TB Joshua hakuwahi kubatizwa wala kumpokea Yesu! Nimeshangaa sana

Huyo Mungu kazi yake kuzuia ulimwengu wenye mabaya au kwa sababu tu anao huo uwezo?
 
Heshima yako bwana kiranga ...
 
Thibitisha Mungu yupo, usiseme tu inawezekana yupo.
Sasa kwanini asiseme inawezekana? we jamaa unafurahisha sana nishakwambia hakuna uthibitisho ila bado umeshikilia tu kudai uthibitisho.
 
Sasa kwanini asiseme inawezekana? we jamaa unafurahisha sana nishakwambia hakuna uthibitisho ila bado umeshikilia tu kudai uthibitisho.
Kwa sababu, kujua kipi kinawezekana na kipi hakiwezekani kunaenda na uthibitisho.

Ukitaka kusema tu "inawezekana" unaweza kuzusha uongo wowote ukauwekea "inawezekana".

Inawezekana Magufuli hajafa.Bado anaishi Ikulu.

Inawezekana Tanzania si nchi ila watu wote wanaofikiri kuna nchi inaitwa Tanzania wanaota ndoto moja.

Inawezekana JF ina aliens kutoka Andromeda Galaxy wanafanya experiment.

Inawezekana mapiramidi ya Misri yamejengwa na Mfugale.

Inawezekana Joe Biden ni mjusi aliyejibadilisha kuonekana kama mtu.

Inawezekana Vingunguti kuna mtambo wa bomu la nyuklia uliowekwa kisiri na serikali.

Inawezekana kati ya Dar na Zanzibar hakuna bahari, yale ni mauzauza tu.

Inawezekana usiku tukilala tunaenda Malaga Spain.

Inawezekana majeshi yote duniani yana askari saba tu wanaotuchezea shere tuwaone wengi.
 
T.B Joshua.
Zaidi amelelewa na Mama yake, kwani Baba yake alifariki akiwa mtoto mchanga.
Mama yake Joshua alikuwa Mlokole na Joshua alisoma shule ya Msingi ya Kilokole yaani Kipentekoste.

Hivyo basi Mchungaji wa Mama yake ndio aliye Mbatiza T.B. Joshua.

Na kama baadhi walokole wa hapa Tanzania, T.B Joshua alivyopata ufahamu akaanzisha Kanisa lake la Synagogue.

Kuhusu kuwa Mwema.
Mwema ni Mungu peke yake.
 
Mbana una Amin Kuna electron na proton kwani ulishawah kuziona Ila nguvu zake unaziona
 
Huyo Mungu kazi yake kuzuia ulimwengu wenye mabaya au kwa sababu tu anao huo uwezo?
Tabia yake ya kuwa na upendo wote haipo consistent na ulimwengu wenye kuweza kuwa na mabaya kuwepo.

Ulimwengu huo ukiweza kuwepo,una violate hiyo tabia yake. Na kama Myngu huyo ndiye siupreme being mwenye uwezo wote, ujyzi wote na upendo wote, hawezi kuwa violated.

Tukiona ulimwengu wenye kuweza kuwa na mabaya umeweza kuwepo, maana yake Mungu huyo hayupo. Angekuwepo, ulimwengu unaoruhusu mabaya kuwepo usingekuwepo.

Mungu huyo hayupo. Kuwepo kwake ni hadithi tupu za watu tu.

Ndiyo maana mpaka leo hakuna anayeweza kurhibitisha yupo.
 
Neno "inawezekana" linaenda na uthibitisho? yani uwe na uthibitisho wa jambo halafu utumie neno "inawezekana"?
 
Mbana una Amin Kuna electron na proton kwani ulishawah kuziona Ila nguvu zake unaziona
Kwani wapi nimekwambia nataka kumuona Mungu?

Unaelewa hoja yangu?

Unaelewa sijapinga uwepo wa Mungu kwa sababu haonekani tu?

Unaelewa ninaposema Mungu muweza yote,mjuzi wa yote na mwenye upendo wote hayupo natumia hoja gani kufikia hitimisho hilo?
 
Neno "inawezekana" linaenda na uthibitisho? yani uwe na uthibitisho wa jambo halafu utumie neno "inawezekana"?
Wapi nimesemq hivyo?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Nakwambia hivi, kutumia neno "inawezekana" unaweza kutumia kwa uongo wowote. Hivyo, katika mazungumzo ya kutafuta ukweli na uongo, twende na uthibitisho.

Ukitaka kujificha katika kichaka cha "inawezekana" unaweza kusema inawezekana daraja la Salenda la Dar es Salaam linaunganisha mabara ya Asia na Ulaya ila sisi hatujui tu.

Usiishie kusema inawezekana.Thibitisha.
 
Kwani wapi nimekwambia nataka kumuona Mungu?

Unaelewa hoja yangu?

Unaelewa sijapinga uwepo wa Mungu kwa sababu haonekani tu?

Unaelewa ninaposema Mungu hayupo natumia hoja gani kufikia hitimisho hilo?
Kuona matokea yake huku dunian Ni udhibitisho kwamba yametokea kwa nguvu fulan Sasa hyo nguvu ndio Mungu , tatzo lako umesha jengo kichwan Mungu anatakiwa awe hivi au vile ndo maana unataka kudhibitishiwa Mungu unae mtaka ww kma fkra zako zinavyotaman Mungu awe hivyo
 
Kiranga Ninatamani nikuulize swali dogo tu,lakini usikasirike mkuu
Kwa nini unafikiri ushafikia uwezo wa kuniuliza swali la kunikasirisha?

Na utajuaje hapa nimekasirika na hapa nimepiga chafya tu kwa reflex action, nzi aliye karibu anaweza kufikiri nimekasirika, lakini kiukweli hana hata nguvu za ubongo zinazotakiwa kunikasirisha?
 
Hata uthibitisho unaweza kufojiwa na ukatumika kwa jambo ambalo si la kweli,kila neno lina maana yake na matumizi yake sasa jamaa katumia neno "inawezekana" sasa hayo ya kutumia hilo neno kwa uongo au kweli haimzuii yeye kutumia hilo neno.
 
Huyo Mungu kazi yake kuzuia ulimwengu wenye mabaya au kwa sababu tu anao huo uwezo?
Hizo tabia zake za kuwa na upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote z8nqp8ngana na ulimwengu wenye kuweza kuwa na mabaya kuwepo kqma vike shilingi ya Nyerere ukiirusha ikaangukia kichwa kunavyopingana na shilingi hiyo kuangukia mwenge.

The two are mutually exclusive.

Shilingi ikiangukia kichwa, maana yake haikuangukia mwenge, and vice versa.

Vivyo hivyo, ulimwengu unqoruhusu mqbaya kuwepo ukiwezekana kuwepo, maana yake huyo Mungu hayupo.

Huyo Mungu akiwepo, maana yake ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya haupo.

Ulimwengu unaoweza kuwa na mqbaya upo.

Hivyo, huyo Mungu hayupo.
 
Hiyo nguvu ni nini?

Una judge hiyo nguvu ni Mungu kabla ya kuijua hiyo nguvu ni nini?

Ukiambiwa hiyo nguvu ni gravity, utasema gravity ni Mungu?
 
Ameshazikwa?
 
Nimekuuliza huyo Mungu kazi yake kuzuia ulimwengu wenye mabaya? maana kama ni upendo hata binaadamu wanao upendo,ujuzi na uwezo.
 
Hata uthibitisho unaweza kufojiwa na ukatumika kwa jambo ambalo si la kweli,kila neno lina maana yake na matumizi yake sasa jamaa katumia neno "inawezekana" sasa hayo ya kutumia hilo neno kwa uongo au kweli haimzuii yeye kutumia hilo neno.
Sasa kama hata uthibitisho unaweza kufojiwa, utajuaje huu ukweli na huu uongo kabla ya uthibitisho?

Huoni kwamba kama hata uthibitisho unaweza kufojiwa, kauli inayotolewa bila uthibitisho unaweza kuficha uongo zaidi, na ili kuhqkiki kujua ukweli ni upi na uongo ni upi uthibitisho ni muhimu, kwa sababu moja ya kazi ya uhakiki ni kuangalia kama uthibitisho unaweza kufojiwa?

Yani hapo ulichosema ni sawa na mtu afungue duka, anauza vitu. Mchele, sukari, maharage, sabuni, mafuta etc.

Anataka kuuza vitu apate faida.

Halafu anasema, hata noti zinaweza kufojiwa, kwa hivyo atawapa watu vitu bure tu. Hakuna haja ya kulipia. Hata noti zinaweza kufojiwa.

Wakati, kiuhalisia, kwa ntu anayetaka faida kibiashara, ukweli kwamba hata noti zinaweza kufojiwa unatakiwa kuongeza uhakiki wa noti, si kuruhusu watu wachukue bidhaa bure kwa sababu hata noti z8linaweza kufojiwa.
 
Hebu tuliza akili.

Hivi mtu akikwambia inawezekana kesho ikanyesha mvua halafu kesho yake mvua isinyeshe utasema aliongea uongo? ndio maana nikakwambia kila neno lina maana yake na matumizi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…