Tazama ushahidi huu wa kimahesabu wa Michango ya Lissu Unaothibitisha CHADEMA haifikishi wanachama hata million Moja

Tazama ushahidi huu wa kimahesabu wa Michango ya Lissu Unaothibitisha CHADEMA haifikishi wanachama hata million Moja

Chama changu cha CCM Tayari kipo imara na madhubuti sana na ndio maana kinaendelea kubeba matumaini ya watanzania na kupigiwa kura za ndio katika kila uchaguzi,pamoja na kuendelea kuaminiwa.

Nimeshasema hapa kuwa tubishane kwa hoja na takwimu.weka hoja niweke hoja. Hao wanachama wenu mamilioni mnaosemaga mnao wapo wapi? Wamejificha wapi?

Chama Chako ?

Sikujua kama unamiliki Chama
 
Mwenyekiti wa ccm ni chama mshindani, hapaswi kuwa ni msimamizi wa tume. Wakati wa uchaguzi nchi inapaswa kuwa chini ya Jaji Mkuu, na sio chini ya rais ambaye anagombea urais. Matokeo ya mgombea yoyote ikiwemo urais yahojiwe mahakamani. Tume ya uchaguzi iondolewe Kinga ya kushitakiwa mahakamani kwa makosa ya kuharibu uchaguzi.
Wakati kampeni zinapofunguliwa Mwenyekiti, (CCM) huwa katika mchaka mchaka, na mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi yeye huwa center kumonitor both side, yeye husimamia zoezi mpaka mwisho.
-Mkuu wa tume ya uchaguzi / Mteuliwa Jaji Mkuu - angalia nafasi za hawa watu, kitaaluma.
-------
INFACTS TUNA MFUMO WETU KAMA TAIFA LA WATANZANIA.
 
Mambo ya chadema waachie wenyewe! Ukiona chadema ni nzuri na unahitaji mabadiliko ktk hiko chama basi chukua kadi kuwa mwanachama

Tulia na chama chako jenga chama chako, kosoa chama chako, kijenge chama chako!

Usingoje makonda aje akosoe ndio nawe utokeshimoni...!

Usingoje mwenyekiti wako aseme ndio nawe useme! Wakati huo akiwa kimya unamsifia ata kama amekosea!

Jenga chama chako, jenga taifa lako!

Chama chako kipo madarakani miaka nenda rejea, kina mapungufu kibao! Paza sauti kujenga nchi na chama

Kemea watendaji wazembe!

******
Wewe atakuwa mtendaji wanyumba kumi hakuna utafanya, ata ile kazi ya Anuani za makazi sijui kama ulifanya kwa ufanisi kwa namna unavyoishi katika hii platform!
Bora umempa za uso huyo mbogamboga anayetumia tumbo kufikiri badala ya kichwa
 
Lissu hakuchagulika 2020, hachaguliki 2025, na wala hatochagulika kuwa Raisi wa Nchi hii 2030....

Mbona hilo liko dhahiri?

Eniweyi...


Wamchangie utabibu wake wa Exposure Therapy.

Labda, narudia labda hapo afikiriwe kuwa Chief Negotiating Officer wa Mikataba chini ya Wizara ya Madini.
 
Ndugu zangu watanzania,

Ukisikia watu wanafiki,waongo,ndumila kuwili na walaghai basi ni wafuasi wa CHADEMA. Hadharani watakujaza upepo,kukuvimbisha kichwa,kukupa kiburi halafu kumbe nyuma ya pazia wana kucheka tu na kukuona kama sinema tu.

Wafuasi wa Lissu kinafiki na kilaghai walishamuaminisha na kumvimbisha kichwa Lissu kuwa wana mpenda na yeye akakubali kuwa anakubalika sana na anaweza hata kuwa Rais Wa nchi hii wakati hata wafuasi wake tu wanaona kamwe na katu hawezi kuwa Rais wala kiongozi wa ngazi ya juu.

Sasa tangia ameanza kuomba michango ya kununua gari la kifahari kwa ajili ya mizunguko yake imeshangaza na kusikitisha kuona mpaka sasa karibia wiki Ni watu 1673 tuuuuu ndio wameweza kumchangia Lissu hela. Hii ni aibu ,fedheha na jambo la kusikitisha sana tena sana.

Hii inaonyesha wazi na dhahiri Lissu hakubaliki kabisa ndani ya CHADEMA na wengi pengine hawakubaliani kabisa na aina ya siasa zake ,hasa lugha zake mbaya na chafu za kibaguzi na chuki kwa wale ambao hakubaliani nao . kama ambavyo amemshambulia Mheshimiwa Rais kwa lugha za kibaguzi na chuki.

Watanzania na wanachadema wametuma ujumbe bila kujali itikadi zao za kisiasa kuwa hawamuungi mkono lisssu na aina ya siasa zake za chuki na kibaguzi. Jiulize tu ndugu yangu Lissu ana wafuasi wangapi kwenye mitandao yake ya kijamii? Kwanini wamegoma kumchangia? Imekuwaje kati ya mamilioni ya watanzania ndani na nje ya nchi imeshindikana hata watu elfu tano tu yaani 5000 kupatikana kumchangia?

Maana mtu anayekupenda ,kukuunga mkono katika harakati zako na kazi yako ni lazima awe wa kwanza kujitoa na kukuchangia kwa hali na mali. Mfano mimi hapa nilipo ikitokea Rais Samia akasema anahitaji mchango basi ni lazima nitakwenda kuuza hata mahindi yangu ili tu nipate pesa ya kumchangia. Nitafanya hivyo kwa kuwa ninampenda na ninamuunga sana mkono kwa uchapa kazi wake,na utumishi wake unaogusa maisha yetu, mfano kwetu sisi wakulima ambapo tumefaidika na uongozi wake.

Sasa Lissu ndio afahamu ya kuwa hata uchaguzi wa 2020 hakuibiwa kura kama alivyokuwa akidai ,bali ni kuwa watanzania hawampendi na hawamkubali na kumuunga mkono kwa yeye kuwa Rais .kwa kuwa wanaona hatoshi hata chembe kushika nafasi hiyo.anaweza kuwa anafaa kwenye kazi nyingine lakini siyo kazi ya Urais maana hana sifa za Urais zinazohitaji mtu makini,mzalendo,mchapa kazi,mwenye maono,mtulivu,mwenye subira,msikivu,anayejuwa wakati gani aongee na wakati gani akae kimya,wakati gani afanye maamuzi na wakati gani avute subira,nini aongee awapo hadharani na kipi akae kimya.Urais unahitaji mtu mwenye hekima, busara,upendo kwa watu wote.

Urais unahitaji mtu mwenye chujio la maneno,mtu mwenye muunganiko mzuri wa akili na mdomo wake,mwenye kufikiri kabla ya kuzungumza na siyo kuzungumza ndio ufikiri,mtumweye uwezo wa kuwaunganisha watu wote bila kujali dini zao,makabila yao,kanda zao na hata jinsia zao. Urais unahitaji mtu mwenye kifua cha chuma japo ana moyo wa nyama na damu.

Urais hauhitaji mtu mropokaji, mkurupukaji,mwenye mihemuko,jazba,hasira,mwenye kuongea neno lolote lile linalomjia mdomoni pake au mtu mwenye kujiona ana akili kuliko watu wote,mtu asiye shaurika wala kukubali ushauri wa watu wengine. Urais hauhitaji mtu wakuwagawa watu kwa kusema hawa ni Maccm au Mapoliccm. Huyo hatufai hata kidogo.

Lissu amepelekewa ujumbe mzito sana na mchungu sana ambao utampa somo zitoo sana kama atahitaji kujifunza. Ni lazima sasa ajifunze na kubadilika.asijione ana akili sana kupita watu wote .

Lissu anazidiwa ushawishi na nguvu ya kukubalika hata na msemaji wa club ya Simba Ahmed Ally achilia mbali Ally Kamwe wa Yanga, ambaye huhamasisha mashabiki wake kuujaza uwanja wa Benjamini mkapa unaobeba mashabiki elfu sitini kwa viingilio vya kuanzia Elfu tano kwa viti vya mzunguko mpaka laki mbili kwa VIP A?

Ole wake apitishwe na CHADEMA kugombea Urais uchaguzi ujao kushindana na mama yetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hasssan ataona aibu atakayovuna katika sanduku la kura. Lissu Akipata kura hata laki moja Basi akachinje kuku ale.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
mwaka 2020 magufuli alipigiwa kura siku 2 kabla ya uchaguzi mkuu. hili lilitokea pale ofisi za ccm mkwajuni nilikuwepo eneo hilo na nilishuhudia vijana wale wakipewa wali kwa maharage na kuahidiwa bk 5000/ na hawajapewa mpaka uchao. haya yalifanyika mgombea akiwa lisu
TUTAMCHANGIA KULIKO KUCHANGIA MWENGE WA UHURU
 
..maana yake Watanzania wamepigika.
Hawajapigika bali hawapo tayari kuchangia ujinga wa kumnunulia mtu gari la kifahari na la mamilioni pesa kwa kazi ya kuzunguka tu. Wakati mtu na watu hao hao kutoka chama chama hicho hicho wamesikika mara nyingi wakipinga magari ya anasa na kifahari halafu leo tena wanataka gari la aina hiyo hiyo achangiwe Lissu. Ndio maana wenye akili Timamu wamegoma.
 
Hawajapigika bali hawapo tayari kuchangia ujinga wa kumnunulia mtu gari la kifahari na la mamilioni pesa kwa kazi ya kuzunguka tu. Wakati mtu na watu hao hao kutoka chama chama hicho hicho wamesikika mara nyingi wakipinga magari ya anasa na kifahari halafu leo tena wanataka gari la aina hiyo hiyo achangiwe Lissu. Ndio maana wenye akili Timamu wamegoma.

..kwani imeshaamuliwa gari gani anatakiwa kupatiwa?
 
Lissu amekivua nguo chama Chenu kwa kuonekana ni chama cha kibabaishaji kwa kukosa na kushindwa kumpatia gari makamu mwenyekiti wake.
Cdm sio chama kinachoungwa mkono na wauza unga, wakwepa kodi nk, bali ni chama Cha watanzania masikini. Na hakuna popote cdm inajivunia kuwa na uwezo wa kununua magari, bali kuwakomboa watanzania toka mikononi mwa chama Cha majizi, yaani ccm.
 
Cdm sio chama kinachoungwa mkono na wauza unga, wakwepa kodi nk, bali ni chama Cha watanzania masikini. Na hakuna popote cdm inajuvunia kuwa na uwezo wa kununua magari, bali kuwakomboa watanzania toka mikononi mwa chama Cha majizi, yaani ccm.
Unanikumbusha watu wanao ahirisha kufikiri kwa nafsi, (human herding).
 
Wakati kampeni zinapofunguliwa Mwenyekiti, (CCM) huwa katika mchaka mchaka, na mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi yeye huwa center kumonitor both side, yeye husimamia zoezi mpaka mwisho.
-Mkuu wa tume ya uchaguzi / Mteuliwa Jaji Mkuu - angalia nafasi za hawa watu, kitaaluma.
-------
INFACTS TUNA MFUMO WETU KAMA TAIFA LA WATANZANIA.
Huo sio mfumo wa watanzania, Bali ni mfumo wa kukibeba chama tawala. Pitia mapendekezo yote ya tume zilizoundwa kuelekea mfumo wa vyama vingi, na baada ya mfumo wa vyama vingi. Hakuna popote walipopendekeza mfumo wa uchaguzi uliopo, au muundo wa aina hii ya kiutawala.
 
Back
Top Bottom