Tazama ushahidi huu wa kimahesabu wa Michango ya Lissu Unaothibitisha CHADEMA haifikishi wanachama hata million Moja

Unasemaje? Huoni mpaka sasa yamechangiwa mamillioni kwa mamillioni? Hujaona pesa zinachangwa hadi millioni mia moja kwa mkupuo? Unafahamu walimu peke yao walichangia kiasi gani?
Leta evidence million 100 zimechngwa wapi zimehifadhiwa kwenye account gani tuweze kukuamini?? Kama sio propaganda kama wenzio walio salimia na kufeli
 
Kwa hiyo kuna wanachadema ambao mpaka sasa hivi hawafahamu kama kuna mchango unaoendelea kwa ajili ya kumchangia Lissu kununua gari mpyaaaa? Hao wanaofahamu kama Lissu anahitaji msaaada wa michango hawawezi kufika hata laki moja ndani na nje ya nchi? Kama laki moja wanafika inashindikana nini kupatikana walau hata million 50 mpaka wakati huu? Maana watu laki wakichanga mia tano tano inapatikana millioni hamsini. CHADEMA kubalini tu kuwa kwa sasa hamna wanachama wa kueleweka na wenye mapenzi mema na CHADEMA na ambao wanaweza kujitolea hela zao kumpa mtu kama Lissu anayetoa lugha za kibaguzi na chuki .
 
Wewe unalazimisha fikra zako ziwe ndiyo uhalisia,ndiyo hapo unapokosea na kwa vile moyo wako umeujaza chuki kwa Chadema basi kila kitu cha Chadema kwako wewe ni hasi tu. Anyway ni haki yako kuwaza lolote ndiyo demokrasia yenyewe ila tu usimuone mwenye fikra tofauti na wewe kuwa ni adui,ni mjinga,mpumbavu na siyo mzalendo. Sisi wote ni Watanzania hakuna asiyeipenda Tanzania kwani hatuna nchi nyingine zaidi ya hii lakini pia hatuwezi kufanana mitazamo na fikra. Relax usiumize sana moyo wako kwa chuki ukidhani kuwa ndiyo utaonekana unaisaidia CCM yako.
 
Wafuasi wa cdm huwa wanatoa kura na sio fedha. Fedha ni jambo la hiari. Na Lisu hataki fedha chafu, hivyo hizo atakazopata ni watu waliojifunga mikanda. Cdm sio chama Cha matajiri wauza unga kama wa ccm, Bali cha walalahoi.
Mkuu hivi kweli mbwembwe zote zile Lisu ni wa kukosa wafuasi laki 5 wa kuchangia elfu moja moja ili apate milioni 500 ya shangingi?
 
Mmeanza kugombana Chawa
 
Unasemaje? Huoni mpaka sasa yamechangiwa mamillioni kwa mamillioni? Hujaona pesa zinachangwa hadi millioni mia moja kwa mkupuo? Unafahamu walimu peke yao walichangia kiasi gani?
Leta ushahidi unapiga kelele mamilioni ya maneno bila ushahidi ni sawa na taarabu
 
We jamaa unahangaika na Chadema sana. Chama chenu mfu
We endelea kung'ang'ana na million10 ukifikiri wanachadema wamekwama! Tambua Kuna ambao hawahitaji kujitangaza! Na kwa taarifa yako wapo wanachadema wenye ukwasi walioupata kihalali na sio Kwa ufisadi kama wa ccm! Na ambao sio ajabu Kwa muda huu unaobwabwaja humu wewe Luka mshamba,gari imeshatolewa order kiwandani tena bullet proof! Na tunatambua ninyi ni wachawi,ikitua tu bandarini tunawekea uchawi proof!
 
Anae changiwa ni lissu au ni chadema? Em tuliza ubongo mkuu ushaambiwa na mdau henga chama chako!! Mchango wa lisu kawaomba wa tz wote hata wewe ukiguswa changia
 
Mkuu hivi kweli mbwembwe zote zile Lisu ni wa kukosa wafuasi laki 5 wa kuchangia elfu moja moja ili apate milioni 500 ya shangingi?
Huo ni mchango wa hiari sio kodi.
 
Sio kwamba hawana wanachama wa kutosha ila huo ni ushahidi kwamba hawakubaliani na utapeli huo wa kutaka kutumia kigezo cha kumchangia Lissu kumbe ni kutakatisha fedha chafu kutoka ughaibuni. Nani anajua exactly nani kachanga kiasi gani? Chadema ni watakatishaji Waziri sana wa fedha kwa njia hizi hizi za michango.
 
Chama chenye watu kama wewe wanaofanya analysis za kitoto kama hizi, ni chama ambacho kinaleta umaskini mkubwa kwa watanzania. hakifai kuendelea kuongoza nchi hii.
 
Chama chenye watu kama wewe wanaofanya analysis za kitoto kama hizi, ni chama ambacho kinaleta umaskini mkubwa kwa watanzania. hakifai kuendelea kuongoza nchi hii.
Ulichofanya wewe ni kupiga mayowe na siyo kujibu hoja.
 
CHADEMA mnaandikaga utafikiri mmepofuka akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…