetakiwa kuchukua hatua mnazotaka, msimwogope, mwenyewe anawaambia siku zote msema kweli ni mpenzi wa Mungu.