Tazama picha ya gari lililotengenezwa na wanafunzi wa UDSM

Tazama picha ya gari lililotengenezwa na wanafunzi wa UDSM

Vyombo vya moto ni neno generalize ambalo ndani yake lina matawi yake

Hicho chombo nacho ni tawi miongoni mwa vyombo vya moto, ukiite Vyovyote bado kinabaki kuwa gari "outomobile/vehicle"
 
daah. kaka punguza madharau 😂😂
Nimempa maua yake mwamba.

Zamani ukimcheka mtu ana gari baya unaulizwa "Baba ako analo?".

Sasa hapo ukimcheka anaweza kukuuliza, wewe lako ulilotengeneza liko wapi? 🙂 🙂
 
Hicho chombo nacho ni tawi miongoni mwa vyombo vya moto, ukiite Vyovyote bado kinabaki kuwa gari "outomobile/vehicle"
Hakiwezi kuwa gari kwasababu magari tunayajua.

We kama ni injinia wa hicho kidude sisi tutakupa sifa kwa kutubunia kitu kipya ambacho mwanzoni hatukuwahi kukiona.

Ebu fikiria mwenyewe kampuni ya Toyota ikisikia kuna machuma yameungwa ungwa yakaweka na siti afu watu wakasema gari, watajiskiaje?

Watu wanatumia akili kubwa kutengeneza magari afu we unakuja na kidude chako unasema gari, kweli?
 
Unajua hata ule ungo anaosafiria bibi yako usiku ni gari ??🤣🤣
 
Kwa sasa watu hawaanzii nyuma, wanaanzia wenzao walipofika kwenda mbele. Hilo gari linafanana na 1930s na baada ya hapo ni store. Yule jamaa ambaye hakuwa kasoma miaka kadhaa zi alitengeneza gari likaonyeshwa analipiga misele hadi likawa maonyesho ya sabasaba.
Ni dunia ya mashindano lazima ulete vitu vyenye ushindani.

Kuanzia pale walipofikia wenzetu ni sawa na kumchukua mtoto asiyejua kusoma na kuandika halafu umuingize darasa la 7 kufanya mtihani na wenzake waliopitia madarasa yote, ni vyema katika hali hiyo naye afanyiwe "crash programs" kwanza ndipo aingizwe darasani kufanya mtihani na wenzake, hicho walichofanya hao wanafunzi ni kama crash program.

Itakuwa ni ajabu mtu kupiga danadana hujui halafu uingizwe uwanjani kucheza mechi !!🤤
 
Unajua hata ule ungo anaosafiria bibi yako usiku ni gari ??🤣🤣
Ndio maana nimesema kwa tafsiri yako wewe kila kitu ni gari

Hata mtu anayeendesha kwa kuharisha utasema nayo hiyo ni driving fani na hicho kinachoeneshwa ni gari
 
anastahili kupongezwa. sema shida unaunda bodi ila injini sasa, unakuwa umeungaunga tu mashine za watu ambazo huwezi kutengenezea kitu chako hadi kwa ruhusa yao (patent rights). tungepata mtu anayeweza kutengenenza injini za vitu vya moto kama magari, bodi mbona ni rahisi tu. hata halihitaji ufike chuo kikuu. kwani wale wanaotengeneza mabodi ya mabasi ya mikoani wamefika university? ila injini sasa utakuta wanaweka ya scania etc.
 
Ndio maana nimesema kwa tafsiri yako wewe kila kitu ni gari

Hata mtu anayeendesha kwa kuharisha utasema nayo hiyo ni driving fani na hicho kinachoeneshwa ni gari

Hapa hatuzungumzii "kuendesha" tunazungumzia "gari", drone yenyewe inaitwa UAV, hiyo "V" hapo stands for Vehicle.
 
Samaleko!

Hii ni picha ya gari lililotegenezwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDSM. Vipi maoni yako kuhusu huu ubunifu tutawafikia Wachina, Wajapani na German huko mbeleni au tuendelee na huu ubunifu uliojaa utundu.

wameunganisha bodi tu. Kuna kampuni tayari tanzania za kuunganisha body zipo Arusha na kampuni za mabasi. Yaani hata kuunganisha body wameshidwa. Hakuna hata kimoja wametengeza
 
Hongereni litumike katika katika mahoteli, mtu hataki kutembea vinamtembeza hadi nje ya receiption au hadi nje ya chumbani kwake
 
Hapa hatuzungumzii "kuendesha" tunazungumzia "gari", drone yenyewe inaitwa UAV, hiyo "V" hapo stands for Vehicle.
Tayari ushataja drone hiyo ni kitu kingine sio gari
 
Lete ushahidi wewe!!, we unadhani unaweza kushindana na mimi katika kiswahili??.
Hao wote walioandika "Mtelemko" ni wajinga??, wewe tu ndio mjuaji bila kuleta ushahidi!!.

Lugha ni matumizi ya maneno yaliyokubalika na sio matumizi ya maneno kulingana na matakwa na raha au urahisi wako binafsi katika matamshi, wewe unaona raha na umezoea kutamka "re" badala ya "le" na unataka kulazimisha iwe hivyo.
Sishindani na wewe ila kasome kamusi ya kiswahili kama kuna neno mtelemko wewe kama huwez tamka r pole
 
Samaleko!

Hii ni picha ya gari lililotegenezwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDSM. Vipi maoni yako kuhusu huu ubunifu tutawafikia Wachina, Wajapani na German huko mbeleni au tuendelee na huu ubunifu uliojaa utundu.

Mwanzo mzuri sana tena sana....kikubwa kuna combination zinatakiwa kufanikisha ubora zaidi ikihusisha watu hawa
*Machenical
*IT
*Electronics na
*Automation
*Macheincal body building engineers

Kupata jambonkubwa zaidi
 
Ni mwanzo mzuri. Hata hao wengine walipoanza hazikuwa za kupendeza
Mwanzo mzuri gani bana, mwanzo wa kindezi. Wakati Kenya wanarusha Satelite sisi tunatengeneza toy car ya maonyesho halafu tunajisifu?! Kwanza hiyo ni ya dizel au petrol?! https://jamii.app/JFUserGuide Politics!
 
wameunganisha bodi tu. Kuna kampuni tayari tanzania za kuunganisha body zipo Arusha na kampuni za mabasi. Yaani hata kuunganisha body wameshidwa. Hakuna hata kimoja wametengeza
Watu walikua wanachukua chase za scania wanatengeneza mabasi sasa hivi hawafanyi sana sababu kuna makampuni ya china yanatengeneza bodi kama yutong, zhongtong n.k

Watu walikua wanachukua chase za fuso wanatengenezea mabasi kwa hiyo walichofanya hao wanafunzi ni ujinga wangetakiwa waje na kitu bora zaid hicho
 
Back
Top Bottom