Mkuu
matunduizi habari.
Mkuu
matunduizi jina lako linaweza kuwa linaongea mengi kuliko uliyosema umeyasikia.
Biblia katika Warumi 10: 9-10 inasema "
Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu"
Pia Biblia inasema katika mathayo 28: 19-20 kwamba "
Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati.”
Pia biblia inasema katika Marko 16: 15-16 kwamba "
Basi, akawaambia, “Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri Habari Njema kwa kila mtu. Anayeamini na kubatizwa ataokolewa. Asiyeamini atahukumiwa"
Hata bila kuingia ndani sana naomba kueleza kwamba mistari niliyoandika hapo inasisitiza kwamba:-
1. Kumpokea Yesu kama ni Bwana ni uamuzi binafsi ambao unaweza kuufanya ukiwa pekee yako au katika hadhara mfano kanisani au katika Crusades kama zinazoendelea wiki hii chini ya "Christ for All Nations - CFAN"
2.Ili kuukulia Wokovu unahitajika kuanza maisha ya uanafunzi wa Kristo kwa njia ya kusoma Biblia mwenyewe au kuwa chini ya kiongozi fulani wa kiroho mfano Mchungaji. Hili ni jambo lililowachukiza wachungaji wengi wa Nigeria kwavile T.B Joshua hakuwahi kuwa chini ya Mchungaji yeyote (Mentor) kama wao walivyokariri kwamba ni formula ya kiblilia ambayo hawajasema imeandikwa wapi?
3. Kubatiza kiblia i.e Immerse au kiswahili kuzika ni kitendo cha nje ambacho mtu mzima sio mtoto anaudhihirishia ulimwengu kwamba kwa kumpokea Yesu kama ni Bwana na Mwokozi wake amekufa katika dhambi na HIVYO BASi anaonyesha ishara ya kuuzika mwili wa DHAMBI kwa njia ya UBATIZO
Kwa uzoefu wangu wa kufuatilia mambo kiroho ya makanisa ya Nigeria, viongozi wengi wa kikristo wamekuwa na chuki binafsi na T.b Joshua kwa miaka mingi sasa. Wanachojaribu kukifanya ni kufuta "Legacy" aliyoiacha T.B Joshua.
Ahsante