Tazama picha ya gari lililotengenezwa na wanafunzi wa UDSM

Tazama picha ya gari lililotengenezwa na wanafunzi wa UDSM

Nadhani kama nchi tungewekeza zaidi kwenye vijana wa IT, kilimo na ufugaji. Haya mambo ya kutengeneza magari tumeshachelewa sana. Hilo gari hata kama linaweza tembea HALINUNULIKI. Hapo naona faida itakayopatikana ni kijana kujulikana na kupata ajira kwenye viwanda vinavyohusika na alichosomea lakini pia itategemea na GPA yake. Ifike sehemu tujiambie tu ukweli
Hatujachelewa iwapo plan, nia na uongozi bora upo. Hatutakiwi kuunda tena hii design ya 1920. Tuibe technolojia kwa kupeleka wanafunzi nje, wasome na kufanya kazi kwenye viwanda vya magari. Wakirudi huku wanachanganya mawazo kwa pamoja na kutoka na kitu. Mbona China anaiba?
 
Linazidiwa na lile la taliban. Hakuna jipya hapo wala ugunduzi. Kama kawaida baada ya maonyesho tunaweka store mpaka maonyesho mengine twaja na new.
Zile hilikopta kule Arusha na Mbeya nafikiri sasa ni makazi ya panya na mende.
 
Mzee Kapalata wa sido vingunguti kaanza kutengeneza gari kama hili miaka kumi iliyopita.

Saba saba lilikuwa kinakuwepo kwenye maonesho na sido lipo.

Huyo mzee kapalata hata elimu ya shule ya msingi hajawai kusoma. Ila ametengeneza gari kama hilo kitambo sana.

Udsm wanafanya leo huku watu ambao hawajaenda shule wamefanya miaka 10 iliyopita.

Na inawezekana gari la mzee kapalata kawauzia hao wanafunzi wa udsm ili nao wauze sura
Kwani mtu inahitaji kukaa shule kujifunza kupika? Au kufua ? Kuna kitu tunaita ujuzi unakaa unaangalia unapata ujuzi kwa kurudia rudia kufanya unapata uzoefu.
 
Hakuna neno mtelemko kwenye kiswahili ni mteremko acha ubishi wa kitoto


Lete ushahidi wewe!!, we unadhani unaweza kushindana na mimi katika kiswahili??.
Hao wote walioandika "Mtelemko" ni wajinga??, wewe tu ndio mjuaji bila kuleta ushahidi!!.

Lugha ni matumizi ya maneno yaliyokubalika na sio matumizi ya maneno kulingana na matakwa na raha au urahisi wako binafsi katika matamshi, wewe unaona raha na umezoea kutamka "re" badala ya "le" na unataka kulazimisha iwe hivyo.
 
Kichwa cha habari kimesema gari

Ukiangalia picha inaonesha Guta

Ebu tuacheni kwanza
 
Swali muhimu kabisa ni: je wameweza kuunda engine yake from the scratch ??

Nauliza swali hilo kwani gari hasa ni Engine, ukiweza kuunda Engine basi vyote vilivyobakia ni mtelemko tu, kuunda Engine ndio elimu ya ma-engineers.
Mbona watu mnajadili gari kwa kutumia rejea ya picha ya guta?

Hapa ndio mnanichanganya
 
Nadhani kama nchi tungewekeza zaidi kwenye vijana wa IT, kilimo na ufugaji. Haya mambo ya kutengeneza magari tumeshachelewa sana. Hilo gari hata kama linaweza tembea HALINUNULIKI. Hapo naona faida itakayopatikana ni kijana kujulikana na kupata ajira kwenye viwanda vinavyohusika na alichosomea lakini pia itategemea na GPA yake. Ifike sehemu tujiambie tu ukweli
Labda kinakuwa, pengine miaka inavyozidi kwenda kitakuwa fuso
 
Hilo gari likigongana na baiskeli iliyobeba mkaa huwezi toboa. Kazi nzuri, vipaji kama hivi inabidi viendelezwe. Nimeona nchi kama Ghana wamejitahidi sana katika hili.
Hilo gari mnaliona nyinyi tu jamani mbona mi silioni?
 
Mbona watu mnajadili gari kwa kutumia rejea ya picha ya guta?

Hapa ndio mnanichanganya


Guta nalo ni gari lenye miguu mitatu jinsi ilivyokuwa pikipiki ni gari yenye miguu miwili.
 
Back
Top Bottom