Sheria ya takwimu ina kipengele kimoja kimekaa kimtego sana.
Kwamba takwimu unazozitoa kwa umma uwe umezipata kwa chanzo kinachoaminika chenye uhalali wa kutoa takwimu hizo kwa mujibu wa sheria.
Sasa kusema uwiano wa uteuzi ni 80% kwa 20% kwa dini zilizopo.....hii ina utata.
Kwanza Tanzania hakuna dini mbili pekee.
Niishie hapo.
Maendeleo hayana vyama!
*KUSHIKILIWA KWA SHEIKH PONDA ISSA PONDA KUHUSIANA NA WARAKA WA SHURA YA MAIMAMU*
Nimeusoma Waraka ulioandikwa na Taasisi ya Shura ya Maimamu inayoongozwa na Sheikh Ponda Issa Ponda. Kilichonisukuma kuutafuta na kuusoma Waraka huo ni kufuatia taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kukamatwa kwa Sheikh Ponda ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na Waraka huo. Ninakiri kuusoma Waraka huo kupitia Jamii Forums ambao ndio wamechapisha pia picha ya Ponda iliyopo hapa chini.
Waraka huo una mambo mengi na yenye kufikirisha akili. Kuna mahali kuna takwimu zinazoonyesha utafiti kwa upande wa waandishi ili kuthibitisha kile walichokiandika. Kuna malalamiko, kuna ushauri, na tahadhari. Kwa ujumla, Waraka ule unaweza kuchukuliwa kuwa ni maoni ya wahusika kwa Serikali na jamii ya Watanzania.
Tunashauri kuwa hekima kubwa inahitajika katika kushughulikia jambo hilo. Wahusika (Mamlaka) wanao uhuru wa kutolea ufafanuzi mambo kadhaa yaliyojitokeza ndani ya Waraka. Waraka umekuja kama hoja na hivyo ipo haja ya hoja kutumika katika kujibu au kupangua hoja! Sio kila hoja inaweza kuwa na ukweli wote, lakini si kila hoja inaweza kuwa na uwongo wote.
Mamlaka zinatakiwa kushughulikia suala hili kwa weredi, umakini na utulivu. Ni vizuri kujikita katika kuangalia ukweli, uwongo au uhalisia uliomo ndani ya Waraka. Mamlaka zinaweza kuepuka mtego wa kuangalia 'personalities' zilizo nyuma ya Waraka bali zijihusishe zaidi na hoja zilizomo. Kama hoja zilizomo ni za Ponda kama Ponda, basi zitakufa zenyewe. Lakini kama hoja zilizomo zinaishi na zinawakilisha sehemu kubwa ya watu, basi hoja hizo zitaishi hata Ponda asipokuwepo. Malalamiko hujibiwa na kushughulikiwa. Ushauri hupokelewa na kufanyiwa kazi au kukataliwa. Tuhuma huchunguzwa na kutolewa taarifa. Tunadhani hayo yote yanaweza kufanywa na Mamlaka.
Mwito wetu kwa Waislamu wote ambao wanatajwa kuwa wamewakilishwa kupitia Waraka huo ni kuwaomba kuwa watulivu wakati wadau wengine wanalitafakari na kulishughulikia suala hilo.
Ninaomba hekima, utulivu, uvumilivu, na upendo katika hili kwa wote wanaohusika.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
*Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula -* Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani